Hivi kwanini mwanamke upenda kutoa siri za mwanamme wake na kufananisha wanaume

Changes boy

JF-Expert Member
May 17, 2017
552
362
Tusaidieni wanawake, kwanini mnapenda kutoa siri za mausiano ya kwako na mwanamme wako kwa watu ambao hawajui mausiano yenu Bali kwa kusikia.
Mara nyingi uchangia kuvunjika kwa mausiano maana Leo ulikua na tabia hizi kesho unakua na nyingine kutokana na ushauri wa rafiki zenu.
Unakuta mdada kaishaumizwa Mara kibao kila akikutana na mwanamme mwingine anaona kama walewale, kunawengine mwanamme wanakua na uvumilia ila uvumilivu ukiwashinda wanasepa na kunawale hawawezi vumilia kidogo tu anasepa.
Wanawake badilikeni? Hivi ndio sababu kubwa kwa kuachwa kwenu na wanaume.
Utajiremba kila urembo, utavaa kila mavazi, uko nzuri sana lakini kuna tabia mwanamme hawezi vumilia hata uweje atasepa, tena bora akuage kunawengine kimyakimya
 
Dah nishawahi ku Date na Redio mbao ikawa inanipaka kinoma kwa wana. Sema nashukuru niliitema, that time nilikuwa ndio najifunza mapenzi.. Very decent nikaonekana kolo!
 
Ndo wameumbwa hivyo wengi kama sio wote.

Ila kwa mwanamke anaejielewa hawezi fanya hayo na kama akifanya ni kwa mipaka.

Wanawake tumeumbiwa wengi ili tuchague yupi anafaa na yupi hafai.sio kujizolea tu.

Kama unadate na dada wa vibarazani,vigodoro na stori za saluni tegrmra hayo mambo.

Ila ukweli wanawake wengi sana hulka zao ziko hivyo.lazima watakuwa na marafiki zao wanaoshare mambo yao ya siri.

Kwa anaejielewa atakuwa anashare vitu vya kawaida sana.

Hapo ndo wanaume tuwe tunafanya mazuri mana ukifanya baya limefika kwa jirani kupitia mkeo.mwanamke na siri hawawezani.

Jamaa kuna jambo la siri alimwambia mkewe akawambai usiiseme siri hii napesa hiii hapa itunze siri(1M) mwanamke akakubali.siku chache mbele Mwanamke akapatwa na ugonjwa usiojulikana akapelekwa spitali na mume.
Dokta akamfanyia vipimo akamwambia mbona uko sawa? Dada akasema dokta niitie mume wangua.mume akaitwa alipokuja yule mke akamuambia mumewe"mume wangu milioni yako hii hapa nimeshindwa kuitunza siri yako usije niua kwa presha bure".

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nyongeza
 
Attachments

  • Screenshot_20190414-150833~2.png
    Screenshot_20190414-150833~2.png
    175.5 KB · Views: 34
Wanawake wanao dekezwa dekezwa ndio huwa ivyo,ukidate na demu kilegelege kumdekeza dekeza full ujinga wa kubebishana ki dar.Lazima akupande kichwani kukufananisha na upuuzi aliopitia kukusema kwa marafiki zake,kwa umma.Ila ukimpeleka kijeshi kiume hawezi kufanya mambo ya kipuuzi kwanza hatakua na muda huo pili itakua aibu kwake kwakuwa marafiki zake watamwona kakalia kuti kavu😎😒.
 
😂😂😂asante mkuu
 
kumpeleka kijeshi namuonea huruma halafu wanaiga na Mimi nitapelekwa kijeshi. Ikifika hivi nitapata shida
 
Wameumbwa hivyo wachache sana wako kimya.......tena wachache mno.....wanajielewa.....ila na hao wachache mkimwagana atapayuka hata ya sirini.........
 
Ndo wameumbwa hivyo wengi kama sio wote.

Ila kwa mwanamke anaejielewa hawezi fanya hayo na kama akifanya ni kwa mipaka.

Wanawake tumeumbiwa wengi ili tuchague yupi anafaa na yupi hafai.sio kujizolea tu.

Kama unadate na dada wa vibarazani,vigodoro na stori za saluni tegrmra hayo mambo.

Ila ukweli wanawake wengi sana hulka zao ziko hivyo.lazima watakuwa na marafiki zao wanaoshare mambo yao ya siri.

Kwa anaejielewa atakuwa anashare vitu vya kawaida sana.

Hapo ndo wanaume tuwe tunafanya mazuri mana ukifanya baya limefika kwa jirani kupitia mkeo.mwanamke na siri hawawezani.

Jamaa kuna jambo la siri alimwambia mkewe akawambai usiiseme siri hii napesa hiii hapa itunze siri(1M) mwanamke akakubali.siku chache mbele Mwanamke akapatwa na ugonjwa usiojulikana akapelekwa spitali na mume.
Dokta akamfanyia vipimo akamwambia mbona uko sawa? Dada akasema dokta niitie mume wangua.mume akaitwa alipokuja yule mke akamuambia mumewe"mume wangu milioni yako hii hapa nimeshindwa kuitunza siri yako usije niua kwa presha bure".

Sent using Jamii Forums mobile app

Hii imenikumbusha kisa kimoja nilihadithiwa na rafiki yangu muda mrefu kidogk, ni kisa cha masikitiko, kama kilitokea kweli au laa siwezi jua ill kinayo mafundisho mawili, moja tusijichukukie sheria mkononi au tuwe na subira na pili ndiyo hilo la wanawake kukosa moyo wa kaba.

Jamaa mmoja alikuwa na mkewe wamekaa nje ya nyumba yao kibarazani muda huo akatokea mtoto wa jirani na kipande cha mkaa akachora ukuta wa nyumba ya huyo jamaa kwa ule mkaa, ( si unajua mambo ya watoto), yule jamaa kwa hasira alimrushia fimbi ikampata kichwani yule mtoto akaanguka na kupoteza maisha lakini hakuna aliyeona hilo tukio mbali ya wao wawili- wakashauriana kuchukua mwili na kwenda kuuzika katika uwa ( back yard) wa nyumba yao na wakala yamini kutunza siri.

Yule jamaa akaenda kwa baba yake na kumueleza tukio hilo baada ya majirani kuhangaika huko na huko kumsaka mtoto wao na baba yake akamshauri; - "haraka fanya juhudi nenda peke yako kwa siri kafukue hiyo maiti na uizike mahali pengine na kachimbe shimo la taka pembeni mwa hilo shimo ulilofukua hiyo maiti na iwe siri yako bila mkeo kujua", yule jamaa akatekeleza kama alivyoambiwa na baba yake.

Ikapita miaka, lakini kila ikatokea mtafaruku kati ya huyo jamaa na mkewe, mkewe huchukua tukio lile la mauaji kama fimbo ya kumchapa huyo mumewe na humwambia:- "mimi nitasema wewe ndiye ulifanya yale mauaji", kwa hali hiyo yule jamaa alikosa raha kabisa, na kwa kuona hali hiyo yule mke akawa kapata silaha kubwa ya kutumia dhidi ya mumewe panapotokea kutokuelewana kati yao.

Sikumoja ukatokea ugomvi kati yao na yule mwanamke akaropoka kwa sauti hiyo kauli yake akajisaha kwamba majirani walikuwa wakiwasikiliza pindi walipokuwa wakigombana, loo siri ikawa imevuja na maramoja mama na baba wa yule mtoto wakaenda polisi kutoa maelezo na muda mfupi tu karandinga ikafika yule mama na mumewe wakaswekwa ndani kwa uchunguzi-- yule mama alipominywa na polisi akataja kila kitu, yule jamaa akakomaa akipinga maneno ya mkewe akisema kuwa mkewe kuna wakati hurukwa na akili kwani lile shimo analosema walimzika yule mtoto lilikuwa shimo la taka na baadaye walilifukia baada ya kujaa.

Polisi kitengo cha upelelezi (forensic) walikwenda kwenye eneo la tukio na kuanza kazi ya kufukua ili kuona kama kuna masalia ya mifupa, hawakukuta kitu isipokuwa takataka tu licha ya kufukua kwa siku tatu mfululizo.

Lakini jamaa na mkewe walisota rumande miaka kadhaa na baadaye yuke mume kuachiwa kwakuwa ushahidi ulikosekana na yule mke kufungwa kwa kutoa ushahidi wa "UONGO".

Hayo ndiyo mambo ya wanawake.
Jamaa aliokoka kutokana na hekima na busara za baba yake.
 
Back
Top Bottom