Hivi kwanini Rais Magufuli anawajali wanafunzi kuliko waalimu

Walimu wote walifeli, ikashindikana kabisa kusomea ualimu ndiyo wakaamua kwenda kusomea ualimu.

watu wa namna hii ni waoga na hawajiamini. wanashukuru hata kwa hicho kidogo wanachopata, maana hawastahili kabisa kwa jinsi walivyofeli.

angalia kenya ambako ili uwe mwalimu lazima ufaulu na kuna bodi ya kusimamia taaluma ya ualimu, huwa wanaidindia serikali
Na wewe ndo uwezo wako wa kufikiria unpoishia hapo.
 
Shida ya nchi hii ni moja tu, ukweli huitwa tusi. Hivi hili la ualimu ni kada ya waliofeli linahitaji mjadala? ndiyo mnalisikia kwangu kwa mara ya kwanza? nawatusi walimu ama nasema ukweli? aliyefaulu vzr kidato cha 6 (mf div 1) anaweza kweli kwenda kusoma ualimu? ualimu kabisa ktk nchi hii? hata bamedi hapendi ualimu. waulizeni watoto wenu majumbani na shuleni uone kama kuna hata 1 atatamani ualimu. si bora ukawa machinga.
Wewe kwanza una elimu ya kiwango gani? Isije kuwa tunafanya arguments na watu hawajasoma hata elimu ya lazima.
Ni kweli wapo wasioupenda ualimu kama ilivyo wengine wasivyopenda fani unayoipenda wewe lakini haimaanishi kuwa wanaosoma ualimu ni waliofeli labda uwe specific unaongelea level ipi.

Kuna watu nawafahamu wamefaulu kwa kiwango cha daraja la kwanza kabisa tena wengi tu na wanasomea ualimu. Mfano mdogo tu ebu angalia admission ya wanafunzi wa ualimu shule kuu ya elimu udsm halafu ndio urudi tena ku-comment hapa!
 
Back
Top Bottom