Hivi kwanini Serikali inashindwa kuwaendesha EWURA?

Hii EWURA wamrudishe yule mkurugenzi aliyesimamishwaga na PM.Bwana Felix Ngamlagosi naimani atatusaidia Sana.Maana Mpaka sasa Toka aondoke imepwaya Sana.
Acha kumsagia kunguni Mkurugenzi Mkuu wa sasa ambaye ni kichwa kizuri chenye elimu kutoka vyuo vikuu vikubwa vya USA
 
..ewura kama mamlaka ya udhibiti haitakiwi kuingiliwa na serikali ktk kutekeleza majukumu yake.

..wana taratibu zao za kufuata mpaka kufikia maamuzi ya kupandisha au kuteremsha bei ya bidhaa au huduma wanazosimamia.

..serikali inaweza kuwa-challenge ewura kama watakuwa wamekiuka sheria au taratibu zinazotakiwa kufuatwa ktk kufikia maamuzi na kutekeleza majukumu yao.
Inakula % sokoni ..huo ndo udalali wenyewe...yaani ni serikali ya energy Tanzania...je na walimu wawe na % ktk kila school fees inayolipwa.
 
EWURA ni mamlaka, haipaswi kuingiliwa na serikali kwenye kutimiza majukumu yake.

Swali ni je? Hawana justification za kupandisha bei? Kama wanayo, tatizo liko wapi? Serikali iseme ukweli, kwenye lita 1 ya mafuta kodi na tozo ni kiasi gani? Wasiwalaumu tu EWURA
Hapo kwenye kodi na tozo kwa lita moja ndipo ilipo siri ya bei kubwa ya mafuta hapa Tz ukilinganisha na nchi za jirani kama Zambia nk. Serikali imekimbilia kukamua wenye vyombo vinavyotumia hii nishati kama vile ni vyombo vya anasa bila kufikiri kwamba kwa kufanya hivyo itasababisha mfumuko wa bei kwa bidhaa mbalimbali na kumfanya mwananchi asiweze kumudu maisha.

Baada ya upandaji mfululizo wa bei za mafuta, kilichokua kinafuata ni kupanda kwa nauli au migomo ya vyombo vya usafiri na upandaji wa bei za bidhaa au kuadimika. Hilo lingeleta mkanganyiko kwa wananchi na kusababisha kelele kwa serikali.

Katika hayo mapitio ya hivyo "viashiria vinavyosababisha" kupanda bei ya mafuta, wajikite tu kwenye huo utitiri wa kodi na tozo, hakuna cha bei ya soko la dunia wala kingine zaidi ya hapo. Zambia nao wanatumia mafuta hayo hayo yanayotoka kwenye hilo hilo soko la dunia na yanapitia kwenye bandari yetu ya Dar es Salaam.
 
Acha kumsagia kunguni Mkurugenzi Mkuu wa sasa ambaye ni kichwa kizuri chenye elimu kutoka vyuo vikuu vikubwa vya USA
Hao wote ni wasomi wazuri na walifanya Kazi kwa Pamoja.Ni Bora Felix kama ilivyoelezwa Awali ya Kuwa alisamimishwa basi Mhe.Majaliwa kama alivyokuwa amemsimamisha arudishwe aendeleze Kazi na huyo msaidizi wake ambaye ni Kaimu mkurugenzi Kwa Sasa.
 
Umejibu kwa weledi na hekima sana. Acha kazi iendelee
 
Hapo kwenye kodi na tozo kwa lita moja ndipo ilipo siri ya bei kubwa ya mafuta hapa Tz ukilinganisha na nchi za jirani kama Zambia nk. Serikali imekimbilia kukamua wenye vyombo vinavyotumia hii nishati kama vile ni vyombo vya anasa bila kufikiri kwamba kwa kufanya hivyo itasababisha mfumuko wa bei kwa bidhaa mbalimbali na kumfanya mwananchi asiweze kumudu maisha.

Baada ya upandaji mfululizo wa bei za mafuta, kilichokua kinafuata ni kupanda kwa nauli au migomo ya vyombo vya usafiri na upandaji wa bei za bidhaa au kuadimika. Hilo lingeleta mkanganyiko kwa wananchi na kusababisha kelele kwa serikali.

Katika hayo mapitio ya hivyo "viashiria vinavyosababisha" kupanda bei ya mafuta, wajikite tu kwenye huo utitiri wa kodi na tozo, hakuna cha bei ya soko la dunia wala kingine zaidi ya hapo. Zambia nao wanatumia mafuta hayo hayo yanayotoka kwenye hilo hilo soko la dunia na yanapitia kwenye bandari yetu ya Dar es Salaam.
Hapa umenena hawa jamaa wamegeuza mafuta sehemu ya kuvuna pesa Kwa matumizi wanayoyataka bila kuangalia madhara yake.Hawajali mfumko wa Bei unaotokea, hawajali mabadiliko ya maisha yanayoleta umasikini zaidi.

Inakuwaje nchi yenye bandari kubwa na maliasili nyingi halafu haina vita inashindwa kubuni vyanzo vipya vya mapato.Hatukatai kuwa maendeleo ya nchi huletwa na kodi na tozo ila akili itumike na hizo pesa zinazokusanywa zitumike kweli kwenye vitu muhimu vya maendeleo sio matumizi ya kulipa a mishahara na posho nono kiasi watu wanaona raha kuzipandisha kila kukicha.Naleta maelezo ya hizo Kodi (tax) na tozo (levies);zao zilivyopanda maradufu halafu Titus Kaguo Kwa niaba ya EWURA anakuja kutudanganya eti Bei ya mafuta kwenye soko la dunia imepanda kumbe ni kukamua mwanachi bila kujali matokeo yaani hii nchi imekua ya ajabu mno.Inarudi kipindi kilee.....
 
OVER 15 TAXES AND LEVIES A MAJOR REASON FOR HIGH FUEL PRICES IN TANZANIA

The Energy and Water Utility Regulatory Authority (EWURA) on Tuesday August announced price caps for fuel for the month of September, indicating a new record in price increase.
According to the September cap rates, the price of petrol at the Dar es Salaam port has increased by Sh84, diesel Sh29, while kerosene sees its price jump by Sh18.
With the increase, consumers were required to pay Sh2,511 for a litre of petrol in Dar es Salaam, Sh2,291 for diesel, and Sh2,194 for kerosene.

Ewura attributed the upward trajectory to global crude prices.
But then later in the evening the same regulator made a sudden turn around by suspending the new prices until further notice.
However as motorists wait for the latest prices , I has been learnt that taxes, levies and charges imposed on petroleum products are a major reason for the high prices.
Before a liter of petrol reaches the final consumer, it will attract more than 15 different taxes, levies and charges which make up over 40 percent of the total cost.
The taxes include Wharfage, Railway Development levy, Customs processing fees, Weights and Measures fee, Tanzania Bureau of Standards charges, Tasac Charges, Ewura Fee, Fuel Marking, Demurrage costs, and Surveyors’ costs.
Others are Financing Cost, Evaporation losses, Fuel Levy, Excise Duty, Petroleum fee, charges payable to executive agencies, and Service levy payable to local government authorities (Wholesale) and service levy payable to local government authorities.
For example during the month of July, the CIF (Cost Insurance and Freight) for a liter of petrol that arrived at the port of Dar es Salaam was Sh1,162.
The final retail price after all the other margins have been factored in brought the costs to Sh2,405.
Tanzania imports 100 percent of the petroleum products in refined form

C&P
 
Umejibu kwa weledi na hekima sana. Acha kazi iendelee
Hakika.Nchi yetu inajengwa nasi Sote.Huyo Mzee Felix wangemrudisha tu,alipokaa nje naimani atakuwa na mawazo chanya na ataendeleza kazi alipokuwa ameishia na wenzake.Kazi iendelee
 
Hakika.Nchi yetu inajengwa nasi Sote.Huyo Mzee Felix wangemrudisha tu,alipokaa nje naimani atakuwa na mawazo chanya na ataendeleza kazi alipokuwa ameishia na wenzake.Kazi iendelee
mimi sidhani kama huyo Felix ndio mwenye uwezo kuliko watu wote Tanzania. Haya mawazo yaondoe. Tunachotaka kuona ni serikali kuindesha EWURA kwenye kazi zao sio wawe wanajipangia kila kitu.
 
Hakuna taasisi ya serikali itakuwa fully autonomous, yaani ina absolute power ya kufanya chochote, Hiyo.ni taasisi ya serikali chini ya wizara ya maji,japo kuna aspect ya Nishati.kwaakili ya kawaida kwakuwa majukumu yake ni udhibiti wa maswala nyeti yanayogusa raia moja kwa moja kama gharama za maji au nishati (mafuta,gesi,umeme etc) kuna wakati katika hali ya kawaida walitakiwa waombe muongozo katika kutoa bei mpya tena itakayozidisha ugumu wa maisha kwani watakaolaumiwa ni serikali kwa ujumla.kwa hili la juzi walichemsha kulingana na hali ilivyokuwa huku "tozo" kubwa zikilalamikiwa zishushwe,huku luku-property taxes, nk. Sasa wewe unakuja na 'nyundo' nyingine tena kali ambayo hiyo tena ndio itapandisha gharama zote za maisha.ule ungekuwa ni uchonganishi mkubwa kati ya serikali na wananchi wake as it was a very wrong timing,hata kama hesabu zinasoma hivyo,kuna maslahi zaidi ya kuangalia.

..ewura ina bodi ya wakurugenzi na management.

..mwenyekiti wa bodi anateuliwa na raisi. wajumbe wanateuliwa na waziri.

..mkurugenzi mkuu anateuliwa na waziri. Na anapatikana kutokana na mchakato wenye ushindani.

..wakurugenzi walio chini yake wanateuliwa na bodi ya wakurugenzi kupitia mchakato wenye ushindani.

..kwa hiyo kuna sauti au uangalizi wa serikali ktk utendaji wa Ewura.

..Hata hivyo Ewura inafanya kazi kwa mujibu wa SHERIA zinaelekeza utendaji wa mamlaka za uthibiti wa bidhaa na huduma.

..Nakubaliana na hoja yako kwamba matatizo yaliyopo yamechochewa na tozo na kodi tulizoletewa ktk bajeti ya 2021/22.
 
mimi sidhani kama huyo Felix ndio mwenye uwezo kuliko watu wote Tanzania. Haya mawazo yaondoe. Tunachotaka kuona ni serikali kuindesha EWURA kwenye kazi zao sio wawe wanajipangia kila kitu.

..ewura imekuwa ikiongozwa na kaimu mkurugenzi mkuu tangu felix ngamlagosi alipo ondolewa kwa maagizo ya Waziri Mkuu Majaliwa mwaka 2017.

..nakumbuka aliondoka kutokana na mgogoro wa IPTL ku-renew leseni ya kuzalisha umeme.

..Ewura wali-renew leseni huku serikali ikiwa mbioni kuwashtaki na kuwaweka kizuizini James Rugemalira na Habinder Singh ambao ni wamiliki wa IPTL.

..Kilichofuatia hapo ni Mkurugenzi Mkuu wa Ewura kuondolewa kazini kwa maelekezo ya Waziri Mkuu. Na tangu wakati huo Ewura imekuwa ikiongozwa na kaimu mkurugenzi mkuu.
 
Me taasisi zote sioni impact yake. Takukuru ni zero, Ewura ni zero, TRA ni takataka kabisa, TCRA ndio uuuuuuuwiiiiiiiiii.

Hizi mamlaka ni ngumu sana kuwa na ufanisi katika jamii ya watu wasasa wasio na maamuzi na wanazidiwa nguvu na tutaasisi tudogo kama polisi na CCM
 
Hata
..ewura imekuwa ikiongozwa na kaimu mkurugenzi mkuu tangu felix ngamlagosi alipo ondolewa kwa maagizo ya Waziri Mkuu Majaliwa mwaka 2017.

..nakumbuka aliondoka kutokana na mgogoro wa IPTL ku-renew leseni ya kuzalisha umeme.

..Ewura wali-renew leseni huku serikali ikiwa mbioni kuwashtaki na kuwaweka kizuizini James Rugemalira na Habinder Singh ambao ni wamiliki wa IPTL.

..Kilichofuatia hapo ni Mkurugenzi Mkuu wa Ewura kuondolewa kazini kwa maelekezo ya Waziri Mkuu. Na tangu wakati huo Ewura imekuwa ikiongozwa na kaimu mkurugenzi mkuu.
hata wewe unaweza kuwa mkurugenzi wa EWURA kwani EWURA ina nini cha ajabu basi kila mtu mwenye elimu anaweza kuwa.
 
Back
Top Bottom