Hivi kwanini Serikali haitaki kuelewa? Bunge lirudi hewani. Kama tatizo ni gharama, wataje bei tutalipa..

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Huu mjadala najua sio mpya. Lakini naweka viambatanishi vya Utafiti uliofanywa na unaorudiwa rudiwa kufanywa kila mara..

5.JPG


Yaani hayo mashilingi yote hapo juu yamekolea majibu chanya ya wananchi wanaotaka Bunge lionyeshwe ili tupate kujua hawa jamaa wanatuwakilisha kweli mjengoni au wanababaisha tu tufanye maamuzi mapya!

Ni hivi, pamoja na majibu ya kisanii ya waziri wa Habari ninayemheshimu, Dkt. Mwakyembe, kwamba eti taasisi au watu wenye uwezo wa kugharamia kurushwa LIVE kwa Bunge waende wizarani wapewe mchanguo (ilihali tunajua hizi ni sound tu), bado uhitaji wa suala la vipindi vya Bunge kwenda hewani LIVE ni mkubwa.

Sawa, kodi zetu mmekataa kutumia kutupatia habari ambayo ni haki yetu kikatiba, sisi watanzania kawaida hatuna hiyana na sio watu wa vinyongo, tunaomba mtutajie hadharani ni kiasi gani kinahitajika ili tuanze harambee...

Kama hamtaki semeni tu. Msituzungushe!
 
Muendelezo wa kulialia. Mshaambiwa nendeni wizarani mkapewe mwongozo... Hamtaki!
 
Kwa kweli ni bora gharama ziwekwe hadharani! Ili kama Kuna wazalendo wanaopenda kujua ama kufuatilia bunge waweze kuchangia..
 
Kuwa mwanamke mzuri na kichwani ukapewa akili ni moja ya zawadi alizokupa mwenyezi mungu hongera sana Dada kwa kuumbwa hvyo..
 
Back
Top Bottom