Hivi kwanini dawa za kulevya zinapokamatwa haziteketezwi hadharani kama bangi?

mitale na midimu

JF-Expert Member
Aug 26, 2015
10,420
17,722
Unga /Madawa ya kulevya Mara ukisikia yamekamatwa huwa hatuoni mchakato wa uteketezwaji wake kama tunavyoona vitu vingine haramu kama bangi, silaha haramu zikikamatwa vijijini.

Nini chanzo au ni technology ya uteketezwaji wake inahitaji usiri?

Msaada kutoka kwa wajuvi wa mambo.
 
Hayo yana kazi hospital.

Yakibaki yanabadilishiwa matumizi, yanatoa maandazi flani safi sana, watu wanakula.
 
Hili ndilo swali nlilataka kumuuliza Makond na siro!!
Labda kamishna mteule atakuja kujibu hapa...
 
Kuna sababu mbalimbali za kutoteketeza ikiwemo yafuatayo:
  1. Kwanza inabaki kama kielelezo cha ushahidi mahakamani, itakaaa mpaka mwenendo wa kesi itakapokwisha
  2. Kuna madhara ya kiafya yanayotokana na kuteketeza hayo madawa, uteketezaji wake unahitaji mitambo ya kisasa kuzuia adhari kwa binadamu na mazingira na wanyama
  3. Hubakizwa kwa uzembe wa namna moja au nyingine ili wengine wajinufaishe au waponee humo humo kama mvyosikia kwenye vyombo vya habarri hata wale jamaaa nao wapo wenye chain
 
Mkuu heshima yako, ashakum si matusi.
Ila haifai kuuliza maswali ya kitoto.
Jibu unalo.
 
Kwa kifupi huwa unateketezwa. Baada ya kesi huwa wanapeleka kwenye vinu vya kutengenezea klinker pale Wazo , Mbeya , Tanga na kuchomwa chini ya usimamizi mkubwa wa police. Ugumu uliopo ni kujua kama kinachochomwa kweli ndo kilicholengwa.
 
serikali inapenda watoto ila haipendi utoto....
gram moja kama ni 50,000 kwenye kilo moja zipo ngapi, (50,000x1000=50mil) hii ni ela nyingi sana, inafaa kufanyia cancelin waathirika wote na ikabaki. sasa kama tumekamata tano 3 za unga. unadhani iyopesa niya karanga iyo ni bajeti ya taifa hatuezi kwa kweli hatuwezi kuteketeza unga na watanzania wananjaa tutasaga maindi yetu kisha tuwape unga,. kama ni kusafirisha njee yasiende maindi uende unga.,
 
lakini vipodozi, dunia nzima tutajua, unga katika maisha yangu niliwahi sikia unachomwa mara 1 tu na kule tanga, na hata hivyo wanaokamatwa hawaonyeshwi kwenye tv au magazeti huwa wanafichwa, utasikia tu jeshi limekamata lakini hatuwaoni
 
Kama tumegoma kuchoma pembe za ndovu ndio unataka tu chome unga

Usilete mchezo kwenye pesa
 
Kwa kifupi huwa unateketezwa. Baada ya kesi huwa wanapeleka kwenye vinu vya kutengenezea klinker pale Wazo , Mbeya , Tanga na kuchomwa chini ya usimamizi mkubwa wa police. Ugumu uliopo ni kujua kama kinachochomwa kweli ndo kilicholengwa.
Kidoogo bado kweli au sikweli, bt naweza sema huenda kweli
 
Kwa kifupi huwa unateketezwa. Baada ya kesi huwa wanapeleka kwenye vinu vya kutengenezea klinker pale Wazo , Mbeya , Tanga na kuchomwa chini ya usimamizi mkubwa wa police. Ugumu uliopo ni kujua kama kinachochomwa kweli ndo kilicholengwa.
Huenda ikawa ingawa sijui zaid
 
Unga /Madawa ya kulevya Mara ukisikia yamekamatwa huwa hatuoni mchakato wa uteketezwaji wake kama tunavyoona vitu vingine haramu kama bangi, silaha haramu zikikamatwa vijijini.

Nini chanzo au ni technology ya uteketezwaji wake inahitaji usiri?

Msaada kutoka kwa wajuvi wa mambo.
Huwa tukidhikamata tunadhihifadhi halafu tunadhiuzaga mdogomdogo zingine tunatumia wenyewe ili kuhakikisha kama kweli ni original au fweki.!
 
Back
Top Bottom