Hivi kwa nini Watu wa Morogoro wanapenda sana ugomvi na mabishano?

rosemarie

JF-Expert Member
Mar 22, 2011
6,887
3,412
Tuliingia Morogoro juzi na tumekaa ni siku ya tatu lakini sijafurahishwa na jinsi watu wa Morogoro wanavyopenda kujisifu,maugomvi na hawapendi kabisa kuona mtu yeyote hasa asiye toka Morogoro aongee kitu mbele yao
Tumekaa Mbeya na Tunduma kama nilivyowaletea kisa cha mihela ya bwerere huko Tunduma mwishoni mwa mwaka jana
tukiwa Mbeya kwa takriban week tatu hatujawahi kugombana na mtu yeyote awe bar maid au dereva tax au mtu yeyote yule tuliyekutana mahali popote
kwa mtazamo wangu wa haraka haraka watu wa Mbeya wana akili sana na wana uwezo mkubwa sana wa kumsoma mtu,hilo wana Mbeya nawapa hongera ndio maana maendeleo kwenye mkoa wenu yanakuja kama mvua yaani speed ya ajabu
sasa tupo Morogoro ni siku ya tatu lakini tumeshagombana na watu mara nne??unaweza kuamini hilo??tumegundua watu wa marogoro wanapenda sana ugomvi,hata kama anafanya kazi mahali pa kutoa huduma na wewe ni mteja anaweza kugombana na wewe,,naomba kuuliza hawa watu wa morogoro ni watu wa aina gani??halafu wanakuwa kama hawajiamini,yaani ukiongea naye usipokuwa makini anaweza kusema umemdharau kumbe siyo,halafu wanakuwa kama hawapendi watu wanaotoka nje ya Morogoro??inawezekana hawa watu ni wabaguzi???jamani naombeni mnisaidie kwenye hilo,tupo hapa ni siku ya tatu lakini nawahimiza wenzangu tuondoke maana tunaogopa kugombana na watu
 
Aaaah usijaribu kutengeneza league ya kubishana na watu Morogoro, af kuna kuna lugha ya kuongea kwa kutaja jina la mtu huku akimaanisha vingine..
Bure Mtagwa > Kitu cha bure.
Yusuf Macho> Unaangalia sana
 
Morogoro mnawaonea. Nendeni Kigoma ndio mtajua duniani kuna watu na viatu

Upo sahihi hata mjini hapa watu wa kigoma wanajidai wanajua kila kitu pengine hata mwezi hajamaliza..wabishi sana hili la ukweli..kuhusu morogoro ndo ninasikia leo.
 
Aaaah usijaribu kutengeneza league ya kubishana na watu Morogoro, af kuna kuna lugha ya kuongea kwa kutaja jina la mtu huku akimaanisha vingine..
Bure Mtagwa > Kitu cha bure.
Yusuf Macho> Unaangalia sana

Afande Sele ni mkazi wa morogoro..
 
tuliingia morogoro juzi na tumekaa ni siku ya tatu lakini sijafurahishwa na jinsi watu wa morogoro wanavyopenda kujisifu,maugomvi na hawapendi kabisa kuona mtu yeyote hasa asiye toka morogoro aongee kitu mbele yao
tumekaa mbeya na tunduma kama nilivyowaletea kisa cha mihela ya bwerere huko tunduma mwishoni mwa mwaka jana
tukiwa mbeya kwa takriban week tatu hatujawahi kugombana na mtu yeyote awe bar maid au dereva tax au mtu yeyote yule tuliyekutana mahali popote
kwa mtazamo wangu wa haraka haraka watu wa mbeya wana akili sana na wana uwezo mkubwa sana wa kumsoma mtu,hilo wana mbeya nawapa hongera ndio maana maendeleo kwenye mkoa wenu yanakuja kama mvua yaani speed ya ajabu
sasa tupo morogoro ni siku ya tatu lakini tumeshagombana na watu mara nne??unaweza kuamini hilo??tumegundua watu wa marogoro wanapenda sana ugomvi,hata kama anafanya kazi mahali pa kutoa huduma na wewe ni mteja anaweza kugombana na wewe,,naomba kuuliza hawa watu wa morogoro ni watu wa aina gani??halafu wanakuwa kama hawajiamini,yaani ukiongea naye usipokuwa makini anaweza kusema umemdharau kumbe siyo,halafu wanakuwa kama hawapendi watu wanaotoka nje ya morogoro??inawezekana hawa watu ni wabaguzi???jamani naombeni mnisaidie kwenye hilo,tupo hapa ni siku ya tatu lakini nawahimiza wenzangu tuondoke maana tunaogopa kugombana na watu
nadhani ni kwa sababu ya ufupi.
 
Kigoma wewe noma,wanajifanya wajuajiiiiiiiii diamond zitto ali kiba ngasa
 
Makabila mengi ya milimani wanapenda sana ubishani na malumbano.
Mfano, Wakinga, Wapare, Waluguru etc
Acha kutoa majibu ya ovyo ovyo. Toa sababu yenye mshiko, kwa nini hawa watu wa milimani ni wabishi na wapenda malumbano?
 
Ukisema watu wa Morogoro una maanisha nini? Watu wote wanaoishi morogoro? Watu wenye asili ya morogoro? Hebu kuwa specific kidogo mkuu
 
Ni asili ya kizaz chao toka mababu zao. Hao walozarisha hyo tabia ni wapogoro. Jina lao lilitokana na mtu alokuwa mgeni kwenda hko na kila jema alilofanya walimbeza basi jamaa akahitimisha kwa kusema ardhi ya MIGOGORO. hilo likiwa jina baada ya wageni kushindwa kutaja neno Mgogoro wakaita MGOROGORO na baadae wakaja weka sawa na kuita Morogoro. Hivyo basi wabantu hao wakawa wamepata jina la Wabantu wa eneo hilo kama wapogoro. HIVYO BASI USISHANGAE KAKA.
 
Ukisema watu wa Morogoro una maanisha nini? Watu wote wanaoishi morogoro? Watu wenye asili ya morogoro? Hebu kuwa specific kidogo mkuu

Mkuu kwa kweli hatuelewi kama wale wana asili pale au wanaishi pale lakini tunahisi tabia kama zinafanana vile,sisi pale ni wapitaji tunashindwa ku figure out
 
watanzania wote wanapenda porojo hata wewe mtoa mada unasomeka hivyo coz maelezo mengi yanajirudia rudia,nenda mikoa yote hata tatizo ni uchangamfu wa watu eneo husika. hata hao unao sema ni wa moro wengi wamehamia tu miji ming inawatu waliohamia
 
Njoo MUSOMA mkuu...naona hujawahi kukutana na watu wabishi na wagomvi weye.........

Mkuu asigwa, kwa tabia yake ya kupenda kubishana na wenyeji, ingekuwa Musoma sasa hivi angekuwa umelazwa DDH ilihali Mtenda kosa kakimbilia kizingani au Kenya.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu asigwa, kwa tabia yake ya kupenda kubishana na wenyeji, ingekuwa Musoma sasa hivi angekuwa umelazwa DDH ilihali Mtenda kosa kakimbilia kizingani au Kenya.

yapni kweli aisee...tena mwenyeji akimaliza kazi anakwenda MWIGHOBELO anapanda boti huyoo anazama zake KIBUI....
 
Mkuu kwa kweli hatuelewi kama wale wana asili pale au wanaishi pale lakini tunahisi tabia kama zinafanana vile,sisi pale ni wapitaji tunashindwa ku figure out


Then usifanye hasty generalization, how do you know kwamba watu iliokwaruzana nao labla ni wachaga ua wakurya au wanyakyusa? Maana Tanzania ya leo sijui utaenda wapi ukute mji una wenyeji tu na hakuna mchanganyiko wa makabila, mimi siijui.

Halafu how do we know ulikua katika state gani wakati unakwaruzana na hao watu? Labla ulikua vyombo?

Nimeishi mbeya, Morogoro mpaka nimejenga, na sio mwenyeji kote huko na sijawahi experience hizo mambo unaleta hapa tena bora ungesema Mbeya huko lakini sio Moro,Mbeya kuna eneo linaitwa Mbozi, muulize mwenyeji yoyote wa mbeya atakusimulia habari za watu wa mbozi.
 
Back
Top Bottom