Hivi kwa Tanzania ni lazima ukiwa Mwanasiasa pia uwe na uwezo mkubwa wa kuwa Mnafiki na Muongo?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,464
108,619
Kauli ya mwaka 2018

"Natoa Wito kwa Wakuu wote wa Mikoa hadi wale wa Wilaya kuhakikisha kuwa kila Mfanyabiashara mdogo mdogo wa Kitanzania (Wamachinga) awe na Kitambulisho ndipo aweze Kufanya Biashara yake. Ole wake kwa Mkuu wa Mkoa na Mkuu wa Wilaya ambaye nitakuta Mkoa wake haujalitimiza hili kwani ni Jambo la lazima ili Serikali ipate Mapato yake"

Kauli ya mwaka 2020 tarehe 22 Septemba

"Sitaki Wamachinga wowote ambao watakutwa hawana Vitambulisho vya Kufanyia Biashara wafukuzwe au wabughudhiwe. Muwaache wafanye Biashara zao na ole wake kwa Kiongozi yoyote yule ambaye atawasumbua. Na siyo lazima sana Wafanyabiashara hawa (Wamachinga) wawe na hivyo Vitambulisho. Nadhani mmenisikia hivyo muwaache kabisa "

Kuna Watu wanadhani Tanzania ile ya miaka ya 1940's iliyokuwa na Chuo Kikuu kimoja tu, basi pia ndiyo hii ya leo ya 2020 yenye Wasomi wengi.
 
Mwaka huu mpaka watakana hata vyeo na nguo walizokuwa wanavaa! Hoja za Lissu sio mchezo! Lakini ushauri wa bure mie nawapa CCM, wakitaka kusalimika sio kukana matendo yao wenyewe bali watubu na wawaombe radhi waathirika wote.

1. Wawaombe radhi machinga waliopewa sekeseke la vitambulisho hivyo na wawarudishie 20 yao

2. Wawaombe radhi waliowabomolea nyumba bila fidia na wawalipe walichostahili kulipwa

3. Wakawaombe radhi Wahaya kule Bukoba na wawape pesa zao za tetemeko

4. Wawaombe radhi watumishi wa umma na wawafidie fedha zao walizo wadhulumu miaka 5 na wawapandishe madaraja wote wanaostahili.

5. Wawaombe radhi wanufaika wote wa mikopo ya elimu ya juu, washushe riba ya marejesho mpaka 8% na wawarudishi fedha zao wote waliokatwa toka 2016.

6. Wawaombe radhi raia na wapinzani kwa kuwadhulumu kufanya shuguli halali za kisiasa na misukosuko yote waliyowapayisha!

Kiukweli waungame kila dhambi wanayoamini kuwatendea Watanzania na kama kuna fidia ya athari wawalipe ndipo wajuwe salama yao!
 
Sio tu bongo mpaka n'gambo hakuna uhuru wa habari. Kuna uhuru wa mwenye chombo mitambo na mwenye mali.

Screenshot_2020-09-17-06-42-18-1.jpg
 
Bahati nzuri zote zipo hivyo ni 'Jukumu' lako 'Popoma' Mwandamizi kama Wewe Kuzitafuta kutoka katika Vyanzo mbalimbali tu ili Ujiridhishe sawa?
Unapoquote weka ni Lini, wapi, ikiwezekana na tarehe.

Sio kishabikishabiki kama umeandika Uzi wa chitchat
 
Wawaombe radhi wastaafu na waathirika wa FAO LA kujitoa

Wawaombe radhi ndugu wa waliotekwa
wote

Waseme Ben Saa nane yu wapi

Waliookotwa ufukweni kwenye viroba

Wamuombe radhi CAG Assad na billion 7 zilipotelea wapi

Wawaombe radhi vijana wa Udom aliowaita vilaza
 
Dunia ya sasa ogopa vitu viwili, Mungu na teknolojia. Zamani kwa vile taarifa hazikuwa zikipatikana kirahisi na pia utunzaji wake haukuwa rahisi , basi viongozi waliweza kuwalaghai wananchi walivyopenda. Kwa sasa kila kitu kipo mtandaoni na ukifanya mchezo utaishia kula matapishi yako.
 
Back
Top Bottom