Kwanini siku hizi hakuna ugunduzi wa Nahau au Methali?

MAKULUGA

JF-Expert Member
Jan 21, 2011
7,171
9,383
Nimekuwa nikiuliza sana ,imekuwaje kizazi cha sasa hakigundui tena methal na nahau kama ilivyokuwa zamani! Nimetumia neno kugundua kwa kuwa nimekosa neno sahihi.

Je, ni kwanini methali ,nahau na vitendawili vyote ni vya zamani!
 
Nimekuwa nikiuliza sana ,imekuwaje kizazi cha sasa hakigundui tena methal na nahau kama ilivyokuwa zamani! Nimetumia neno kugundua kwa kuwa nimekosa neno sahihi.
Je ni kwa nini methali ,nahau na vitendawili vyote ni vya zamani!
Chips kuku na ubongo nao umekuwa broila
 
Mi nadhani sio kwamba hakuna methali wala nahau mpya za wakati huu ,zipo ila nadhani hazijarasmishwa na taasisi husika mfn;kuandikwa kwenye vitabu mbalimbali vya kufundishia.
Samahani nimekosa mfano wa kuambatanisha kwa sababu mm sio mtaalam wa lugha
 
Mkuu kama huana hata mfano mmoja maelezo yako yanatia shika!
 
Methali ni nyingi tu kama hivi;

kula nyomi.
cha mtu mavi;
paka haishi kwa msela;
wadai asali akulambe nani;
ondoka usemwe
kanzu bila kofia ni dela

hizi zote zimeshao rodheshwa baraza la kiswahili
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom