Hivi kwa nini wanawake wa siku hizi hawafahamu kupika vyakula vizuri | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi kwa nini wanawake wa siku hizi hawafahamu kupika vyakula vizuri

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mshume Kiyate, Oct 16, 2011.

 1. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #1
  Oct 16, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Wana JF.
  Siku za karibu nilipata mualiko kutoka kwa rafiki yangu moja kula chakula cha jioni.

  Nilipofika nyumbani kwa rafiki yangu, jamaa kanikalibisha vizuri pamoja na mke wake, chakula kikaletwa mezani.

  Tukaanza kupakua chakula kwenye sahani nilichokiona ni Wali na Sausage, ambazo wamefanya mboga pamoja na juice za box.

  Kwa kweli kila nikiweka mdomoni Wali na Sausage, radha yake inanishinda nikaamua kujiladhimisha tu mpaka nikakimaliza lakini nipo hoi.

  Ukimuona mke wa rafiki ni mrembo sana lakini hafahamu kupika, huu ni mfano mmoja tu, lakini nimeona wanawake wengi wa sasa hivi hawajui kupika.

  Wadau tatizo ni nini naomba tujadili hii kitu
   
 2. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #2
  Oct 16, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  aaiisee Wali na sausage ni bonge la disaster hata kama ukiamua uka fodge hio sausage upike kwa kuikalangiza. Sababu ni nyingi kwa kweli ambazo hupelekea hivo....

  Malezi...

  Wazazi wengi hasa Mama ambae ndio ana nafasi kubwa saana ya kumlea binti ili awe mwanamke kamilifu hua mara nyingi huchemka na kufikiri kwamb akimlea mwanae kisasa (kisasa hapa imekua defined vibaya) kua alelewe akiwa vidole juu.. bila kumfundisha kazi za msingi kama vile usafi wa nyumba... kufua nguo... mpangilio wa numbani na most importantly kupika.

  Elimu

  System ya elimu sasa hivi imebadilika saana... Na for the worse kwani watoto asilimia 95 ya maisha yake yamelenga tu elimu.... Mtoto toka grade one yupo boarding... mara anaesoma day anasoma na tuition (jamani imagine tuition ya darasa la kwanza)... Maisha yake yoote shule... Likizo akija anatafutiwa tuition na akirudi ajipumzishe na ajisomee... at the end of the day anakua a very great person careerwise but kupika hawezi...

  Ushamba & Ulimbukeni...

  Ladies wengine anaona sifa kusema kua hajui kupika... ili sijui aonekane matawi ama lah! sielewi.... For mie naelewa kua mtoto wa kike yeyote ambae amelelewa nyumba ya mama/mlezi anaejua kweli definition ya a true African woman... atamfundisha tu binti yeyote ndani kupika...awe mwanae ama lah ni muhimu mno.

  Uvivu...

  Kupika sio miujiza.... hata kama bahati mbaya ikatokea kua mtu hajui kupika ni muhimu akajituma na kujifunza na taratibu atajua.... Mwingine ni mvivu mno... ya akipika avavichemsha chemsha tu basi anaona kamaliza hakuna la ziada... Hata aende kwa mwenzie akapenda chakula hata kujisumbua na kuuliza vipi kapikaje habari hana kabisa!
   
 3. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #3
  Oct 16, 2011
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Mkuu AshaDii umeongea vizuri sana,

  Jambo lingine naloona hapa ni wanawake wengine wanaroho za kichoyo, wivu na kupenda kulipiza kisasi. Utakuta mwanaume keshamweleza kuwa kutakuwapo na mgeni siku ya leo au siku fulani lakini mwanamke anachukulia ndo muda wa kulipiza kisasi ugomvi wa siku za nyuma. Au utakuta mwanamke hapendi kuona wageni kwake, kwa hiyo anafanya vitu hovyo hovyo ili asitembelewe tena.

  Wangu mimi anajua, akicheza vibaya napanda mwenyewe jikoni natoka na kitu kikali kwa hiyo hawezi kufanya upuuzi wa kupika hovyo.
   
 4. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #4
  Oct 16, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Nakubaliana na AshaDii kwenye mchango wake ni kweli malezi yanachukuwa sehemu kubwa sana kwenye hili tatizo
   
 5. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #5
  Oct 16, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  Siku hizi mabinti wanaolewa tayari ana 'house girl' wake....
  Unategemea nini??????
   
 6. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #6
  Oct 16, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Dah!! Halafu unakuta nyumba ina house girl wawili
   
 7. Mhadzabe

  Mhadzabe JF-Expert Member

  #7
  Oct 16, 2011
  Joined: May 20, 2009
  Messages: 1,648
  Likes Received: 715
  Trophy Points: 280
  Haki ya MUNGU Ashadii leo umetoa jibu ambalo ni jibu! Nakugongea "ka senks."
   
 8. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #8
  Oct 16, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  kati ya yote hayo naona malezi yanachangia sana. mzazi akishaona an hg basi hataki binti afanye kazi yoyote. kama binti nae ni cha uvivu ndio kabisaaa. sio tu kupika hata kufanya usafi pia wengi hawajiwezi.
   
 9. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #9
  Oct 16, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  na wazazi wengine unakuta binti akiolewa na house girl wa nyumbani anahamia kwa binti....
  yaani...
   
 10. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #10
  Oct 16, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,052
  Likes Received: 3,082
  Trophy Points: 280
  Nakukubali sana AshaD..kwa kuongezea tu,wanawake watajua wapi kupika na wakati kula kwao ni chips na take away?...ndo maana wanaume tunaona haina haja ya kuoa kama hata kupika mke hajuhi ama anaona ni karaha

  NB.wanawake jamani hatuwahoi na kuwaleta ndani ili kuja ku-do tu,kama ndo hvyo ni bora nitembelee ambiance nikagonge za kikweli,nikikuleta ndani ni nafasi yako kujituma ktk kila jambo
   
 11. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #11
  Oct 16, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Nakumbuka home tulikuwa na house girl lakini alikuwa hagusi nguo zetu tulikuwa tunajifulia wenyewe na kufanya usafi wenyewe
   
 12. h

  hayaka JF-Expert Member

  #12
  Oct 16, 2011
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 476
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  kuwa na house girl hiyo sio tatizo! Shida kubwa kinadada wengi wamekuwa wavivu na hawajitumi wala hawana ubunifu.
   
 13. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #13
  Oct 16, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Yah!! Nimeishaona mara mbili hapo umenikumbusha kuna kijana mmoja alioa sasa mzee wake kwenye compound yake alikuwa na nyumba mbili sasa ile moja ndio akampa mtoto ndio awe anakaa humo humo watu wakawa wanasema hakuna tofauti maana unaingia geti mmoja na mzee wako ma-house girl walewale tena waliongezeka wakawa wanne ukijumlisha na wale wa mzee wake hapo bado haujazungumzia house-boy waliokuwepo yaani in total nyumba ilikuwa ina wafanyakazi wasiopungua sita house girl wanne na house boy wawili sasa hapo mtoto anaweza kujifunza hata kufagia kweli?
   
 14. G

  Gavanor Member

  #14
  Oct 16, 2011
  Joined: Oct 15, 2011
  Messages: 60
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  unidai soda baadae.
   
 15. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #15
  Oct 16, 2011
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  AshaDii aksante kwa jibu zuri sana.

  Mtoa mada tatizo ni kutojua kupika au aina ya chakula ulichokikuta? Nilitegemea ungesema wali ulikuwa mbichi! Inawezekana kabisa kuwa huyo mdada anajua sana tu kupika but siku hiyo hiyo ndo ilikuwa menyu of the day bana na wenyewe weshaizoea na wanaipenda!

  Ila ni kweli nakubaliana na jibu la AishaDii kwa asilimia zote!
   
 16. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #16
  Oct 16, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Na house boy mmoja wa kufua...
   
 17. klorokwini

  klorokwini JF-Expert Member

  #17
  Oct 16, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 8,710
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 135
  Heri hiyo wali na sausage! Niliwahi kutembelea nyumba moja nikawa napigwa juice tu, kila ikimaliza najaziwa. Halaf lile jidada likajifanya kuniambia kwa mbwembwe "Unajua shem? humu tunaish kizungu, tunakeep shape, si unajua figure ni muhim shem?, likamalizia na kicheko cha pwani" , Baada ya kufatilia nikaambiwa kumbe hauzigeli wao kaenda kijijini kumuuguza babaake wa kambo, hamna cha uzungu wala uhafu kasti.

  Dah! hasira za kukosa ubwabwa sku ile zilinifanya nizime sim kabisa yaani.
   
 18. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #18
  Oct 16, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Olooooo kumbe!
   
 19. Tabutupu

  Tabutupu JF-Expert Member

  #19
  Oct 16, 2011
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 5,650
  Likes Received: 4,412
  Trophy Points: 280
  Sikuhizi kwenye vibanda vya chipsi foleni wanaume, wadada, wakaka, etc. labda mafuta ya taa yamepanda bei. Ninavyo jua watoto wa dotcom wanajua kupika ni kaiz ya mdada mdogodogo anayeitwa hausigel. Japo hata wanaume wa sikuhizi nao vimeo. kama keo hajapika na unajua kuna mgeni , ingia jikoni watajifunza. huo ndio ukichwa wanyumba. Kuna wanaume wasio jua chochote cha nyumbani, anacho jua ni nguo ilyo nyoshwa iio wapi. Mwanamke kimeo + mwanaume kimeo =balaa.
   
 20. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #20
  Oct 16, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Mkuu, soma vizuri bandiko langu hakuna mwanamke ambae ajui kupika.

  Nimesema hivi wanawake wengi wa siku hizi hawafahamu kupika vyakula vizuri, mimi binafsi ni Mwanaume, sijui kupika baadhi ya vyakula lakini najua vyakula vizuri.

  Chakula kizuri kinajulika bana, kwanza kinavutia kwa macho pili harufu, tatu delicious..

  Kupika ni fani lazima ufundishwe kama wewe umezoe kula vyakula ili ujaze tumbo wengine tupo tofauti mkuu
   
Loading...