Hivi kwa nini siku hizi nyumba nyingi kina mama ndio wenye sauti kuzidi kina baba? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi kwa nini siku hizi nyumba nyingi kina mama ndio wenye sauti kuzidi kina baba?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mshume Kiyate, Oct 24, 2011.

 1. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #1
  Oct 24, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Wana JF...
  Nimejaribu kufanya tafiti kidogo kwenye jambo hili kupitia kwa jamaa zangu wa karibu..

  Katika tafiti zangu sehemu kubwa za nyumba zetu nimeona kina mama ndio wenye sauti kubwa ndani ya nyumba ya kimaamuzi..

  Wanaume wengi tumekua hatuna sauti ndani ya nyumba zetu.

  Hata vitu vidogo kuamua utamkuta mwanaume anasema mpaka wife aje ndio takuambia..

  Hata watoto siku hizi matatizo yao wanawambia mama zao, huku wakiwacha baba zao..

  Hivi kwa nini imekuwa hivyo kina mama ndio wanakuwa na sauti kuzidi kina baba..

  Tujadili wakuu tupate kujua..
   
 2. MkimbizwaMbio

  MkimbizwaMbio JF-Expert Member

  #2
  Oct 24, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Ndio usawa wanaoulilia wakina mama. Msipo kuwa makini baadae hali itakuwa mbaya zaidi.
  Mimi upuuzi huo sina kabisa, hata vitabu vya dini vimenipa mimi mwanaume madaraka ya kuongoza famili, sasa hii democracy ya siku hizi ndani ya familia imewafanya wanaume kuwa kama mabinti.

  Plz wanaume, Tafakari na chukua hatua, Bora lawama kuliko fedheha.
   
 3. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #3
  Oct 24, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Hujapita nyumbani kwangu bwana.....
   
 4. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #4
  Oct 24, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Ni kwa sababu wanwake ndio wanotawala majumbani............. wewe hujui Paka lake jiko!?
   
 5. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #5
  Oct 24, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  CAMARADERIE.
  Nyumbani kwako kukoje?
   
 6. kukumdogo

  kukumdogo JF-Expert Member

  #6
  Oct 24, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 686
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 80
  sasa wewe upite nymbanikwako alafu utuambie sisi hapo ni kwako.
   
 7. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #7
  Oct 24, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,029
  Likes Received: 3,052
  Trophy Points: 280
  Heri lawama kuliko fedhea...demokrasia na ndoa wapi na wapi jamani?hizo elimu zenu hukohuko madarasani na maofisini siyo kwenye himaya yangu ktk ndoa takatifu..UPUUUUZI MKUBWA
   
 8. feis buku

  feis buku JF-Expert Member

  #8
  Oct 24, 2011
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 2,371
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Mwanamke si ndo nguzo ya familia jamani!!!! au imebadilishwa!?
   
 9. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #9
  Oct 24, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  Hapana sio kuongozwa na kina mama; tena mwenyewe umesema vitu vidogo vidogo; ni kweli dialy run na vitu vidogo vidogo ndani ya nyumba ni jukumu la mama; huwezi kuja kwangu kuazima pasi nikupatie ...............utamsubiri wife ama ?
   
 10. Chantel Biya

  Chantel Biya Member

  #10
  Oct 24, 2011
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  No wonder.............matatizo hayeshi kwenye hizi ndoa, kuna power struggle inaendelea.
  Hapo chini nime quote maneno hayo, niseme kabisa si yangu..........

  "The greatest asset we have in human existence is our soul growth, but somehow we have that confused with becoming powerful"
   
 11. Mtego wa Noti

  Mtego wa Noti JF-Expert Member

  #11
  Oct 24, 2011
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 2,229
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 160
  hapo nakuunga mkono...sasa anataka mpaka penseli na nguo za watoto ahusishwe baba miakwamia. baba anacheza na fatique nzitonzito bwana siyo issue za kilo moja ya sukari nyumbani...
   
 12. IGWE

  IGWE JF-Expert Member

  #12
  Oct 24, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,750
  Likes Received: 1,326
  Trophy Points: 280
  nakuunga mkono kwa 100%
   
 13. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #13
  Oct 24, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Mkuu, nimesema hata matatizo madogo madogo mpaka mke haulizwe...matatizo makubwa yote anatatua mwanamke.

  Wengi wanaume walionaswa kwenye mtego huu hawajitambui na wanapokumbushwa wanakuwa wakali sana sijui kwa nini
   
 14. figganigga

  figganigga JF-Expert Member

  #14
  Oct 24, 2011
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 14,971
  Likes Received: 6,601
  Trophy Points: 280
  sikuhisi wanawake wanawaletea kibess wanaume sababu ya limbwata.mia
   
 15. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #15
  Oct 24, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Kuna jamaa yangu mmoja wife wake kampiga marufuku kutembea hovyo baada ya kazi..

  Ukipita nyumbani kwake jioni jamaa kakaa nje na watoto wife hayupo..
   
 16. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #16
  Oct 24, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,463
  Trophy Points: 280
  mwanamke sawa na waziri mkuu
  yeye ndie mtendaji..
  wewe mwanaume ni sawa na mfalme
  sio lazima uwe bize na kila kitu
  acha waziri mkuu afanye kazi yake
   
 17. v

  valid statement JF-Expert Member

  #17
  Oct 24, 2011
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 2,737
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  wakati mwengine mume akiamua kumsikiliza mkewe, watu wa nje mnaita ANAKALIWA. Si ndo mnaita mwanaume hana sauti
   
 18. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #18
  Oct 24, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Mkuu, kuna mambo ya mwanamke kufanya nyumbani kama vile kupamba nyumba, fenicha na mambo mengine..

  Lakini ukitaka kununua nyumba au kusaidia ndugu zangu, kuwalipia hada shule au kusaidia jamaa yangu mpaka wife akubali..

  Mama anaumwa kutoa pesa mpaka wife akubali...lol..
   
 19. AMINATA 9

  AMINATA 9 JF-Expert Member

  #19
  Oct 24, 2011
  Joined: Aug 6, 2011
  Messages: 2,132
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  mama ni moyo baba ni kichwa ktk familia so moyo una nguvu kwani ukistop tu tap mtu kafa lkn kichwa ikistop mtu hafi bali anakua tu kichaa ila anaendelea kuishi
   
 20. m

  muhanga JF-Expert Member

  #20
  Oct 24, 2011
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 873
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  sishangai sana maana mtoa mada ni chatu dume! halafu mchangiaji wewe ni mkimbizwa mbio (bila shaka wakimbizwa na mkeo unaojitia kumdharau hapa) tena akikujua umelala nje!! hivi kumbe mke kuwa na sauti ndani ya nyumba ni 'crime'?? sikujua kama hilo linaweza kuwekewa mkakati na wanaume eti kabla hali haijawa 'mbaya zaidi'. vitabu vya dini enzi hizoooo vilikuwa vinamzungumzia 'mwanamume' aliekuwa anajua vema majukumu ya kuwa mume ndani ya nyumba. ck hz wanaume wengi wamepoteza hizo 'sauti' kwa sababu wanawake walio wengi ndio wanaotunza familia, sasa cjui kama mume ni suruali au majukumu. na kama ni suruali basi hata sie wanawake tunavaa!! sauti mnayoilalamikia hapa ni 'nguvu ya uchumi' kama huna kitu mfukoni unategemea umpazie nani sauti wakati pesa ni zake! nani atakubali akatafute pesa halafu wewe mume uje uzipigie kelele??? jijenge kiuchumi utaheshimika na kila mtu tena hata wanaume wenzako. usitake yale mambo ya enzi za mawe eti tu kwa kuwa you carry those suspicious bags between 2 legs and rifle without even bullets basi uwe na kibezi... that was looooong looooooong time ago!!!
   
Loading...