yani...dohKuna ule wimbo wa Dogo Janja..Ngarenaro kuna sehemu anaimba..
"Unanipaga mpaka mambo ya uwani".. Sasa najiuliza mambo ya uwani ndio yapi hayo kama sio kuchezea tope..
Kweli kabisa mkuu, mimi huwa najiuliza hivi hizi bongo fleva zinafaa kweli kufundishia "fasihi" kama zilivyokuwa nyimbo za kina "Marijani"? Miaka 30 inayokuja vijana wetu watajifunza nini kutokana na hizi bongo fleva?
Hapo ni kila zama na wakati wake,mambo yanabadilika na ngumu kuzuia
Sawa kabisa unamwambia ni "makalio", ok, sasa anamsikiliza Diamond kwenye wimbo wa Salome akisema; "mie bebi, kwenye msambwanda, huwa siendagi ngenge ni ngangaaa".... Hapo unafikiri watoto wanapata picha gani?Makalio!! unamwambia huo ni msamiati mpya
Mimi napenda sana muziki wa "country". Lakini hiyo haina maana kuwa sisikilizi aina nyingine ya muziki. Hata "bongo fleva" pia nasikiliza sana lakini siyo zote zilizojaa mashairi machafu. Isitoshe wakati mwingine siyo rahisi kukwepa kuzisikiliza hizi nyimbo zenye mashairi machafu hasa zinapopigwa kwenye vyombo vya usafiri kama daladala n.k.Kwa heshima na taadhima naomba uwasaidie kutunga Chief
Lakini naomba unijibu haka kaswali ulaya huwa unasikiliza ama kutizama nyimbo za nani lakini pia naomba nikuulize nyumbani kwako una CD ama flash za nyimbo za aina gani ya muziki?
Mimi napenda sana muziki wa "country". Lakini hiyo haina maana kuwa sisikilizi aina nyingine ya muziki. Hata "bongo fleva" pia nasikiliza sana lakini siyo zote zilizojaa mashairi machafu. Isitoshe wakati mwingine siyo rahisi kukwepa kuzisikiliza hizi nyimbo zenye mashairi machafu hasa zinapopigwa kwenye vyombo vya usafiri kama daladala n.k.
Nikiwa nyumbani kwangu naweza kuamua aina ya muziki ninaotaka kusikiliza, lakini unapokuwa kwenye public place siyo rahisi kuchagua nini unataka kusikiliza.
Nakubaliana na wewe kabisa, sisi hatuwezi kubadilisha mawazo ya hawa "Wasanii" lakini Serikali inaweza kuzisimamia sheria zake hasa kwa kuitumia BASATA, kwani sasa imekuwa kama vile BASATA wao wanaangalia tu video na kuzikosoa bila ya kuangalia "mashairi" pia. Matusi yanaimbwa wazi wazi hata kama wanatumia misemo fulani fulani, lakini misemo hiyo inajulikana wazi kuwa ni matusi.Basi sawa kaka nimekwelewa na umetoa mchango kama mdau wa muziki na si mihemko kama wafanyavyo wengine lakini safari yamabadiliko ni sisi wenyewe na wao wanatupa tutakacho,tizama hao sijui wasafi wanatembea na kiki kila siku za aibu na ujinga wa kila aina huku wakipata wajinga wengi wanaopenda ujinga ndo maana unaona mavoko anashindwa kwenda na kasi yao coz si mtu wa sikendo ama matusi ya wazi
Lakini wao wanatupa zaidi kile wanachoamini ndicho tupendacho ni kama tu Joti kuvaa sketi na mambo ya kishoga huku tukimsapoti kwa kusema anafanya komedi,ile sio komedi mzee na ingekuwa hivyo basi majuto ama Mr Bean wangelipishana kununua madela
Lililojema ni kujikalia kimya maana hatuwezi kuflash vichwa vya wapumbavu bora wale wajinga ila si hawa wapumbavu ambao zito kwenye mkutano wa kuongelea ripoti anamaiki mbili huku Diamond akizungumzia video za utupu akiwa na maiki kumi na tano za media kubwa acha waimbe kaka
Kwani we hupendi.Ndio wasikilizaji wanachopenda
Napenda kidogoKwani we hupendi.