Hivi kwanini kwa sisi wanaume wengi, ni rahisi kumpata mdada usiemtaka, ila kumpata mdada unaemtaka inakuwa ni ngumu?

AlphaMale

JF-Expert Member
Oct 26, 2019
613
1,401
Nimeshaobserve sana hili suala yaani kwa mfano mimi nisipomtamani mdada rohoni, huyo mdada lazima anishobokee, kosa ni kuwa nikiona mdada halafu moyoni nikaanza kumtamani sana na kumpenda na kumuwaza kila siku, bhasi huwa simpati.

Hii haijalishi muonekano wake, mdada anaeza akawa mzuri tu, ila aagh nkamwangalia na kusema hata nkimtongoza atanipotezea muda, halafu anaeza asikae akilini mwangu, na hata nikilala nisimwazie wala kumtamani, ila baada ya muda huyo mdada mzuri ataanza shobo na mimi, just because rohoni sikumtamani.

Ila nikimtamani mdada kimawazo, hata kabla ya kutongoza, huyo mdada anakua hana interest kabisa na mimi, she won't give a damn about me, na anakua hajui kama na-exist

Why does this happen?
 
Aaah wapi kwa nyie wanaume ndo rahisi zaidi kumpata humpendae, kuliko sisi wanawake, manake sisi tunachaguliwa na nyie mnachagua....ukipojihamini ni uzembe wako tuu

Dada yangu, ulioyasema sio rahisi kama unavofikiria, mara nyingi kwa sisi wanaume ili tupate wanawake tunaowapenda, inabidi tukubali kupendewa hela, bcoz wanawake tunaowapenda wanakua hawatupendi, na hawana time na sisi..

Sisi wanaume tukipata wanawake tuliowapenda toka moyoni bila kutumia hela ni bahati sana.

Ndo maana wanaume wengi wanaishia kuoa wake wanaowaona wa kawaida au sura ngumu, wakijifariji mbele ya jamii kuwa hao wanawake ni wife material, kumbe walikataliwa na wanawake waliowataka ceicey
 
Hutokea pea mbili zinazotamaniana kupendana lkn pia hutokea pea mbili moja kutompenda mwenzake.. kupenda Ni Kama mtego tu,ikitokea mkanasana ndo imeenda hiyo!.. mkuu hapa unataka tupige hesabu za probability..😜
 
Nakumbuka Physics ya Form ngapi sjui topic ni MAGNETISM inasema kuwa "UNLIKE POLES ATTRACT LIKE POLES REPEL". PERIOD.
 
Ukishajua hilo utakuwa unaelewa tunaishi na wapenzi wa watu wengine hili ni kweli kabisa.

Wengi tunafosi tu ila watu tulionao kimsingi hatukupaswa kuwa nao. Hivyo ukihisi hupendwi vile unapenda uelewe kabisa huyo hakuwa wako.
 
Jibu ni rahisi tu, madamu demu kazi yake kukubali au kukataa basi siku zote itakuwa ngumu kwa Mwanaume. Ni easy kwa demu kupata Mwanaume anayemtaka akiamua kuliko kwa Mwanaume kupata demu, ...
 
Back
Top Bottom