Hivi kwanini lugha ya kingereza haitiliwi mkazo nchini mwetu?

Mimi sisemi tusome kata, nasema tusome kwa kiswahili. Ninachokuambia mimi ingekua rahisi polisi kufanya kazi yao kama lugha ingekua rafiki. Hata hivyo encryption sio suala la kujua computer na hacking tu, FBI walishindwa kufungua simu iliyofungwa na iCloud na mtu tu, mpaka wakaenda Apple kuomba msaada. Bill Gates na Zuckerberg walikua wanajifunza kichina kuwasiliana na wachina. Tutafsiri mambo yote kwa kiswahili halafu tuone kama hatujajenga mitreni na migari ya haha wenyewe.
Nawewe hujiulizi hao watoto wa viongozi wametufanyia nini?
Ulitaka wakufanyie nini?? Wakupande mgongoni?

Watu wanachakarika huku na kule kupata ajira na kuji-expose ulimwenguni.

Tukuulize wewe uliyevimbiwa viporo, "UMETUSAIDIA NINI NA KISWAHILI CHAKO" .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi sisemi tusome kata, nasema tusome kwa kiswahili. Ninachokuambia mimi ingekua rahisi polisi kufanya kazi yao kama lugha ingekua rafiki. Hata hivyo encryption sio suala la kujua computer na hacking tu, FBI walishindwa kufungua simu iliyofungwa na iCloud na mtu tu, mpaka wakaenda Apple kuomba msaada. Bill Gates na Zuckerberg walikua wanajifunza kichina kuwasiliana na wachina. Tutafsiri mambo yote kwa kiswahili halafu tuone kama hatujajenga mitreni na migari ya haha wenyewe.
Nawewe hujiulizi hao watoto wa viongozi wametufanyia nini?
Watoto wa viongozi nao karibu wote wanaingia kwenye mfumo wa ccm ili waendelee kula na baba zao kwa kuwaibia watz kwa kisingizio cha uzalendo, hivyo kukusaidia mtanzania wa chini mara nyingi ni ndoto especially katika hii awamu ya kujipendekeza ili wapewe vyeo.
Mimi nachoongelea hapa, ni intense exposure inayoletwa na kingereza, wape watu opportunity ya kuijifunza then waache wachague wakifika huko mbele, ila usiwakandamize kwa kuwadumaza fikra kwa kutowapa fursa ya kujua lugha ya kimataifa.
Hata mandela alijifunza afrikaans ili aweze kujifunza culture ya wakaburu na baadaye akafanikiwa kuwa kiongozi wao.
Wewe huwezi kuwa maskini alafu ukajifanya jeuri huku wenzako wanaokuzunguka wanasonga tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
INASIKITISHA SANA, SANA, SANA namna ambayo wananchi na viongozi wengi wa nchi hii wanavyochukulia Kiingereza.!!!! Nadhani HAKUNA kiongozi yeyote mwenye cheo kikubwa nchi hii ambaye hapeleki watoto wake kwenye shule za English Medium au kuwapeleka shule nje ya nchi kusoma. Huu ni ukweli ambao Watanzania wengi sana wanaufahamu, kwa hivyo napowasikia wananchi wakisema kwamba hakuna haja ya kujifunza Kiingereza bali Kiswahili ndio uzalendo NASHANGAA SANA !!

Tunataka nchi yetu iwe ni nchi ya viwanda. Maelezo yote ya namna ya kutumia mashine za viwandani yako kwa lugha ya Kiingereza. Tukitaka kupata masoko ya bidhaa zetu lugha ya mawasiliano ni Kiingereza. Mtu akitaka kuongeza ujuzi wake kwenye jambo lolote lugha inayotumika kwenye mtandao wa internet ni Kiingereza. Fundi wa mashine (kwenye nchi ya viwanda) akitaka kuagiza spea lugha inayotumika ni Kiingereza. Sasa kwa nini sisi Watanzania 'tunakimbia na kuogopa" Kiingereza kiasi hiki?

Tunasema Kiswahili ni lugha yetu. Ni kweli. Lakini lugha yetu YA ASILI SIO KISWAHILI japo ni karibu kila Mtanzania anazungumzwa Kiswahili. Kiswahili ingekuwa ni LUGHA YA ASILI ya KILA Mtanzania, tusingekuwa na lafudhi (accents) mbalimbali zinazomtambulisha mtu anayekiongea. Mchaga akizungumza Kiswahili utajua tu huyu ni Mchaga kwa ile lafudhi yake. Mhaya naye, na Msukuma, Mkurya, Mmasai, Msambaa na watu wa makabila mbalimbali wakisema utajua hii ni lafudhi ya kabila fulani. Maana ya kuwa na lafudhi hii ni kwamba LUGHA YA ASILI ya mtu huyo aliyekulia kijijini ni lugha ya kabila lake na SIO Kiswahili. Kwa hivyo kwa wengi wetu, KISWAHILI NI LUGHA NGENI KAMA KILIVYO KIINGEREZA. Labda ni wale tu waliozaliwa na kukulia mijini ndio hawana lafudhi ya kilugha.

Kwa sababu nilizotaja hapa juu, nakuombeni sana Watanzania wenzangu tujisukume kujifunza Kiingereza tukijua kwamba kitatusaidia sana katika maisha yetu ya baadaye.

.
 
Mwaka ujao tarehe 18 August 2019,Jopo la members wa SADC watakuja kufanya mkutano TZ na Rais ndio atakuwa Mgeni Rasmi nina uhakika siku hiyo lazima hatakuwepo nchini atakahimiwa na Mama SAMIA SULUHU,Chezea NGELI YA GENGE AKA KINGE? KILIKUJA NA MELI.
 
Natumai wakristo wanasherekea dominika nyingine katika calender ya shajara huku waislamu nao wakipumzika kusubiria wiki ianze tupambane kutafuta ugali wa familia.
Kuna jambo linasikitisha sana nchi mwetu, na viongozi wetu kwa kujua watanzania wana mawazo duni wanazidi kuwaangamiza kielimu na kiexposure.
Lugha ya kwanza ya kimataifa nchini mwetu haitiliwi mkazo kabisa na awamu hii ndio inaamua kuwapumbaza watu kwa kukazania kiswahili as if tuna mambo ya msingi tunayoyafanya kama nchi.
Shule za awali na msingi, lugha ya kufundishia ni kiswahili lakini unaposogea sekondari hadi vyuo ni 'ngeli', hii inashangaza sana.
Watoto wa viongozi wote wanasoma shule za ukweli na wengi wako nje ya nchi ambapo wanapata exposure ya kutosha, ila huku ndio wanapumbaza watu tu wakomae na kiswahili.
Inafika mahali, hata kuwa na uwezo katika nyanja za kimataifa watz wengi hawawezo kucompete, alafu mijitu bado inashangalia tu 'uzalendo uzalendo'.
Kujua lugha ngeni kunakuexpose na mambo mengi, especially kujua wenzako wanafanya nini, na kunakusaidia kupevuka mawazo na kuwa more creative.
Ila cha kushangaza zaidi, wakitangaza kazi utasikia competency in written and verbal english is a must, sasa kazi wanaziandaa kwa nani?
Mfano mmoja wapo, ni uchaguzi wa ubunge wa afrika mashariki, watu waliokuwa hawajui kingereza vizuri hadi wabunge wanawacheka ila waliokuwa vizuri mfano wa mtoto wa maghembe aliyesoma nje na kufanya kazi huko kwa miaka mingi, alikuwa anateleza tu na kupigiwa makofi kibao kuwa anajua mengi na yuko vizuri.
Sasa kwa mantiki hii, haya mambo ya ccm kudumaza akili za watu na kushangiliwa kwa upuuzi ni kwa manufaa ya nani?

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu Kiingereza ni muhimu,Watanzania tusidanganywe.
 
Watoto wa viongozi nao karibu wote wanaingia kwenye mfumo wa ccm ili waendelee kula na baba zao kwa kuwaibia watz kwa kisingizio cha uzalendo, hivyo kukusaidia mtanzania wa chini mara nyingi ni ndoto especially katika hii awamu ya kujipendekeza ili wapewe vyeo.
Mimi nachoongelea hapa, ni intense exposure inayoletwa na kingereza, wape watu opportunity ya kuijifunza then waache wachague wakifika huko mbele, ila usiwakandamize kwa kuwadumaza fikra kwa kutowapa fursa ya kujua lugha ya kimataifa.
Hata mandela alijifunza afrikaans ili aweze kujifunza culture ya wakaburu na baadaye akafanikiwa kuwa kiongozi wao.
Wewe huwezi kuwa maskini alafu ukajifanya jeuri huku wenzako wanaokuzunguka wanasonga tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Unafikiri, kama nchi tukijifunza kwa kiingereza ndo tutakwamuka kiuchumi?
 
1.Hivi sisi tusiojua kingereza,tunatofautiana nini na wanaojua kingereza kama Zambia, Kenya, Malawi, Ghana Zimbabwe, je wamefanikiwa kwenda uchumi wa kati na kingereza chao au wote tunalialia njaa tu?
2.Katika dunia ya utandawazi hivi unawezaje kulialia eti serikali haitilii mkazo hali kuna kila kitu ktk mitandao, kama upo siliasi unahitaji miezi 3 tu kujua hicho kingereza.Serikali imekuwekea hiyo miundombinu kwa nini usiitumie, kikwete aliwahi waambia watu wa Tanga kuwa "kama mnasubiri fursa iwafuate mlangoni subirini lakini serikali imewajengea barabara kazi kwen kuitumia".
3.Utafiti umeonesha kuwa matumizi ya kingereza yamechangia kudamza ubunifu na ufaulu duni, rejea tafiti za haki elimu.
4.Tatizo la waafrika sio lugha bali ni udumavu wa akili na kushindwa matumizi sahihi ya akili tulionayo katika kuyatawala mazingira yetu.Ushahidi wa hilo ni kwamba nchi za Afrika zilipeleka watoto/vijana kusoma ulaya kwa lugha ya huko lakini mpaka leo nitajie Muafrika aliethubutu kuivusha nchi yake kwenda kuwa nchi ya teknolojia kutokana na maarifa aliyopata kutoka nchi hizo.Pakistani ilimtuma abdisalam kusoma uingereza alichawafanya waingereza hawatamsahau, mtu mmoja tu alileta mapinduzi ya 'nuclear technology in islamic world'.
5.Hakuna utafiti unaoonesha kuwa maendeleo duni na umaskini barani Afrika ni kwa sababu ya kutumia lugha za asili.
6.Wanaoshadadia kingereza bado wametawaliwa na utumwa wa fikra ambao wazungu walitumia miaka mingi kuujenga na itachukua miaka mingi kujitambua, hapa wapo phd mpaka wasiojua k.k.k.
7.Tunatakiwa tuanze kutilia mkazo lugha ya komputer kutoka ngazi za chini ambayo ndio lugha ngeni barani Afrika na inatolewa vyuoni tu.Hii ndio lugha inayotawala teknolojia na haijatiliwa mkazo sio kingereza.Naomba niishi tu hapa lakini yapi mengi ya kujiuliza.
Hivi,unapata hasara gani kwa kujua Kiingereza?Mbona zipo faida tele tu.Hivi Watanzania tumekuwaje,mbona mawazo yetu yako duni sana.Tunadanganywa kwamba Kiingereza sio muhimu kwa kupewa flimsy reasons na sisi kwa kuwa hatukijui tunakubali.Hivi nani katuloga?It's beneficial to know as many languages as possible,Kifaransa,
Kichina,

Kijapani,Kijerumani Kirusi nk.kama ingewezekana.Kwa nini tunakuwa na mediocre reasoning?Hivi aliyekuambia kwamba maisha yako yote you will only communicate with Tanzanians only ni nani?
 
wewe unaandika pumba tu, unashindwa kujibu maswali ya msingi kazi kudhihaki watu kama muhadzabe vile
Kuna pumba zaidi ya kutetea kutojua Kiingereza?

Wewe unachostahili ni dhihaka tu , huna akili hata moja.

Eti ooohh si tutatafsiri Kiingereza kiwe Kiswahili.

Utakitafsiri vipi Kiingereza kama haukijui Kiingereza?

Unapaswa kwanza Kukijua Kisha ukitafsiri.

Elewa hilo ewe Juhha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna pumba zaidi ya kutetea kutojua Kiingereza?

Wewe unachostahili ni dhihaka tu , huna akili hata moja.

Eti ooohh si tutatafsiri Kiingereza kiwe Kiswahili.

Utatakifsiri vipi Kiingereza kama haukijui Kiingereza?

Unapaswa kwanza Kukijua Kisha ukitafsiri.

Elewa hilo ewe Juhha.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mimi ni mwanaume, wewe ni jinsia ipi? Naweza kua naumiza akili kumbe upo na PMS.
 
Hivi,unapata hasara gani kwa kujua Kiingereza?Mbona zipo faida tele tu.Hivi Watanzania tumekuwaje,mbona mawazo yetu yako duni sana.Tunadanganywa kwamba Kiingereza sio muhimu kwa kupewa flimsy reasons na sisi kwa kuwa hatukijui tunakubali.Hivi nani katuloga?It's beneficial to know as many languages as possible,Kifaransa,
Kichina,

Kijapani,Kijerumani Kirusi nk.kama ingewezekana.Kwa nini tunakuwa na mediocre reasoning?Hivi aliyekuambia kwamba maisha yako yote you will only communicate with Tanzanians only ni nani?
Kuna faida za kujua kiingereza, ila kujifunza kwa kutumia kiingereza kwa mswahili sio sawa. Wasome tu kiingereza hata kihindi wakitaka, ila tujifunze mambo kwa kiswahili.
 
Kuna faida za kujua kiingereza, ila kujifunza kwa kutumia kiingereza kwa mswahili sio sawa. Wasome tu kiingereza hata kihindi wakitaka, ila tujifunze mambo kwa kiswahili.
Mkuu kwani tukijifunza kwa Kiingereza kuna ubaya gani?Hivi hatuoni kwamba it's the best way to know it.Practise makes perfect mkuu.Hivi kwa nini tumejikatia tamaa kwamba hatuwezi kujifunza Kiingereza?Mbona ni lugha tu you can learn it.
 
Kiingereza tusome tu, mi sina tatizo na hilo. Ila physics na utaalamu mwingine tujifunze kwa kiswahili. Mtu akitaka kichina akisome ila masomo yawe kwa kiswahili. Kuihusisha Artificial Classification na mazingira yetu ni kwa kiingereza ni kazi sana ila mtu akikufundisha dissection kwa kiswahili vigumu sana kutoelewa. Utajua hii ni ateri, utajua hii ni osofagasi, utajua puru kila kitu na kukilinginisha na unavoviona kila siku.
 
Dah,kazi kweli kweli.Haya mkuu.Ila ukweli utabaki kwamba unahitaji kujua Kingereza,written and spoken,tena fluently,whether you like it or not.
 
Back
Top Bottom