Hivi kwanini CHADEMA hamshauriki? Hivi siku mkiwa na dola na maguvu atawashauri nani mumsikilize?

Azizi Mussa

Verified Member
May 9, 2012
8,596
2,000
Disclaimer;
=========

Kwanza; moja ya mambo magumu sana kwa sasa kwenye nchi yetu ni kuwa mkweli na,
Pili; mada hii hailengi kutetea uonevu wowote unaofanywa na yeyote kwa mtu yoyote kwa sababu yoyote ile.
==========
Duniani kuna matatizo mengi tu na hilo hakuna anayekataa; yalikuwepo, yapo na yataendelea kuwepo mpaka mwisho wa maisha yetu. Mtu anayekuambia matatizo yaliyopo au yanayomkabili kila siku badala ya kuja na ubunifu wa kukabiliana nayo anachosha sana. Sio kwa sababu matatizo anayosema yanamkabili ni ya uongo, bali kwa sababu matatizo hayatatuliwi kwa kurudia rudia kuyasema vile vile, kwa namna ile ile na kwa watu wale wale na kwa mazingira yale yale bali kwa ubunifu na kuchukua hatua sahihi.

Kwa mfano, kila siku ukimsikiliza mtu analalamika alivyo masikini na asivyo na hela; halafu unamshauri afanyeje atoke hapo lakini hafanyi, kesho tena analamika hivyo hivyo, inafikia hatua anachosha, si kwa sababu anasema uongo, bali anazungumzia zaidi matatizo badala ya kuja na solutions ‘in a serious note’ na anapopewa solutions anajifanya hajaziona.

Kama ilivyo kwa baadhi ya vyama, mmekuwa mkishauriwa mara nyingi namna ya kufanya ili mfanikiwe na kupunguza changamoto na matatizo yanayowakabili, lakini hamjawahi tu hata ku ‘appreciate ‘ushauri mnaopewa achilia mbali kuutekeleza. Matokeo yake, mnafanya mambo yale yale, mnapata matatizo yale yale, mnatoa malalamiko yaye yale, kwenye mazingira yale yale na kwa hadhira ile ile na mnataka kuaminiwa.

Kwa mfano, mmekuwa mkiitisha mikutano na waandishi wa habari, kabla hamjafanya inasambaratishwa, kisha mnakamatwa, kisha mnalalamika kuonewa inapita. Baada ya muda mnafanya hivyo hivyo, inajirudia tena na tena. Utadhani hamjawahi kushauriwa ni nini cha kufanya ili kuepukana na mzunguko huo, au mnayoshauriwa hyafai na mlishawahi kuwa na hoja za msingi kwa nini hayafai.

Mtu tu anaweza kujiuliza, si mlisema mnaanzisha mikutano ya hadhara nchi nzima kuhamashisha mabadiliko ya tume ya uchaguzi, wakushauri wakashauri na kushauri, kwamba kama hilo lina u serious, njia bora za kutumia kulingana na mazingira ni zipi, lakini hola! Mmefikia wapi sasa? Mtasema tatizo korona, lakini mbona hamkufanikisha kabla la korona, mtasema mikutano ilipigwa marufuku, je, mlipotangaza mikutano nchi nzima ilikuwa imeruhusiwa? Maswali ni mengi sana na najua hayatajibiwa zaidi ya watu kuleta kejeli hapa lakini yote ni heri tu.

Swali ambalo linafikirisha sana, ni kwa nini hamsikilizi ushauri hata uwe mzuri kiasi gani licha ya kwamba unalenga kuwasaidia ninyi wenyewe kuepuka matatizo yanayoepukika? kinyume chake mnafanya vile vile na mnaishia kukwama na kulalamika kila siku katika namna ile ile na mazingira yale yale?

Kwa mfano, sasa hivi kupitia intanet, unaweza kuwasiliana na mamilioni ya watu ukiwa kokote duniani na kufanya mijadala ‘instantly” bila gharama na usumbufu wowote.Mnapodhani kuwa mna ujumbe ambao mnafikiri ni muhimu, kwa nini msiufikishe kwa jamii kwa njia hii? kinyume chake mnaitisha mkutano na vyombo vya habari licha ya kuwa mnajua mtaishia kusambaratishwa na kukamatwa na mna uzoefu wa kutosha kwenye hilo? Ni swali rahisi hivyo tu yani.

Na kama mnashindwa kuelewa na kufanyia kazi kitu rahisi namna hii licha ya madhila yanayowafika, kwa nini muaminike kwenye mambo makubwa na complicated labda?

Na kama sasa hivi hamna dola wala nguvu kubwa lakini hamshauriki hata kwenye vitu simple kama hivi, ni nani atakayedhubutu kuinua mdomo au kalamu yake kuwashaurini siku mkiwa na mamlaka ? licha ya wasiwasi kwamba hamtasikiliza ushauri wa mtu, mtu anaweza kujiuliza juu ya usalama wa huyo atakayejaribu kushauri katika mazingira hayo.

Mwisho wa siku kila mtu na kichwa chake kwani ni vigumu kumlazimishia mtu kuelewa kitu kama yeye anaiona dunia kutoka kwenye 'angle' tofauti na wewe. Lakinini muhimu kubadilika.Najua kuna watakaojibu ‘kawashauri CCM kama wanashaurika’,ni sawa tu vile vile.
 
Bia yetu

JF-Expert Member
Apr 14, 2020
4,986
2,000
Mkuu Chadema wameshajikatia tamaa wanajua October hawatakua na Mbunge hata mmoja

Wanachofanya sasa ni kuombea tusifanye Uchaguzi ili waendelee kula ruzuku
 
Azizi Mussa

Verified Member
May 9, 2012
8,596
2,000
Verified user huwezi kuwa na hoja binafsi. Ukiwa nayo wafa!
Moja ya tatizo kubwa tulilonalo ni kujadili mtu badala ya kujadili masuala. Unakuta mtu anakuja na hoja ya msingi, badala ya watu kupima hoja, ubora wake, udhaifu wake, faida na hasara zake, wanapambana kuonesha jinsi mleta mada asivyofaa.

Wewe unaamini kumjadili mleta mada itasaidia kutatua matatizo ya msingi yanayokabili siasa zetu ikiwemo tatizo linalozungumzwa kwenye mada ya msingi?
 
Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
23,999

Ukileta hoja kwa mfano: Wapinzani hawaonewi.au say Nyerere hajafa yuko Butiama...... then tutakujadili wewe.

Ukileta hojakuwa Stigilazi goji utanufaisha taifa.. tutajadili hoja hiyo maana inajadilika kwa watu wenye akili zao...
nadhani umenielewa
 
denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
1,475
2,000
Hapa mleta mada naona unawalaumu Chadema kwa ustaarabu wao, nothing else.

Ieleweke wazi, baada ya lile tamko la kupiga marufuku mikutano ya siasa Chadema walilalamika wakidai sheria za nchi zimevunjwa.

Sasa baada ya hapo ilitegemewa wenye mamlaka wajirudi waone udhaifu wao warekebishe mambo, lakini badala yake wakaendelea kuwa viburi, na Chadema kwa upande wao wakaendelea kuwa wavumilivu mpaka walipotaka pawepo maridhiano, lakini bado watawala wakawa viburi.

Baada ya Chadema kuona malalamiko yao hayasikilizwi, ndio sasa wakaamua wao kuanza mikutano ya hadhara lakini baada ya M/kiti wao kutangaza, siku hiyohiyo ndio tukaambiwa Corona imewasili nchini.

Sasa kwenye mazingira haya ulitaka Chadema waendelee na mikutano yao nchi nzima huku wakiweka rehani afya za wapenzi na wanachama wao ambao wangehudhuria hiyo mikutano, hasa ukizingatia Corona inaambukizwa kwa njia ya hewa?!

Kimsingi sijaona mantiki yako kwenye kuilaumu Chadema kuhusu mambo wanayoanzisha kutotekelezeka, kama vile hakuna sababu za msingi zinazowafanya washindwe kutekeleza mambo hayo, sababu zipo.

Kwa mfano hili la leo utawalaumu Chadema kwa lipi, wao wameitisha mkutano, baada ya kufuata taratibu zote wanaambiwa na polisi mkutano hautafanyika, tena polisi wanaenda kumzuia Mbowe nyumbani kwake!

Hapo unataka Chadema washindane na polisi wakati wao hawana polisi?!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Azizi Mussa

Verified Member
May 9, 2012
8,596
2,000
Ukileta hoja kwa mfano: Wapinzani hawaonewi.au say Nyerere hajafa yuko Butiama...... t
Hii maada haihusiani na wapinzani kuonewa au kutokuonewa au Nyerere kafa.

Nasema; kama unalima nyanya, unajua kipindi cha mvua nyanya zinaharibiwa na ukungu, na ili uweze kuvuna, unatakiwa kutumia dawa flani au kulima kwenye green house,na umeshashauriwa kufanya hivyo mara nyingi unapuuza, unaendelea kulima kawaida tu, halafu nynya zikishambuliwa na ukungu unalamika kama vile hukujua, au hukushauriwa, hilo hi tatizo.

Hapo tunachojadili sio tena kwamba ukungu unaathiri nyanya au laa.

Kama kwa mfano huu bado utakuwa hujanielewa,basi labda utaeleweshwa na wajumbe wengine.
 
Bome-e

JF-Expert Member
Jan 3, 2014
12,806
2,000
Nimeona mlolongo wa hoja ulizotaja!Nimeona tatizo kubwa sana kwa wewe mleta mada!Yote uliyotaja kama hoja wasizotaka kushaurika ni kwamba ni haki zao za kikatiba!Yaani mtu anakushauri usitumie haki zako ulizopewa kikatiba!Naona tatizo kubwa liko upande wa pili!

Ni kama wewe mtu akupangie mke wa kuoa wakati una haki ya kuchagua,huko ni kumnyima mtu uhuru wake wa maisha!Udikteta wa JPM lawama upeleke CDM,ni sawa kweli?
 
Donasian kabengo

JF-Expert Member
Jul 29, 2016
582
250
Hii maada haihusiani na wapinzani kuonewa au kutokuonewa au Nyerere kafa.

Nasema; kama unalima nyanya, unajua kipindi cha mvua nyanya zinaharibiwa na ukungu, na ili uweze kuvuna, unatakiwa kutumia dawa flani au kulima kwenye green house,na umeshashauriwa kufanya hivyo mara nyingi unapuuza, unaendelea kulima kawaida tu, halafu nynya zikishambuliwa na ukungu unalamika kama vile hukujua, au hukushauriwa, hilo hi tatizo.

Hapo tunachojadili sio tena kwamba ukungu unaathiri nyanya au laa.

Kama kwa mfano huu bado utakuwa hujanielewa,basi labda utaeleweshwa na wajumbe wengine.
Kaa kimya funga baku.....

Huo sio mfano halisia!Mfano halisia ingekuwa kuna mtu tu kutokana na uwezo wake amekuamulia usilime Mahindi badala yake ulime maharage!Sasa kila ukilima Mahindi yeye anakuja na vijana wake wanayang'oe na kuharibu shamba!Je,utaacha kulima Mahindi na badala yake ulime maharage wakati ni haki yako kulima mazao hayo?

Ni kwamba CDM wanalaumiwa kwa kutumia haki zao walizopewa na katiba!Yaani ili ysilaumiwe basi waachane na kufanya hayo ambayo katiba imewaruhusu na badala yake wafanye kile ambacho dola inawataka wafanye!
Naona mleta mada unaelekeza lawama sehemu isiyostahili kupata lawama!
Ipo siku huenda upinzani ukapata haki yao ya kufanya siasa kwa uhuru,hawa ambao wanapitia tanuru kwasasa watakumbukwa kuwa waliendeleza harakati za kupigania uhuru na haki ya kufanya siasa!
 
Tall Guy fam

JF-Expert Member
Jan 16, 2017
643
1,000

Unachokiongea ni sahihi kabisa mkuu, lakini sasa wapinzani wafanyaje ili kukabiliana na changamoto zao? Ndio mleta mada amekuja na majibu na lawama kwamba hawafuati ushauri hebu soma vizuri mkuu.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom