Dr Slaa na Lissu ndo waasisi wa ajenda ya kupambana na mafisadi. Hawa waliwataja orodha ya mafisadi ( list of shame) pale Mwembeyanga Temeke bila hofu wala kupepesa macho. Baadae wababe hawa walizunguka nchi nzima na ajenda hii katika uchaguzi wa mwaka 2010.
Baada ya mmoja wa mafisadi waliotajwa Mwembeyanga, yaani Lowassa, kuingia upinzani, ajenda ya ufisadi ikafa midomoni mwa ukawa na kuhamia kwa CCM na Magufuli. Katika kampeni zake, Magufuli aliahidi kujenga mahakama ya mafisadi ili Lowassa ashtakiwe na afungwe.
Hivi sasa Lowassa amerudi CCM.
Katika uchaguzi huu, pande zote mbili yaani CCM na Upinzani umeua ajenda ya ufisadi. Lakini sio kwamba ufisadi haujafanyika awamu hii. Upo tena babalao ufisadi.
Sasa ni jambo la kushangaza, hakuna hata mgombea mmoja anayekerwa na ufisadi. Sio Lissu wala sio Magufuli. Je, kuna siri gani?