The Humble Dreamer
JF-Expert Member
- Oct 12, 2015
- 7,442
- 10,233
Wakuu Salaam;
Hawa watu wanaosimamia idara ya rasimali watu wanatakiwa watambue kua wao nao ni binadamu kama watu wengine na lazima waheshimu utu wa mtu yeyote achilia mbali hadhi ya huyo mtu.
Hawa Hr's wa kampuni hua na majibu ya hovyo sana wawapo kazini bila kujali anamjibu nani.
Leo nimeenda kuulizia tenda kwaajili ya kuleta mazao fulan kwa hiyo kampuni kwaajili ya kutengeneza vyakula vya kuku, nikaambiwa Hr ndiyo yupo kwa leo, ile kuonana nae tu akaniambia 'kaa hapo'. Kwa hii kauli nilitaka nivue kiatu changu nimzibue nacho nikajizuia. Nikajikaza kukaa dakika 2 nikaondoka zangu bila kumwelezea kwa upana biashara yangu na nia ya kufika kwenye kampuni. Hajajua Mimi nikileta mazao kampuni mwao ndiyo bidhaa zao zikiuzwa wanakuja kulipwa badaye mishahara.
Kufika nje nikamwelezea mfanya kazi mmoja akanishauri nimsubiri Mkurugenzi mwenyewe. Mfanya kazi akanieleza kua kwa saivi wanahitaji mzigo kwani stock inakaribia kuisha.
Huyohuyo mfanyakazi akaniambia hata wakati akiomba kazi na hata wengine pia walipata shida sana kwa huyo HR kusajiliwa.
Sasa nikajiuliza HR kiburi anatoa wapi wakati ilikua ni bahati mbaya tu kumkuta yeye?
Nyie HR specialists na HR managers msione hizo kampuni ni zenu, Bali toeni Huduma kwa jamii kwa weledi na kuheshimu utu wa mtu kwani wote tuko kwenye utafutaji.
Je, wewe binafsi Ulishawahi kukereka na HR kwa lolote?