Hivi kwa viashiria hivi tutarajie nini?

RtsHjcq

JF-Expert Member
Aug 19, 2017
4,753
5,504
Mara baada ya Ndege ya Ethiopia kupata ajali..Naona kumekuwa na usitishwaji wa kampuni ya Boeing baadhi ya nchi mbali mbali TAZAMA

China imeyaagiza Mashirika ya ndani Ndege nchini humo kusitisha kuzitumia kibiashara Ndege aina ya Boeing 737 MAX 8...

‪Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya Singapore imekataza matumizi ya Ndege aina ya Boeing 737 MAX katika anga la nchi hiyo kufuatia Ndege ya muundo huo ya Shirika la Ndege la Ethiopia kuanguka March 10 na kuua Watu wote 157 waliokuwemo ndani ya Ndege hiyo.....

‪Kampuni ya Boeing imeahirisha wiki hii kuionesha Ndege yake mpya aina ya 777X jetliner baada ya Ndege iliyotengenezwa na kampuni hiyo aina ya 737 MAX 8 ya Shirika la Ndege la Ethiopia kuanguka na kusababisha vifo vya Watu 157 (Abiria 149 na Wafanyakazi). (CNN)‬

‪Korea Kusini imesitisha matumizi ya Ndege aina ya Boeing 737 MAX 8 baada ya Ndege ya muundo huo ya Ethiopia kuanguka March 10 na kuua Watu 157, ikumbukwe kuwa Ndege ya muundo huo pia ya Shirika la Lion Air la Indonesia ilianguka October 2018 na kuua Watu 189.

Kampuni ya Boeing Marekani inayotengeneza ndege iliyoanguka Ethiopia imesitisha matumizi ya ndege zote aina hiyo baada ya wachunguzi kubaini ushahidi mpya katika eneo ambako ndege ya Ethiopia Airlines ilianguka na kuua watu 157.

Kampuni hiyo ya Marekani imesema itasitisha usafiri wa ndege zote 371 zinazohudumu.

Shirika linalosimamia usafiri wa anga Marekani FAA, limesema ushahidi mpya pamoja na data mpya za satelaiti zimechangia uamuzi huo wa kupiga marufuku kwa muda usafiri wa ndege hizo.
FB_IMG_1552374069114.jpeg

FB_IMG_1552374064037.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hizo nchi zimesitisha matumizi ya Boeing 737 Max 8 katika anga la nchi zao, tanzania hatuna toleo hilo la ndege.
 
Kwani zile zilizokuja juzi ni zipi???

Sent using Jamii Forums mobile app
tuna airbus na ile boeing

Ile boeing sio sawa na hii 8MAX ile yetu ni DREAMLINER yaani aina moja ila matoleo tofauti

Mfano Toyora wametengeneza LAND CRUISER VX sie tukanunua hili VX Baadae sana wakatengeneza LAND CRUISER V8. baadae ikabainika V8 inasababisha sana ajali ikapigwa marufuku,marufuku hiyo haitoihusu ile VX itaihusu hii V8 tuuu
 
Tanzania tunaye engineer huwa anwaambia wakulu anatengeneza ndege zote hizi kule Boeng. Hivyo hawatafanya lolote mpaka awaambie nini cha kufanya. Aliitengeneza Dreamliner, akatengeneza bombardier, na hata yale mapangaboy alitengeneza yeye, kasoro hizi zinazoanguka KIFAFA hajazigusa yeye, anyaway kuweni wapole hatujapata tarifa za kiinteligesia za namna ya kudeal na hili. Isitoshe ndege inanunua ccm, ingekuwa za chadema zipo lazima zingepigwa pin tu hakuna namna.
 
tuna airbus na ile boeing

Ile boeing sio sawa na hii 8MAX ile yetu ni DREAMLINER yaani aina moja ila matoleo tofauti

Mfano Toyora wametengeneza LAND CRUISER VX sie tukanunua hili VX Baadae sana wakatengeneza LAND CRUISER V8. baadae ikabainika V8 inasababisha sana ajali ikapigwa marufuku,marufuku hiyo haitoihusu ile VX itaihusu hii V8 tuuu
Kwaiyo inamaana sisi tumechukua old model eet

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom