Hivi kwanini lugha ya kingereza haitiliwi mkazo nchini mwetu?

Kila raia wa nigeria akishika sh 1 jumla unapata million 190. Wana GDP kubwa kwasababu wapo wengi ila hamna wanachozalisha, we unajua bidhaa ngapi za kinaijeria? Elimu ya kiingereza ingekua inawasaidia tungekua na magari, treni au piki piki za kinaijeria lakini hakuna. Wahindi wanaleta bajaji na kiingereza hawajui. Wanaijeria wapo wengi ndomana GDP yao kubwa.
Mkuu umeongea point sana, nimekuelewa aisee
 
Mwanangu alisomea English medium akapata matokeo mazuri la 7 serikali wakamchagua secondary ya kata siku alipoanza class wale waliotoka shule za serikali majority hawakujua kuhesabu 1-100 in English! Mwanangu alishangaa sana, akawa darasani anaulizwa sana na wenzake mwalimu ameongelea nini?
Bila jitihada za kumwamisha shule angedumazwa pale kwanza uhaba ni mkubwa sana.
Kiujumla hali ya Elimu nchini ni mbeya sana hususan walimu na mitaala, hivi kwanini shule zote zisiwe kwenye kiwango cha English medium?
Kwa style tuliyo nayo tutaendelea kuajiri na kusimamiwa na wakenya kwa miongo mingi!

Sent using Jamii Forums mobile app
Mbona wapo form 4 kabisaa wasiojua kitu
 
Tatizo sio Kiinngereza wala sio Kiswahili. Tatizo ni kuwa na viongozi wasiokuwa na maono. China kwa maono yao walikumbatia kichina - hadi sasa wako mbali sana. Tanzania hatuna mwelekeo kila baada ya awamu tunaanza upya.
Ujamaa na kujitegemea - tuliwahi kujitegemea lini?
Ruksa - anayetaka kula chura na ale
Ubinafsishaji - mali za taifa zikauzwa kwa bei ya kutupwa
Maisha bora kwa kila mtanzania - mwendelezo wa kufirisi mali za taifa
Na sasa yanayoendelea tunayaona wote. ... \\
Kwa staili hiyo hatuendi kokote, kiingereza hakitusaidii maono ya kitaifa ndo yatatusaidia.
 
As you continue this obvious debate, we are concluding a big franchise agreement or deal) with a major franchisor in the US here in Dar es Salaam for a very big business deal. This is only possible if you are conversant with what English entails. Right? Peleka mtoto wako English Medium achana na wajamaa hao!!!???
 
Kwanini tusisome tu kiswahili mpaka mwisho? Kiingereza hakina faida yoyote ile, wanaijeria wanaongea kiingereza, Ghana wanaongea kiingereza lakini kati yao hakuna hata aliepiga hatua ya maana kimaendeleo, kinachosaidia kwenye elimu ni yaliyomo( content) sio lugha inayotumika. Swala la Bunge la afrika mashariki kusaili watu kwa kiingereza wacha wafanye tu. Bunge lile lipo kwa ajili ya diplomasia ni kama balozi wa Tanzania nchi nyingine. Halina athari yoyote kimaamuzi kwa watanzania, kwahiyo wale wanaojua kiingereza waende tu. Ila hapa kwetu mtu asitukanwe kwa kutojua kiingereza, wala asisailiwe kwa kiingereza. Kujua kiingereza hakusaidii uchumi, zaidi kimasaidia diplomasia na mazungumzo ya hapa na pale.
Tukomae tuwe na content nzuri kwenye elimu yetu sio lugha.
Lazima kuna areas ambazo hao wanaijeria na waghana watakua wanatuzidi !!! Tusidanganyane wala tusifarijiane kuna maeneo usipojua kiingereza utakwama !!! Mfano nafasi za Nazi nyingi watz wanakosa kwasababu ya poor English command tusijifariji!!! Mfano hotel nyingi za kitalii za Tanzania wamejaa wakenya na waganda Kwa kuwa ungenge unapanda watz wanazikosa hizo nafasi!!! Ukienda South Africa walimu wengi wanatoka Kenya na Ug !!! Kwa kifupi sisi watz hatukijui kidhungu kuanzia wasio soma mpaka maprofesa tuache sababu za kitoto
 
Kwanini tusisome tu kiswahili mpaka mwisho? Kiingereza hakina faida yoyote ile, wanaijeria wanaongea kiingereza, Ghana wanaongea kiingereza lakini kati yao hakuna hata aliepiga hatua ya maana kimaendeleo, kinachosaidia kwenye elimu ni yaliyomo( content) sio lugha inayotumika. Swala la Bunge la afrika mashariki kusaili watu kwa kiingereza wacha wafanye tu. Bunge lile lipo kwa ajili ya diplomasia ni kama balozi wa Tanzania nchi nyingine. Halina athari yoyote kimaamuzi kwa watanzania, kwahiyo wale wanaojua kiingereza waende tu. Ila hapa kwetu mtu asitukanwe kwa kutojua kiingereza, wala asisailiwe kwa kiingereza. Kujua kiingereza hakusaidii uchumi, zaidi kimasaidia diplomasia na mazungumzo ya hapa na pale.
Tukomae tuwe na content nzuri kwenye elimu yetu sio lugha.
Tanzania tunaanzaje kuwashinda Ghana na Nigeria? Hayo ni mataifa makubwa yanayojulikana duniani Tanzania tuko kundi la Burundi, commoro nk, lugha ya kingereza ni muhimu na ni silaha kubwa sana kuelekea Mafanikio
 
Huwezi kuuza sokoni kisichotakiwa na wateja. Sijawahi kuona shule binafsi (za watu mmojammoja au kwa pamoja, mashirika ya dini, mashirika ya kimataifa na kadhalika) zinazofundisha kwa lugha ya kiswahili kutoka chekechea mpaka darasa la saba na kuendelea. Wanajua kwamba Kiswahili hakitakiwi na wateja. Anzisha shule ya namna hiyo uone kama utapata wateja. Hizo zinabaki ni za serikali tu.
 
Watu wanzungumzia Internet of Things (IoT) leo sisi tuko tunapiga vita Kiingereza. IoT kwa kiswahili inaitwaje?
 
English sio mchongo maana hata SAUZI AFIRIKA wanajadili na tayari washaamua kiswahili kifundishwe nchini Kwao kuanzia 2020,,,,,,kiingereza mwachie Malkia
 
Chonde chonde ,, kiswahili kwa kuunganisha watanzania ,kielimu hasa sayansi kiingereza ni mahali pake . Hata mkisema China , Ujerumani nk. Wanatumia lugha zao , ni mataifa yaliyoendelea hivyo itabidi ujifunze lugha zao kwani hata sayansi wanaandika kwa lugha zao . Hamuoni watoto wetu wanavyofeli kwa sababu ya lugha? Huenda waalimu nao ni shida !! Check : for your own benefit let me use swahili . Kumbe kimempiga chenga
 
Tunahitaji kujua lugha nyingi na za kimataifa kadiri inavyowezekana. Hapa tunazungumzia English kwa sababu ndiyo lugha iliyoachwa na mtawala wa mwisho wa kikoloni wa nchi yetu, Uingereza. Mtawala wa mwisho angelikuwa mjerumani tungekuwa tunazungumzia kijerumani. Lugha ya kigeni katika mazingira yote ni rahisi kuijua ikifundishwa mashuleni kutoka chini kabisa. Hakuna anayesema Kiswahili hakiitajiki. Kiswahili nacho kifundishwe watu wakielewa kwa ufasaha siyo wale wa siku hizi wanaiga kiswahili cha Kenya ambapo WANAUME wanawaita WABABA na WANAWAKE wanawaita WAMAMA. Ni aibu tupu.. Labda kama msamihati wa Kiswahili sasa umekuwa. Kiswahili ni rahisi kuendelea nacho kwa sababu tunaishi nacho mitaani na kinafundishwa mashuleni. English itumike kama lugha ya kufundishia mashuleni kutoka Chekechea mpaka Vyuo vya elimu ya juu ndiyo tutaielewa vizuri na watoto na wajukuu wa nchi yetu wataielewa vizuri.
 
Watu wanashindwa kutofautisha kati ya faida na ulazima dio maana mnashindwa kuelewana,tulitakiwa tuambiane faida za lugha na si kulazimisha kujua lugha fulani.
 
Back
Top Bottom