Hivi kwanini sauti za Mapadri kuendesha ibada zina fanana?

Jeceel

JF-Expert Member
Feb 6, 2018
1,446
2,000
Nilishawahi kumuuliza mtu wa dini hiyo akanikatilia sio maneno hata sauti
 

areafiftyone

JF-Expert Member
Jan 4, 2017
8,349
2,000
Bwana awee nanyiiiiiiiii
Awe piaaaaa naweeeee

Inueni mioyoooooo..

Mikoa zaidi ya sita nimeishi lakini sauti za mapadre wetu zina fanana je....na.muasisi wa hii sauti...na nini umuhimu wake? View attachment 897499
Ni swali zuri sana,ila naona kama limekaa kimtego mtego hivi.Unajua,Shetani ni mjanja sana.Yeye huwa akitaka kukushambulia anatengeneza kaufa tu,wala hahitaji mlango, ili kuweza kukushambulia.Shetani ukishaiga kitu chake tu,anajua you are weak spiritually,he attacks you!Haka ni kaufa!Nyufa hizi huwa zina tu cost sana.Ibada za underground societies zinatumia sauti za hivyo,na kwa Waroma si ajabu sana,maana Ujesuit ndio msingi wa Kanisa la Roma.Kumbuka kwamba Pope Francis ni Mjesuit.Sikiliza hizi ibada mbili za Kishetani,jibu utalipata!
 

amigod

JF-Expert Member
Mar 10, 2018
345
500
Huu ni utaratibu wao kwa dunia nzima padri kuwa na tune na tone zinazo karibiana na wanafundishwa hivyo wakiwa mafunzoni
 

laudate

Member
May 18, 2018
17
75
Bwana awee nanyiiiiiiiii
Awe piaaaaa naweeeee

Inueni mioyoooooo..

Mikoa zaidi ya sita nimeishi lakini sauti za mapadre wetu zina fanana je....na.muasisi wa hii sauti...na nini umuhimu wake? View attachment 897499
Siyo tune hiyo pekee, zipo tune nyingi zinazotumiwa na waendesha ibada hasa wakatoliki kama mapadre na maaskofu, hizo tune hasili yake ni kilatini hivyo makasisi wote ulimwenguni wa madhehebu ya kikatoliki hutumia hiyo tune/ melodia kwa kutumia lugha zao mama mfano kingereza, kiitaliano n.k ,hapa Tanzania tunatumia tune hiyo kwa kiswahili. Nawaza kusema ni tune ya kilitrujia ya ibada za kikatoliki. Ni tune za unyenyekevu ktk ibada pia inamfanya muumini hashiriki kikamilifu ktk ibada hasa ktk majibizano ya kiongozi wa ibada / kasisi na waumini.Zipo tune tofauti tofauti lakini maneno ni Yale yale, ukienda kanisa lolote duniani la wakatoliki maneno ya ibada ni hayo hayo, chakushangaza hata ibada za jumapili masomo ya maandiko matakatifu na mahubiri yake ni hayo hayo katika makanisa yote ya kikatoliki ulimwenguni, Yaani litrujia zao zipo uniform
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom