WomanOfSubstance
JF-Expert Member
- May 30, 2008
- 5,457
- 956
...ha ha ha... haki ya mungu hata mie chakula cha jirani kilikuwa kinanitoa mate kila siku ...sijui ilikuwa ni utoto? lakini hata wazungu wana msemo "the grass looks greener on the other side!"
...tukirudi kwenye sayansi ya mwafrika; ...na ile ya wale watoto wanaovimba vitumbo halafu unaambiwa "kalambishwa", au "kabemendwa" nayo imekaaje?
QM na Mbu mmenichekesha sana!
Unajua watoto huwa wana kawaida ya kukataa chakula kwao na kupenda kula kwa jirani...hasa wale wakorofi wa kula..na hii hutia aibu maana inaweza kutafsirika kuwa kwao hamna chakula!..Nadhani kama Mbu alivyosema the grass looks greener across the fence.
Kuhusu Kubemendwa ..huu ni msemo niliusikia kwa mara ya kwanza kwenye one of bongo flava songs...na baadae nikasoma kwenye makala.Sijui kama ni ushirikina as such au ni imani potofu kwamba mtoto hudhurika pale mama anapokuwa na mahusiano na mtu tofauti ( mbali na baba ya mtoto).Kama tukichambua kisayansi huwezi kuona co-relation..ila ukiangalia kisayansi..labda kama mama ni mzururaji na hajali usafi binafsi au kuangalia mwanae kwa karibu ni kweli mtoto anaweza kudhurika.Hii itatokea hata pale mama atakapokuwa mzembe kiusafi au vinginevyo hata kama hana mahusiano nje ya ndoa/mbali na baba ya mtoto.