Hivi kwa nini Wanawake mnafanya haya dhidi ya wenzenu?

HorsePower

JF-Expert Member
Aug 22, 2008
3,612
2,566
Juzi na jana, kupitia taarifa ya hbr ya ITV nilisikia hbr ya dada mmoja aliyefiwa na mumewe ambaye likuwa anadai mirathi yake kwenye kampuni la waarabu na huyo boss wake akamtumia meseji nyingi kuwa waonane usiku kuanzia saa nne akiwa pekee yake na amuache mtoto wake mchanga ili aweze kumsaidia.

Alipojaribu kumreport kituoni (maana mazingira yanaonyesha unyanyasaji na rushwa ya ngono) alikutana na polisi (mwanamke) na huyo polisi badala ya kumsaidia yule mama (asinyanyaswe kwa kutoa rushwa ya ngono kupata haki yake) alimnyang'anya simu na kuzifuta zile meseji kuondoa ushahidi (na hii inaonyesha rushwa toka kwa yule boss.)

Matukio kama haya ya wanawake kuwakandamiza wanawake wenzao ni mengi sana na hususan maofisini ambapo maboss wanawake (baadhi yao) pia wamekuwa wakiwanyanyasa wanawake wenzao na hili limekuwa linanikera sana sana.

Naomba kuuliza swali, kwa nini BAADHI ya wanawake wanakuwa wakatili dihidi ya wanawake wenzao kwa mfano wa hapo juu?
 
Elewa walikuja duniani kwa bahati2, bila adam wasingeliubwa na MUNGU.wavumilie we auoni kunasiku ya wanawake duniani lakni ukiniuliza imewasahdia nini siwez kutanabaisha.wanayo majumuia mengi kweli kweli lakini wanajiangalia wao na matumbo yao wanasahau watoto wa mitaani na wamama walio katika hali ngumu kama wajane,..wapo wengine wamefanya miili yao mitaji ya maisha kwa hiyo usiwafikirie sana wapotezee ndio walioleta dhambi dunia for the 1time
 
Ungekuwa unamjua Mungu kama ulivyomtaja hapo juu,ungesha elewa hakuna mwanadamu aliyeumbwa kwa bahati .

Ongea kam mawazo yako binafsi usimshirikishe Mungu.
@babu blessed
 
Ni vigumu kuja na majibu ya kwa nini Wadada huwa na ukatili hasa kwa wadada wenzao , ila kwa mfano wa huyo askari na huyo Muhundi naona kama Ugumu wa maisha kwa askari wetu unaweza walazimisha wachue rushwa bila hata kuangalia thamani ya kazi yake na madhara anayoya sababisha kwa mwenzake, Haiingii akilini mtu anaye tambua wajibu wake akawa na maisha ya kawaida kutokana na kazi yake halafu asaiijali
 
adui wa mwanamke ni mwanamke mwenzake.....

Ila polisi wa bongi zao si unazijua? Kwao Mwenye hela ndo ana haki........
 
Juzi na jana, kupitia taarifa ya hbr ya ITV nilisikia hbr ya dada mmoja aliyefiwa na mumewe ambaye likuwa anadai mirathi yake kwenye kampuni la waarabu na huyo boss wake akamtumia meseji nyingi kuwa waonane usiku kuanzia saa nne akiwa pekee yake na amuache mtoto wake mchanga ili aweze kumsaidia.

Alipojaribu kumreport kituoni (maana mazingira yanaonyesha unyanyasaji na rushwa ya ngono) alikutana na polisi (mwanamke) na huyo polisi badala ya kumsaidia yule mama (asinyanyaswe kwa kutoa rushwa ya ngono kupata haki yake) alimnyang'anya simu na kuzifuta zile meseji kuondoa ushahidi (na hii inaonyesha rushwa toka kwa yule boss.)

Matukio kama haya ya wanawake kuwakandamiza wanawake wenzao ni mengi sana na hususan maofisini ambapo maboss wanawake (baadhi yao) pia wamekuwa wakiwanyanyasa wanawake wenzao na hili limekuwa linanikera sana sana.

Naomba kuuliza swali, kwa nini BAADHI ya wanawake wanakuwa wakatili dihidi ya wanawake wenzao kwa mfano wa hapo juu?

Hapa hakuna uhusiano wowote bali uhusiano wa pesa. Mtaka rushwa haangalii jinsia anaangalia kiasi gani atapata basi1
 
Back
Top Bottom