Hivi kwanini ITV wamemwamini Sam Mahela kuendesha kipindi cha Dk45?

Kidamva

JF-Expert Member
Dec 3, 2013
2,580
1,981
Jana nimeangalia kipindi cha Dakika 45 ITV nimesikitishwa sana na Sam Mahela alipokuwa akimhoji Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro.

Of course alikuwa na maswali ya msingi mazuri, lakini anakosa follow up questions, matokeo yake anamwacha mhojiwa atiririke tu hata kama hayuko sahihi.

Kwa mfano alipomuuliza kuhusu kukamata wapinzani, Sirro alisema Polisi wataendelea kuwakamata kwa sababu ni wahalifu, akaongea pale kama dakika 5 hivi, Mahela amenyamaza tu.

Kwanini hakuchomeka maswali mawili matatu pale? Ina maana wahalifu ni wapinzani tu? Mbona wanakamatwa wakifanya mikutano ya Ndani wakati hata CCM wanafanya na hawakamatwi?

Hapo niliona udhaifu mkubwa wa Mahela, nikabaki kujiuliza; kwa nini ITV wanampa kipindi Kizito kama hiki wakati hana uwezo? Au ITV wanaangalia uzuri wa sura ya mwandishi tu?

ITV wanapata bahati ya kupata vipngozi wazito wa kuwahoji, lakini wanashindwa wanashindwa kuwabana kwa maswali ya msingi. Na hii yote ni kwasababu hawana upeo wa mada mahsusi au hawasomi kabla ya kuhoji mtu.

ITV badilikeni.
 
Mkuu kidamva umesema kweli kabisa..

Shida ya mtu kama Sam Mahela hivi sasa akili yake ipo kwenye uteuzi wa nafasi kama u DC na nyingine za namna hiyo..

Kuanzia Buhohela alivyopata post Ikulu na Godwin Gondwe alivyopata u DC wakitokea ITV, huyu Mahela amepoteza umakini kabisa..

Yani unakuwa mtu unaishi kama kwa kuvizia vizia au kuchungulia chungulia..

Nilimtizama jinsi IGP alivyokuwa akijibu yale maswali bila presha yoyote.

IGP anatakiwa ahojiwe na mtu kama Tido Mhando.
 
Kipindi cha DK 45 ni recorded segment, kwahiyo kinarushwa wakati washa hariri mambo mengi tu, kwa sababu hiyo sio rahisi kuacha maswali yenye ukakasi kama "mbona ccm hawakamatwi", ? Ina maana wapinzani ndo wanaotakiwa kukamatwa tu?
Ukitaka kuniridhisha huwa wanakuwa na tangazo lenye kutoa hadidu rejea za kipindi kitachofata kwa wiki nzima kabla ya kipindi husika kurushwa hewani, hiyo ni justification ya kuwa kipindi kina kuwa kimepitia kwanza "maabara ya uhariri" kabla ya kwenda hewani.
 
Mkuu kuna tatizo kwa baadhi ya waandishi walio wengi kwenye probing skills pia namna ya kutengeneza logical flow of arguments..in most cases wanadhani kumtwanga maswali mengi tu inajitosheleza..

Issue ya Mahela...huyu jamaa nachompendea ana element ya kupenda kazi na kupenda apande....ila SHULE aongeze simaanishi madegree tu....pia kuwa kuwa conversant na topic under discussion sio kuuuliza tu miswali isiyo na logical flow huku ukimuacha msemaji atiririke!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna waandishi wa habari wa maana ndio tatizo. huyo jamaa anatia kichefu chefu hata kuangalia kipindi chake... mi huwa nazima nahama nikiona anavyobinuka binuka kwenye kiti akitupa mikono kusisitiza..
 
...Kwanini hakuchomeka maswali mawili matatu pale? Ina maana wahalifu ni wapinzani tu? Mbona wanakamatwa wakifanya mikutano ya Ndani wakati hata CCM wanafanya na hawakamatwi?.

Wanaoitwa kuhojiwa wengi kwa kukiogopa kivuli cha JPM, huomba maswali at-least masaa 72 kabla ili wayaangalie, wayahariri, waondoe wasioyayapenda au yale yanayokwenda kuwachonganisna na Rais na mwisho wa siku wanataka assurance kwamba wataulizwa hayo tu ''waliyokubaliana''. Hakuna interview huru pale.
 
Wanaoitwa kuhojiwa wengi kwa kukiogopa kivuli cha JPM, huomba maswali at-least masaa 72 kabla ili wayaangalie, wayahariri, waondoe wasioyayapenda au yale yanayokwenda kuwachonganisna na Rais na mwisho wa siku wanataka assurance kwamba wataulizwa hayo tu ''waliyokubaliana''. Hakuna interview huru pale.
Kati ya watu woooteee...umeongea point sn...wengi wanajadili pasipo kujua inside-out ya nature ya hiki kipindi....wanadhani ni mubashara kweli km wanavyosema

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom