Hivi kwa wakazi wa Siha na Kinondoni kuna mgombea yeyote anayejinadi kupitia michezo?

fedson goodness

New Member
Jan 1, 2018
1
0
Kwenye majimbo kadhaa hapa nchini kwetu kunafanyika uchaguzi wa marudio, uchaguzi ambao kampeini zimejawa na Sera za kila aina, lakini wasiwasi wangu ni je katika kampeini hizo kuna mgombea yeyote anayejinadi kukuza michezo jimboni kwake?

Achilia mbali kugawa jezi,mipira na vifaa vingine vya michezo kama njia ya ushawishi kwa vijana ili wawaweke madaraka, je kwenye kampeini zao suala la michezo linatajwa?

Wagombea wengi wamejikita kwenye kurushiana maneno na kunadi Sera nyingine na kusahau kuwa wapiga kura wao ni miongoni mwa wapenda maendeleo ya michezo katika maeneo yao.

Wakumbuke kwamba michezo ni ajira, michezo huleta maendeleo pia michezo hupunguza vijana wenye kujihusisha na uhalifu kwenye jamii.
 
Back
Top Bottom