Bonheur Travels Tanzania
JF-Expert Member
- Dec 29, 2020
- 252
- 499
Salaam,
Tunaendelea kutatua changamoto na kutoa elimu kwa umma katika nyanja mbalimbali.
Uzi huu tutautumia kujua sababu za watu kutosoma vitabu hasa hapa nchini Tanzania. Lazima kuna shida mahali!
Wataalamu wameshaeleza na kuthibitisha kuwa usomaji wa vitabu husaidia kunoa ubongo, kubadilisha tabia za mtu/jamii, kumsaidia kudhibiti mazingira, biashara na faida nyingine lukuki ikiwemo burudani na kusafiri kimawazo, kihisia na kujifunza.
Pia mtu anayesoma na asiyesoma vitabu utofauti wao mkubwa upo kwenye namna ya kufikiri na kutatua changamoto.
Labda tukuulize wewe ambaye huna utaratibu wa kujisomea vitabu; Kwanini hununui kitabu na kusoma? Je, hupendi au basi tu? Nini kifanyike upate ari ya kusoma vitabu?
Funguka, tuzungumze.