Hivi kwa umri wa miaka 41 niliofikisha naweza kutoboa maisha au ndio basi tena?

Pmoses95

Member
Apr 16, 2014
43
157
Wana JF hivi kuna uwezekano wa kufanikiwa kiuchumi unapokuwa na umri wa kuanzia 41?

Mpaka sasa nina mke na watoto watatu. Sina shughuli rasmi, nabangaiza tu.

Naanza kuona kama ndoto yangu ya kuwa na mafanikio kiuchumi inafifia.

Swali langu ni kwenu ninyi Wana JF. Hivi kuna possibility ya kutoboa kwa umri huo? Au ndio nishazeeka Tena!
 
Bado sana unajipa wasiwasi watu wametoboa na 60 mzee wa KFC. Ukifuatilia mtajiri wengi wako 65 na kuendelea na wako poa tu ukiwa na pesa hata miaka 60 unakuwa kawaida maana akili inafanya kazi muangalie Bill Gates, Jeff wako smart ila umri umeenda.

Bado sana kabisa sema kama una majukumu mengi na bado muelekeo hata nyumba bado inakurudisha nyuma kimtindo hata risk kubwa huwezi kuchukua.
 
Bado sana unajipa wasiwasi watu wametoboa na 60 mzee wa KFC...ukifuatilia mtajiri wengi wako 65 na kuendelea na wako poa tu ukiwa na pesa hata miaka 60 unakuwa kawaida maana akili inafanya kazi muangalie bill gates, Jeff wako smart ila umri umeenda.
Bado sana kabisa sema kama una majukumu mengi na bado muelekeo hata nyumba bado inakurudisha nyuma kimtindo hata risk kubwa uwezi kuchukua.
Namshukuru Mungu nyumba ninayo mkuu. Kwa malazi tu, familia inalala pazuri.
 
Usikate tamaa jombaa, kuna sehemu Bado wanahitaji ujuzi wa mikono yako, ni Swala la muda tu, huo umri Bado sana. Kuna boss wangu mmoja mzungu wa SA, ana miaka, 68!

Alipofukuzwa kazi kwenye kampuni yetu, akarudi kwao, akaendelea kutafuta ajira, maana na Cha msingi ujuzi anao, kampuni moja ya Ulaya ikamuona ikamchukua, sasa hivi ana 70+na ni country manager East Afrika nzima, anakula bata tu na anachapa kazi ni energitic kama balobalo wa miaka 30!! Usikate tamaa mangi endelea kuwa na ndoto, tukate tamaa pale tu tutakapo nyamaza milele.
 
Wana JF hivi Kuna uwezekano wa kufanikiwa kiuchumi unapokuwa na umri wa kuanzia 41 ?
Mpaka Sasa Nina mke na watoto watatu. Sina shughuli rasmi, nabangaiza tu.
Naanza kuona Kama ndoto yangu ya kuwa na mafanikio kiuchumi inafifia.

Swali langu ni kwenu ninyi Wana JF . Hivi Kuna possibility ya kutoboa kwa umri huo ? Au ndio nishazeeka Tena!

Maisha ni imani, chochote kinatokea muda wowote. Una nafasi kubwa ya kuwa milionea kuliko kupigwa radi. Hata waliofanikiwa kiuchumi kabla ya 40 huweza kuanguka tena na kurudi sifuri ila hia hawakati tamaa hupambana na kurudi tena katika uchumi mkubwa
 
Back
Top Bottom