Azizi Mussa
JF-Expert Member
- May 9, 2012
- 9,172
- 7,428
Disclaimer;
=========
Kwanza; moja ya mambo magumu sana kwa sasa kwenye nchi yetu ni kuwa mkweli na,
Pili; mada hii hailengi kutetea uonevu wowote unaofanywa na yeyote kwa mtu yoyote kwa sababu yoyote ile.
==========
Duniani kuna matatizo mengi tu na hilo hakuna anayekataa; yalikuwepo, yapo na yataendelea kuwepo mpaka mwisho wa maisha yetu. Mtu anayekuambia matatizo yaliyopo au yanayomkabili kila siku badala ya kuja na ubunifu wa kukabiliana nayo anachosha sana. Sio kwa sababu matatizo anayosema yanamkabili ni ya uongo, bali kwa sababu matatizo hayatatuliwi kwa kurudia rudia kuyasema vile vile, kwa namna ile ile na kwa watu wale wale na kwa mazingira yale yale bali kwa ubunifu na kuchukua hatua sahihi.
Kwa mfano, kila siku ukimsikiliza mtu analalamika alivyo masikini na asivyo na hela; halafu unamshauri afanyeje atoke hapo lakini hafanyi, kesho tena analamika hivyo hivyo, inafikia hatua anachosha, si kwa sababu anasema uongo, bali anazungumzia zaidi matatizo badala ya kuja na solutions ‘in a serious note’ na anapopewa solutions anajifanya hajaziona.
Kama ilivyo kwa baadhi ya vyama, mmekuwa mkishauriwa mara nyingi namna ya kufanya ili mfanikiwe na kupunguza changamoto na matatizo yanayowakabili, lakini hamjawahi tu hata ku ‘appreciate ‘ushauri mnaopewa achilia mbali kuutekeleza. Matokeo yake, mnafanya mambo yale yale, mnapata matatizo yale yale, mnatoa malalamiko yaye yale, kwenye mazingira yale yale na kwa hadhira ile ile na mnataka kuaminiwa.
Kwa mfano, mmekuwa mkiitisha mikutano na waandishi wa habari, kabla hamjafanya inasambaratishwa, kisha mnakamatwa, kisha mnalalamika kuonewa inapita. Baada ya muda mnafanya hivyo hivyo, inajirudia tena na tena. Utadhani hamjawahi kushauriwa ni nini cha kufanya ili kuepukana na mzunguko huo, au mnayoshauriwa hyafai na mlishawahi kuwa na hoja za msingi kwa nini hayafai.
Mtu tu anaweza kujiuliza, si mlisema mnaanzisha mikutano ya hadhara nchi nzima kuhamashisha mabadiliko ya tume ya uchaguzi, wakushauri wakashauri na kushauri, kwamba kama hilo lina u serious, njia bora za kutumia kulingana na mazingira ni zipi, lakini hola! Mmefikia wapi sasa? Mtasema tatizo korona, lakini mbona hamkufanikisha kabla la korona, mtasema mikutano ilipigwa marufuku, je, mlipotangaza mikutano nchi nzima ilikuwa imeruhusiwa? Maswali ni mengi sana na najua hayatajibiwa zaidi ya watu kuleta kejeli hapa lakini yote ni heri tu.
Swali ambalo linafikirisha sana, ni kwa nini hamsikilizi ushauri hata uwe mzuri kiasi gani licha ya kwamba unalenga kuwasaidia ninyi wenyewe kuepuka matatizo yanayoepukika? kinyume chake mnafanya vile vile na mnaishia kukwama na kulalamika kila siku katika namna ile ile na mazingira yale yale?
Kwa mfano, sasa hivi kupitia intanet, unaweza kuwasiliana na mamilioni ya watu ukiwa kokote duniani na kufanya mijadala ‘instantly” bila gharama na usumbufu wowote.Mnapodhani kuwa mna ujumbe ambao mnafikiri ni muhimu, kwa nini msiufikishe kwa jamii kwa njia hii? kinyume chake mnaitisha mkutano na vyombo vya habari licha ya kuwa mnajua mtaishia kusambaratishwa na kukamatwa na mna uzoefu wa kutosha kwenye hilo? Ni swali rahisi hivyo tu yani.
Na kama mnashindwa kuelewa na kufanyia kazi kitu rahisi namna hii licha ya madhila yanayowafika, kwa nini muaminike kwenye mambo makubwa na complicated labda?
Na kama sasa hivi hamna dola wala nguvu kubwa lakini hamshauriki hata kwenye vitu simple kama hivi, ni nani atakayedhubutu kuinua mdomo au kalamu yake kuwashaurini siku mkiwa na mamlaka ? licha ya wasiwasi kwamba hamtasikiliza ushauri wa mtu, mtu anaweza kujiuliza juu ya usalama wa huyo atakayejaribu kushauri katika mazingira hayo.
Mwisho wa siku kila mtu na kichwa chake kwani ni vigumu kumlazimishia mtu kuelewa kitu kama yeye anaiona dunia kutoka kwenye 'angle' tofauti na wewe. Lakinini muhimu kubadilika.Najua kuna watakaojibu ‘kawashauri CCM kama wanashaurika’,ni sawa tu vile vile.