Elections 2010 Hivi kwanini NCCR, TLP hawapatani na CHADEMA?

Mwanamageuko

JF-Expert Member
Oct 31, 2010
8,604
5,579
Kulikoni hapo jameni? Mbatia analia na Chadema!! Mzee wa Nji hii nae vivyo hivyo!! Hivi kwanini na wote wako jahazi moja?? kuna siri gani iliyo sirini hapo???:thinking:
 
Hawana uchungu na Tanzania wala vizazi vijavyo, wanaangalia matumbo yao tu na watakula nini leo.
 
na wengine ni ndumilakuwili.....chadema imewashtukia
 
Ahaa sasa je hiyo njaa iko pande zote ama ni upande mmoja?

Swali jingine:

Mhe. Mbowe 2005 alisema CHADEMA haiwezi kususa sherehe za kuapishwa kwa Rais, si sera ya CHADEMA na pia inaonesha si ukomavu wa kisiasa Je kwanini Mwaka huu wamezisusa?:smile-big:
 
Kwa sababu kiukweli hata kama ccm wasingeiba kura bado chadema wasingeshinda,ndio maana waliyakubali matokeo na kuhudhuria sherehe,lakini mwaka huu wamesema hawayakubali matokeo kwa sababu yanakasoro nyingi na ushahidi wa kutosha,hivyo kuhudhuria matokeo na sherehe za kuapishwa kwao ingekuwa unafiki kwani ingemaanisha wameyakubali matokeo,mm binafsi nawapongeza kwa hilo,kwani wangehudhuria wangekuwa ni wanafiki.unasema hutaki alafu ukipewa unapokea huo ni unfiki.,bravo chadema,bravo slaaaa
 
Mrema na Mbatia wote walikuwa NCCR kabla hakijasambaratishwa na Mrema na kuachiwa Mbatia kukiendesha; sijui wana siri gani waliyokuwa nayo kabla na baada maana hata Marando alisema alikuwa off kwa muda ule wote NCCR ilipokufa ikiwa chini ya Mbatia; sijui huenda kuna kitu kimejificha ila WOTE NI CCM B (wao kama wao)
 
Kwa sababu kiukweli hata kama ccm wasingeiba kura bado chadema wasingeshinda,ndio maana waliyakubali matokeo na kuhudhuria sherehe,lakini mwaka huu wamesema hawayakubali matokeo kwa sababu yanakasoro nyingi na ushahidi wa kutosha,hivyo kuhudhuria matokeo na sherehe za kuapishwa kwao ingekuwa unafiki kwani ingemaanisha wameyakubali matokeo,mm binafsi nawapongeza kwa hilo,kwani wangehudhuria wangekuwa ni wanafiki.unasema hutaki alafu ukipewa unapokea huo ni unfiki.,bravo chadema,bravo slaaaa
Tatizo hapo ni Kumbukumbu, HAWAKUWAHI KUPIGWA KUCHA NA CCM, KUCHA ZILIKUWA ZIKIKITA KWENYE NCCR NA CUF, Sasa ndio imekuwa zamu yao wamejua IUMAVYO.:smile-big:

Lakini je hakuna vita binafsi humo???
 
wanalia kwa wivu wa kijinga, Sio TLP NA NCCR tu, pia CUF wao wamekua wakijitokeza hadharani kabisa kuipinga CHADEMA, ILA WOOTE HAWATAWEZA
 
Mbatia na Mzee wa Kiraracha wanaendeshwa na maslahi binafsi ya kuwanufaisha wao na familia zao tofauti na CHADEMA wanaendeshwa na maslahi ya nchi na mustakabali wa maendeleo ya nchi yetu.
 
Ukitaka kujua ukweli kuhusu 'kuhasimiana' kwa NCCR-Mageuzi na CHADEMA rejea mambo kadhaa katika historia ya vyama hivi. Kwa machache ninayoweza kuwahabarisha hapa ni kwamba;
  1. Waasisi wa chadema ni miongoni mwa watu wa awali kabisa waliohusika na uanzishwaji wa NCCR wakati huo ikiwa kamati kabla ya kugeuka kuwa chama cha siasa pale mfumo wa vyama vingi uliporejeshwa nchini. habari kutoka ndani kabisa ya makundi haya zinasema kwamba, maneno demokrasia na maendeleo yalikuwa kaulimbiu ya awali kabisa ya NCCR, na hadi leo maneno hayo yanaonekana katika logo ya chama hicho. Ilitokea wakati fulani kwamba Mzee Mtei aliishauri kamati ya NCCR iitwe Chama cha Demokrasia na Maendeleo kwa kutumia ile kaulimbiu, lakini ushauri wake haukutumika badala yake akalitumia hilo wazo kuanzisha chama kipya pembeni, yaani CHADEMA ya leo.
  2. Waasisi wangine wa NCCR ambao leo ni watu muhimu sana katika CHADEMA, mf.Prof Baregu, waliondoka NCCR baada ya Mrema na Marando kukipasua chama katikati.Waliondoka hapo wakiiona NCCR kama jahazi linaloelekea kuzama, kutozama kabisa kwa NCCR nadhani ni kwa mshangao wao hadi leo.
  3. Kuna kundi kubwa la wanachama wa CHADEMA ambao waliondoka NCCR kutokana na kutoelewana na Mwenyekiti wa sasa wa chama hiki, J.Mbatia.Orodha ya hawa ni ndefu, kuanzia kwa marehemu, Chacha Wangwe, Komu na wengineo. Mkitaka kujua hili mwulizeni aliyehama hivi karibuni, Mhe.Selasini Mbunge mpya wa Rombo. Wote hawa matarajio yao ni anguko kubwa la NCCR, lakini ajabu bado inadunda japo kwa kuchechemea.
  4. Mbatia na Mbowe hawaivi kihivyo, hasa hasa kwa sababu Mbatia alimpinga hadharani Mbowe wakati akiwania Ubunge kule Hai mwaka 2000, ambapo (huenda kwa sabau hiyo)Mbowe hakufanikiwa
  5. Kifo cha Wangwe ndio kiliharibu zaidi, hata yale makubaliano ya ushirikiano yaliyosainiwa kati ya vyama hivi (pamoja na CUF na TLP)yakafa.
  6. Vijineno vingi vya kutotakiana heri vimekuwa vikiendelea kati ya vyama hivi. Mfano wakati Zitto aliwambia wakazi wa Tanga kwamba NCCR imekufa, Sungura wa NCCR aliibatiza CHADEMA aka ya Chagga Development Manifesto. CHADEMA nao hivi karibuni wamejibu, ati NCCR sasa ni NCCR-Manunuzi!
Kwa maoni yangu wote ni watafuta tone lile lile, hakuna anayetaka kuona mwenzake kapata yeye kakosa.
 
kulikoni hapo jameni? Mbatia analia na chadema!! Mzee wa nji hii nae vivyo hivyo!! Hivi kwanini na wote wako jahazi moja?? Kuna siri gani iliyo sirini hapo???:thinking:

wenyeviti wa chadema, tlp na nccr wote ni wachagga lakini hawapatani kwasababu wanatoka sehemu tofauti kama mrema ni mmrangu, mbatia ni mkibosho na mbowe ni mmachame na kiasili makabila haya huwa hayaivi ktk chungu kimoja!!!

ni jambo la kusikitisha sana upinzani wetu umejikita chini ya viongozi wa kutoka eneo moja na wasioelewana sasa kuitoa ccm madarakani itakuwa ni ndoto labda kama wapinzani wafanye mabadiliko makubwa ya kuondoa uongozi wa vyama vyao toka kwa wachagga na kusambaza uongozi mikoani badala ya kubaki kilimanjaro tu!!! Hii itasaidia kuondoa hisia kuwa chadema na wenzao ni vyama vya wachagga!!!
 
Hata Lipumba nae ni mnyamwezi wa kilimanjaro ndio maana cuf nao hawapatani na chadema.
 
Sahihisho: Mbatia ni wa Kutoka Kirua
 
Hata Lipumba nae ni mnyamwezi wa kilimanjaro ndio maana cuf nao hawapatani na chadema.

Mwambie huyo Tanzania Kwanza mbona analysis yake imekomalia uchaga ameacha CUF km kweli na CUf pia wachaga aseme.. ila kwa kifupi naona km hana hoja ya msingi
 
wenyeviti wa chadema, tlp na nccr wote ni wachagga lakini hawapatani kwasababu wanatoka sehemu tofauti kama mrema ni mmrangu, mbatia ni mkibosho na mbowe ni mmachame na kiasili makabila haya huwa hayaivi ktk chungu kimoja!!!

ni jambo la kusikitisha sana upinzani wetu umejikita chini ya viongozi wa kutoka eneo moja na wasioelewana sasa kuitoa ccm madarakani itakuwa ni ndoto labda kama wapinzani wafanye mabadiliko makubwa ya kuondoa uongozi wa vyama vyao toka kwa wachagga na kusambaza uongozi mikoani badala ya kubaki kilimanjaro tu!!! Hii itasaidia kuondoa hisia kuwa chadema na wenzao ni vyama vya wachagga!!!

Crap :nono:
 
Back
Top Bottom