Hivi kwani ni Lazima Lowassa asikike kwenye media kila mara?

Stroke

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
36,970
45,849
Nashindwa kumuelewa huyu mstaafu maana naona kama vile anapenda media kuliko wenzake.

Kila wiki mara utasikia kaongea na wazee wa chadema, mara madereva boda wamemfuata ofisini kwake, mara waandishi wa habari wamemtembelea.

Nashindwa kuelewa anatumia kofia ipi kumake headlines;

1. Waziri mkuu mstaafu;

Malechela, Msuya, Sumaye, Pinda, warioba, wote hawa wastaafu wenzake wapo kimya mpaka pale inapobidi hutoa statement.

2. Mgombea Urais;

Uchaguzi umeshaisha; Mwighira wa ACT, hashim Rungwe; dovutwa na wenzake wote wapo kimya.

3. Mwananchi wa kawaida;

Kina sisi, wa kawaida hatuongei na media kila mara.

Kama uchaguzi umeshaisha na yeye kashindwa, na kampeni za uchaguzi wa 2020, hazijafunguliwa rasmi, sioni umuhimu wa kumake headlines kila mara. sio vibaya akapumzika kidogo na kuchagua kuzungumza pale inapobidi, sioni ni kwanini kila mara tumuone kwenye media wakati hana cheo chochote chadema wala hagombei nafasi yoyote.
 
Tunaweza kuitafsiri tabia hii ya EL kwa maneno haya-'the last kicks of a dying horse.' Usihofu njoo 2020 EL hatakuwa tishio tena. Niamini.
 
Tatizo za elimu ya shule za kata huwezi kuelewa kuwa watu wa media wanafanya biashara. Na habari zinazouza ni zile za wenye majina makubwa. Kwa hapa Tanzania kwa sasa jina kubwa kuliko yote ni Lowassa ndio maana hata akienda kuchunga ng'ombe zake anaandikwa na kila mtu anakimbilia gazeti. Na watu wa media hawawezi kuacha kufanya biashara eti kwa kuwa kuna watu roho zinawauma. Kama roho inakuuma kula malimao au ipotezee habari ya Lowassa usinunue gazeti
 
Eti jina kubwa kuliko yote ni lowassa teh teh nyumbu bhanaa muache aitwe nyumbu kwa kweli maana hakuna namna labda tu kwa faida yako Jina kubwa kwa sasa ni MAALIM SEIF SHARIF HAMAD km ulikuwa hujui chukua hii.
 
Eti jina kubwa kuliko yote ni lowassa teh teh nyumbu bhanaa muache aitwe nyumbu kwa kweli maana hakuna namna labda tu kwa faida yako Jina kubwa kwa sasa ni MAALIM SEIF SHARIF HAMAD km ulikuwa hujui chukua hii.
Kwani Mssh si wa Zanzibar? Anyway Tanganyika Lowassa ndo Juu. Tulia upewe buku Saba jioni. C Jana 2.1GPA kasema mkumbukwe?
 
Samahani hivi Tanganyika ndio wapi na Tanzania ni wapi maana hueleweki nyumbu.
 
Kuongea ni haki yake kikatiba,ukiona anakukera usisikilize wala kusoma media zenye habari zake!
 
Kama unaona kero LOWASSA kusikika kwene media ata wewe usinge mtaja humu, ujiskii aibu? Unajidai utaki jambo flani wakati ww mwenyewe hilo jambo flani unalitangaza
 
Kina kitu kinaitwa kiburi. Binadamu anaposhindwa kuelewa kwamba anacho kitu hicho ndani yake, halafu hata marafiki wa karibu nao wakishindwa kutoa ushauri, matokeo yake ndio hayo ya mzee wa monduli. Huwa nashangazwa, wakati mwingine hutoa maagizo, yaani kila waziri mkuu mstaafu akitoa agizo, rais atafanya kazi gani!!. Aliutaka sana urais, nadhani kuwa bado haamini kwamba jambo halijawezekana. Ni kweli nguvu nyingi imetumika lakini mikakati haikufanikiwa.

Kuna kitu kingine kinaitwa wivu. Ile tabia ya kujiona kuwa unastahili kuwa wewe na sio mtu mwingine. Anayetoa riiziki ni Mungu. JPM alienda kuchukua fomu bila ya mbwembwe zozote zile, lakini leo ndio rais halali. Anayejikweza hushushwa, sikuona haja ya mzee wa monduli kuchukua fomu akiwa na msururu mkubwa wa watu. Imetumika fedha nyingi na mtu anapokaa chini na kutafakari muenendo mzima wa mambo yaliyofanyika kwa nia ya kupata urais, ni lazima wivu uutese moyo.

Hizo njia zote zinazotumika ili kuonyesha kwamba bado mzee wa monduli anayo credibility kwenye jamii, pia zinamsaidia binafsi katika kujifariji. Yaani ile vita ya ndani kwa ndani kwenye nafsi ya mtu huambatana na baadhi ya tabia zinazoweza kuonekana hadharani. Yote kwa yote huu ni mwaka 2016, uchaguzi mwingine ni mwaka 2020, yakufanyika ni mengi tena kwa faida ya maisha ya mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.
 
Back
Top Bottom