Hivi kwanini mwanaume ukitaka kuoa unapapatikiwa sana na wanawake?

tang'ana

JF-Expert Member
Apr 3, 2015
11,809
15,059
Habari za siku nyingi enyi walipa kodi wenzangu?

Kuna issue nimekua naifanyia observation kwa muda mrefu sana lakini sipati majibu, kuna hii tabia ya wanawake hasa hawa wa hapa kwetu Tanzania.

Yaani wakishasikia tu mwanaume fulani yuko kwenye process za kuoa basi wataanza kujigonga kwake ili tu na wao waonekane wapo au kama unakuta mwanamke mwingine alikua ni X wako na mna miaka kibao hamjawasiliana lakini akipata taarifa tu unaoa basi lazima nae aanze usumbufu.

Hivi lengo lao huwa ni nini hasa au ni ili kuharibiana tu?
 
Aiseeeeee nimecheka sana nakumbuka wakati niko hatua za mwanzo za ndoa nikawa nashangaa mbona kama zilipendwa wangu wameunda kikundi cha mshikamano maana walirudi kama wameambiana vile nakajua kweli nakoelekea kugumu na bado hata ukiwa kwenye ndoa lazima utagundua kuna aina fulani ya wanawake wataanza kukomaa na wewe tofauti na mwanzo.
 
Hamna la maana uoe usiolewe kawaida tu na kuna adhabu ndani yake unatakiwa uishi kinafiki tu ili umridhishe mwenza ndio maana michepuko haishi.
 
Aiseeeeee nimecheka sana nakumbuka wakati niko hatua za mwanzo za ndoa nikawa nashangaa mbona kama zilipendwa wangu wameunda kikundi cha mshikamano maana walirudi kama wameambiana vile nakajua kweli nakoelekea kugumu na bado hata ukiwa kwenye ndoa lazima utagundua kuna aina fulani ya wanawake wataanza kukomaa na wewe tofauti na mwanzo.
Sijui huwa wananusa, au wanajuaje. Alaf ni kama vile upepo maana wanakuja wote kwa pamoja,wanajifanya kukusalimia.
 
Ukiwa na msichana au mwanamke na wao wanataman kujua au kukipata kilichomshawish mwenzao kukubali kuolewa na wewe
 
Back
Top Bottom