Hivi kwa sasa kuna mtayarishaji wa midundo mkali kama S2kizzy Tanzania?

Nafaka

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
12,156
31,028
Kila zama na kitabu chake, ilikuwepo zama za Bongo Records na akina Majani, Prof. Ludigo, Soggy Doggy, Bizzman n.k wakidondosha midude ya level nyingine. Huku alikuwepo MJ Records, kule Mawingu Studio, pale Sound Crafters, pande zile G-Gecords, mara kuna G2 kwa Roy.

Zama zikaja za Dunga akiwa na Lamar, Lamar akaondoka akafungua Fish Crab naye akapita.

Kuna maproducer wamebaki kwa muda mrefu japo hawako high au low mfano wake ni Bob Maneck na AM Records jamaa yupo kwa muda sana maana akina Bob Juniour wamekuja wakamtoa Diamond, wakapotea lakini yeye kabaki.

Sasa kuna hawa watengeneza midundo wa kizazi hiki ambao kiuhalisia siyo maproducer bali ni mabeat makers japo wengine wamejiendeleza zaidi na kutokana na kupata uzoefu wameweza kufanya mengi. Mmojawapo ni S2kizzy a.k.a Zombie. Huyu dogo ana mkono hatari sana anatengeneza kila aina ya mdundo na ni mbunifu sana kwani sauti nyingi unazozisikia kwenye beat amezipiga kwa mdomo wake akazitune akaziwekea effects zikasound kama unavyosizikia mfano.

Wimbo wa Rich Mavoko - Rudi ya Rich Mavoko kuna kisauti kinaria kama kopo fulani inagongwa gongwa mwanzo mwa beat kabla rich hajaanza kuimba, ile aliipiga kwa mdomo.

Kwenya kanyaga kanyaga -Diamond, kuna kisauti kinaanza kwenye intro, na kiko baada ya chrorus kabla verse ya pili ile aliipiga kwa mdomo. Kuna interview wanamhoji majani alisema yeye anawatambua maproducer wakali kama akina S2kizzy

Dogo katengeneza hits kibao maana nadhani kila hits 10, 5 zina mkono wake. Pilia nabadirika badirika mfano
Quarantine.

Wanaona haya
Far Away - Diamond ft Vanessa
Tetema - Rayvanny
La Moto - Moni Central Zone
Nizikwe Tu - Billnas
Nyimbo zote za Wozzu. Kuna nyimbo nyingi sana
 
Kimambo on the beat japo ni kama ana sample beat za watu halafu anaziboresha zaidi. mfano Acha Lizame inafanana na Paranawe ila yenyewe ni kali zaidi. Pia so hot ya kiba imefanana na abi ya krizbeat aliomshirikisha Diamond Ila jamaa ni mkali.
 
S2kizzy bwana! Umeona km huonekani, tunakuona kaka we piga tu kazi ukifa tutakusifia.... Acha haraka basi!
We S2kizzy kazi zake ziko wazi kwasasa hahitaji promo langu hata mimi nimemjua kwa kazi zake
 
Ndugu mleta mada unaposema s2kiss anabadilika maana yake nini?
Sikiliza beat ya la moto ni tofauti sana na beat ya far away na ni tofauti sana beat ya tunavesha na ni tofauti sana na beat ya wanaona haya na ni tofauti sana na beat ya kanyaga kanyaga.
 
Kwenye wimbo wa quarantine hile sauti imetokana na mlio wa simu ya iPhone kama umewai tumia iPhone ukiiweka chaji kuna kisound flani kinatoka Jamaa ndo akapita nacho
 
VP unamjua kweli @NAREHEL
Zama zake zishapita kama unabisha nitajie hit track toka kwake ya 2019 mpaka hii 2020. Kuna videoclip nilimuona s2kizzy akiwa na Nahreel studio nahreel anamwambia ila wewe jamaa ni noma na unatengeneza ela kweli.
 

Similar Discussions

8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom