Hivi kwanini ni ngumu mke na mkwe kukaa pamoja?

dadysam

Member
Nov 15, 2016
48
39
Wakuu habari zenu
Moja kwa moja kwa topic hivi ni kwanini hili swala limekua gumu sana yamenifika wakikaa mbali kuna amani sasa iwe kaja au tumeenda likizo kwa bi mkubwa wiki moja tu amani inapotea nimejaribu kuuliza naambiwa hii kesi ipo sehemu kubwa ya mahusiano hivi tatizo nini hasa???
 
Kama kuna vitu mama yako anavikosa baada ya wewe kumuoa huyo mkeo lazima panuke,na Kama mkeo anaona mama yako ana nguvu sana kuliko yeye mke lazime pachimbike.
Mke asijue umpaacho mama yako,na mama asijue umekamatwa na mkeo
 
Siku zote wanawake wawili kuishi pamoja ni ngumu Sana, ikifanikiwa hua n bahati,
C hao tu wanawake hata ndugu tu mkubwa na mdogo wakikaa pamoja hawaelewan
 
Kwa nini mkwe asikae na mume wake au mke asikae na mume wake? Kwani wameoana hadi wakae pmj?
 
Kama kuna vitu mama yako anavikosa baada ya wewe kumuoa huyo mkeo lazima panuke,na Kama mkeo anaona mama yako ana nguvu sana kuliko yeye mke lazime pachimbike.
Mke asijue umpaacho mama yako,na mama asijue umekamatwa na mkeo
mara nyingi kinachokosekana hapa ni uelewa, mke akiona unamjali sana mama lazima ataona wivu na kwa mama vivyo hivyo lakini tunashindwa kutofautisha kwamba mama ananafasi yake ya kupendwa kama mama na mke pia ananafasi yake ya kupendwa kama mke
 
Kuna kipindi fulani kuna manzi mmoja alifikiaga home alikuaga mpenzi wangu wa utotoni bi mkubwa anamfahamu sababu tumecheza wote..siku nilipataga hela kidogo nikaenda piga misele wakati naondoka nikamuuliza mchuchu nikuletee nini ? Mchuchu alitaka mishkaki na ndizi basi bi mkubwa nimemuuliza nikuletee nini yeye alisema hataki kitu nimepiga misele nimerudi na mishkaki nikaona ghafla bi mkubwa kaingia ndani ila baadae alikuja niambia hata yeye mwenyewe hajielewi ila alisikia wivu balaa nimeletea yule manzi mishkaki nikamuuliza sasa mama wewe si nilikuuliza unataka nini ukakataa yani hakua na maelezo ya kutosha akabaki kusema roho tu imeniuma mwanangu maana wewe ni mtoto wangu mwenyewe wa kukuzaa halafu unamletea huyu mwanmke mishkaki hahaha hio ilikua ni 2012 nilicheka sana aisee
 
Kwa sababu wote ni wapendwa wetu hujui kipimo cha upendo ni wivu nasio kucheka na na kuchukulia poa
 
Mambo haya wanayaweza Wahindi na Waarabu,ngozi nyeusi hatuwezi.Halafu tangu lini wanawake wa Kiafrika wakapendana!?
 
Back
Top Bottom