Hivi kwanini bandari na uwanja wa ndege havionekani mtandaoni?

pererge

JF-Expert Member
Nov 8, 2012
570
250
katika website ya 'live ships map' nimeweza kuiona bandari ya jirani zetu kenya, visiwa vya comoro, madagasca, msumbiji na afrika kusini ambapo zinaonekana taarifa za meli nilizotia nanga, zinazoingia na zinazotoka isipokuwa bandari ya Dar es Salaam ndio haionekani kabisa ingawa hadi mwanzoni mwa mwaka huu ilikuwa ikipatikana. kuna tatizo gani na mnara wa rada upo bado mpta kabisa pale kivukoni? mwenye kulijua hili naomba atufahamishe.

Kwa upande wa uwanja wa ndege hali ni hiyo hiyo, ukiingia kwenye 'live filght tracker' utauona uwanja wa ndege wa Nairobi na Bujumbura ( kwa majirani zetu). Dar na Kia havionekani. Muda huu nimejaribu kuiangakia ndege moja ambayo imetokea Nairobi kuelekea S/Africa, imekuwa ikionekana hadi ilipofika usawa wa anga la kilimanjaro imepotea (siioni tena mtandaoni). Je situliwahi kununua rada ya kisasa kipindi cha Mkapa kwa ajili ya Uwanja wa Dar? kwani haifanyi kazi?
Naomba kujuzwa wandugu.
 
Mipangomingi

JF-Expert Member
Mar 16, 2011
2,714
2,000
Mambo ya Nchi hiyo yanafanyika utadhani watu wake ni wanyama. Wanaotakiwa kuwezesha taarifa nyingi za nchi kufahamika wana-surf JF tu na kusubiri kupiga deal. Huko ulikoenda ni mbali sana maana hata hizo ndege hatuna, ingia kwenye website za Wizara ndiyo utachoka. Ukikutana habari mpya saaana, basi hotuba ya waziri aliyotoa miezi saba iliyopita. Ukiingia kwenye website za Vyuo hata Course curriculum hazipo, sikwambii Prospectus. Ua umeshawahi kujiuliza iwapo kuna vipindi kadhaa vya nchi ambavyo umeviona kwenye vyombo vya Habari vya Kimataifa kwa mfano Aljazeera ambapo nchi kama Kenya imekuwa mstari wa mbele sana kwa habari zake kutangazwa na kituo hicho? Viongozi na watendaji wake wanatembea sana nje ya Nchi lakini wakifika huko wanakuwa busy na kushangaa miundombinu na wanawake ili kujiandikia rekodi kwamba wanawajua wanawake wa nchi fulani walivyo. Je ushaiangalia ramani ya Tanzania namna inavyozungukwa na maji (Nyasa, Victoria, Tanganyika, India strip na mito mikubwa) lakini wakazi wake hawana maji wala umeme? Hiyo Nchi imelaaniwa, huo ndio ukweli japo najiuliza ni kosa gani walilofanya wazee wetu huko nyuma hata ikalaaniwa?
 
pererge

JF-Expert Member
Nov 8, 2012
570
250
Interejensia yetu hairuhusu mambo hayo mkuu!

Sidhani, huko kwa wamarekani wenyewe viwanja vyote viaonekana ndege live zinaingia zinatoka. Nchi nyingi tu hadi Israel wako wazi tu taarifa za ndege ilinradi ni za abiria, zinasaidia hata wasafiri kuelewa kama leo usafiri upo au la ukiwa tu umekaa nyumbani sio hadi uende airport.
 
pererge

JF-Expert Member
Nov 8, 2012
570
250
Mambo ya Nchi hiyo yanafanyika utadhani watu wake ni wanyama. Wanaotakiwa kuwezesha taarifa nyingi za nchi kufahamika wana-surf JF tu na kusubiri kupiga deal. Huko ulikoenda ni mbali sana maana hata hizo ndege hatuna, ingia kwenye website za Wizara ndiyo utachoka. Ukikutana habari mpya saaana, basi hotuba ya waziri aliyotoa miezi saba iliyopita. Ukiingia kwenye website za Vyuo hata Course curriculum hazipo, sikwambii Prospectus. Ua umeshawahi kujiuliza iwapo kuna vipindi kadhaa vya nchi ambavyo umeviona kwenye vyombo vya Habari vya Kimataifa kwa mfano Aljazeera ambapo nchi kama Kenya imekuwa mstari wa mbele sana kwa habari zake kutangazwa na kituo hicho? Viongozi na watendaji wake wanatembea sana nje ya Nchi lakini wakifika huko wanakuwa busy na kushangaa miundombinu na wanawake ili kujiandikia rekodi kwamba wanawajua wanawake wa nchi fulani walivyo. Je ushaiangalia ramani ya Tanzania namna inavyozungukwa na maji (Nyasa, Victoria, Tanganyika, India strip na mito mikubwa) lakini wakazi wake hawana maji wala umeme? Hiyo Nchi imelaaniwa, huo ndio ukweli japo najiuliza ni kosa gani walilofanya wazee wetu huko nyuma hata ikalaaniwa?

Hiyo kitu nimeshaiona sana, website nyingi za serikali ukiingia ili upate taarifa unakuta haijawa updated karibu mwaka mzima.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom