TUPAMBANE SANA
Member
- Nov 21, 2018
- 29
- 26
Nasikitika sana kuona serikali inatulazimisha kuwa maskini. Ni ngumu sana kwa mfanyakazi kuwa tajiri kwa kutegemea kuajiriwa.
NSSF wanapokea kiasi cha asilimia 20 (10 kwangu + 10 mwajiri) hapo hapo Serikali nayo wanakata kiasi cha asilimia zisizopungua 25 mpaka 30 ya mshahara wangu kama kodi.
Sasa inafika Mahali nataka kujiajiri nifanye biashara zangu nashindwa kutokana na kuminywa sana.
Najifariji na pesa yangu iliyopo NSSF kwamba nitaichukua nikafanyie biashara nayo nakuta viongozi na wabunge CCM nao wameikodolea macho na tiyari wameshaiwekea pin kwamba siwezi kuichukua mpaka nifikishe miaka 55 ya kustaafu au 60.
Sasa najaribu kujiuliza Miaka 60 nitaweza kufanya biashara ya ushindani kweli? jibu ni hapana na pia kipindi hicho nguvu zimeshapungua.
Ombi langu kwa viongozi na wabunge Jaribuni tena kuangalia hili swala msituburuze sana jamani haki yangu nipeni yakwenu chukueni Msitumie wingi wenu bungeni mkafikiria kwamba sisi ndio tumewatuma mimi binafsi sipendezwi kabisa na ndio zenu Bungeni. Kila kitu nyie "ndio".
USHAURI KWA NSSF
Fanyeni mchakato wa kukopesha wanachama wenu kama mtu ana kiasi fulani cha pesa basi awe na uwezo wa kukopa angalau nusu ya kiasi alichonacho kwenu ni njia pia ya kukuza uchumi kwenu.
Najua mtakuja na majibu ya Marekani hawafanyi hivi. wala sehemu zingine hawafanyi hivi sasa huwa najiuliza kikiwa kizuri kwenu mnaanza kujitetea na sheria za nchi zingine. Sio kila kitu cha kuiga nasi tufanye klitu wao watuige.
Nikiacha kazi nipewe pesa zangu. Mnafanyia biashara hata kuongezeka haziongezeki hivi unakuja kunipa milioni 100 nina miaka 60 sii kutaka kuniletea mtihani. Ndio maana watumishi wengi wakistahafu ndio wanajenga nyumba na pesa ya kustafia.
Tanzania kuna vitu vingi sana ambavyo serikali wanaweza wakafanya na wala wasitegemee pesa za wanachama wa NSSF.
Mfano serikali kuwekeza kwenye matumizi ya gas kwenye magari madogo na uzuri gas tunazalisha wenyewe hakuna shida, pia kuwekeza kwenye miundombinu kama reli za majiji; mfano kuchukua abiria kutoka Kibaha mpaka Mbande, Mbande Mpaka posta, Gongo la Mboto mpaka Posta, Yombo mpaka Posta nakadhalika.