Hivi kwani kampeni zimeanza!! Huyu mbona anafanya! Tena bungeni!!?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi kwani kampeni zimeanza!! Huyu mbona anafanya! Tena bungeni!!??

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Tasia I, Apr 24, 2010.

 1. T

  Tasia I JF-Expert Member

  #1
  Apr 24, 2010
  Joined: Apr 21, 2010
  Messages: 1,226
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  ............. Pinda na Sitta si mihogo kiasi cha kung'olewa kirahisi majimboni mwao kama mkulima anavyoweza kung'oa mihogo shambani kwake," alisema Shibuda ambaye anajulikana kwa kutokuwa mwoga kuzungumza kinachomkera.

  ............Mheshimiwa spika, katika kusimamia imani ya Chama Cha Mapinduzi, umesimama imara, kusimamia katiba na kanuni.
  Umesimama imara na hata katika kusimamia haki za wafugaji, ulisimama imara. Mheshimiwa spika, uzalendo wako ni mkubwa na ninawaomba wananchi wa Urambo Mashariki mnyonge mnyongeni, lakini haki yake mpeni," alisema Shibuda.

  ...........Mheshimiwa spika umefanya Bunge kuwa kioo cha kutetea maslahi kwa wananchi kwa hiyo nawapongeza wabunge wote kwa kutekeleza na kutimiza mkakati wa kutetea maslahi ya Watanzania kama tulivyoapa kutetea maslahi ya nchi yetu.”
  Awali kabla ya kumsifia Spika Sitta Shibuda alianza kumsifia Waziri Mkuu Mizengo Pinda akimwelezea kuwa ni mnyeyekevu, msikivu na ambaye amekuwa akifanikisha mipango mizuri ya serikali.

  .............Baada ya kumaliza kutoa sifa hizo, Shibuda aliwataka wakazi wa jimbo la Mpanda anakotokea waziri mkuu huyo kuhakikisha wanamchagua tena Pinda kuwa mbunge wao katika uchaguzi mkuu ujao.


  Source: mwananchi gazeti.
   
 2. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #2
  Apr 24, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,668
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Ukishangaa ya Mussa utaona ya filauni. Si unaujua msemo huu?
   
Loading...