Hivi kwanini sisi Watanzania tunapenda kutembea taratibu kama konokono?

Huku joto ukikimbia ni utatoka majasho kwaiyo inabidi utulize spidi ili usilowe jasho. Ulaya baridi kwaiyo inabidi ukimbie kimbie ili kupasha joto misuli vinginevyo ukisimama mda mrefu sehemu moja utajikuta umeshaganda kama barafu.
mkuu..hata mikoa yenye baridi kama mbeya,Arusha na Iringa watu wanatembea taratibu,nimeishi kote huko sijaona tofauti yoyote na Dar kwenye issues za kutembea taratibu.
 
Wakuu,

Nimetembelea nchi kadhaa za Ulaya na Asia, kule watu wanatembea haraka haraka sana kuwahi kwenye mishe zao, lakini huku kwetu watu wanatembea taratibu kama konokono.

Tatizo ni nini?

Acha mambo zako sio kila kitu lazima kuiga!!! No hurry in Africa!!!!! Na nchi inasonga mbele kwa mwendokasi!! Au unadhani unapotembea kwa mwendokasi ndo issues zako zinaenda kufanikiwa!!!!
 
Nilisha experience hiki kitu,siku ambayo sina mishe yoyote town huwa najivuta sana huku naangalia angalia bidhaa na watu,ila nikiwa na mishe ni vurugu mechi naona kama sifiki jinsi foleni isivyosogea.KWA HIYO MIMI KWA MAWAZO YANGU UKIMUONA MTU ANATEMBEA KWA KUJIVUTA VUTA JUA HANA SHUGHULI YA KUFANYA KAENDA KUPOTEZA MUDA TOWN na kinyume chake ni sahihi!!!
 
Ukianza tu darasa la kwanza au la pili unaanza kufundishwa methali zinazo discourage haraka haraka.

Haraka haraka haina baraka.

Mwenda pole hajikwai.

Simba mwenda pole ndo mla nyama.

Kawia ufike etc.

Nafikiri shida itakuwa inaanzia huku.
 
mkuu..hata mikoa yenye baridi kama mbeya,Arusha na Iringa watu wanatembea taratibu,nimeishi kote huko sijaona tofauti yoyote na Dar kwenye issues za kutembea taratibu.
Pilika za uchumi ndo zinachangia mtu kwenda kasi au slow. Hata wewe mwenyewe ukiwa kariakoo kama dili zako zimebuma utarudi ukiwa mpole sana huna haraka na mwazo chungu mzima. Ila sasa ikitokea dili zako zimelipa na unatakiwa urepoti maeneo mawili matatu tofauti mjini utaona kama mda hautoshi utatembea kasi kama radi kwa vile unajua ukichelewa kufika maeneo hupati hela mda ukiiisha. Kwaiyo ukiona wabongo wengi wapo slow siyo kwamba ni utamaduni wao ni vile dili zimebuma na wana mawazo, ukiona mtu yuko kasi ujue anawahi muda asije kuchelewa maeneo yake ya hela akakosa hela kwa sikuiyo. Ni swala la uchumi tu na mzunguko wa pesa, uchumi wetu bongo ni mdogo na watu wengi wameachwa dili zao zimebuma hivyo hawana cha kuwahi, ila wenzetu uko mbele uchumi ni mkubwa na watu wengi mno dili zao zimetiki hivyo ukiona wapo kasi ni kwamba wanawahi mpunga wasije wakachelewa maeneo yao wanakopatia hela. Ni ivyo tu wala siyo swala la rangi au joto au baridi.
 
Hahahaha!! aise umeongea ukweli mtupu mara ya kwanza kutoka nje ya Tz, asubuhi nilivyoamka nikatoka nje nikaona kila mtu anatembea haraka ikabidi nisimame kushangaa watu wanavyotembea haraka haraka mpaka nikamuuliza mwenyeji wangu kulikoni na kuniambia kuwa ndo walivyozoea.
 
Wabongo wengi hawana mishe yoyote kabisa, atembee haraka anawahi wapi.... anaamini mwenda bure si mkaa bure hivyo hutegemea kukutana na mishe yoyote njiani akaunga nayo.

Anaamka asubuhi anajiendea tu asionekane ameshinda nyumbani, ndo maana haishangazi watu kukutana njiani tu na wakaamua kukaa kitako kupiga stori masaa kadhaa.... akitoka hapo huyooo taratibu mwendo mdundo kusaka mishe au kijiwe kipya.
 
Ni kwel kabisa, sabab kubwa ni kuwa watu hawana kazi za kufanya wanategemea mishe za kusikilizia vijiweni, au hata kama wanafanya kazi unakuta hawazipend hawana moraly nazo..waanafanya ilimradi tu..
 
Wakuu,

Nimetembelea nchi kadhaa za Ulaya na Asia, kule watu wanatembea haraka haraka sana kuwahi kwenye mishe zao, lakini huku kwetu watu wanatembea taratibu kama konokono.

Tatizo ni nini?
Umenena mkuu.tatizo kuu lipo dar na sababu kubwa ni chipsi yai na ushamba wa smartphone
 
Sisi tunakwenda kuwa Dona Kantrii

Sisi tuna kila kituu(in his voice)

Sisi ni Matajirii

Tajiri anatembea, anakula taratibu. Tumeambiwa tutembee Kifua Mbereee, sasa utatembea kifua mberee ukiwa spidi!?
 
Kanuni yangu ninayotumia ni hii"walk 25 percent faster"
Kusema ukweli utembeaji wa mtu unaweza kueleza mengi sana kuhusu huyo mtu kuanzia mtazamo wake na uwezo wake wa kufikiri.
Ukiona mtu anatembea taratibu basi ujuwe hata mind yake ipo taratibu sana Katika kupambanua Mambo.Na hii ndo mana nchi za Bara la giza hazipati maendeleo.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom