Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 92,227
- 113,584
Sawa mkuu nimekuelewa turudi kwenye mada yetu tusitoke nje, Je kwanini Ghana inatajwa kuwa ni nchi ya kwanza
kupata uhuru Afrika?
Mimi sijawahi kuitaja kuwa hivyo. Na ukweli wa mambo unaonyesha haikuwa nchi ya kwanza kupata uhuru Afrika.
Ili Ghana iwe nchi ya kwanza kupata uhuru Afrika basi itabidi hizo nchi nyingine zilizoko Afrika ya kaskazini uzihamishe na ziwe kwenye bara lingine.
Zaidi ya hapo huwezi kuiandika upya historia vile upendavyo wewe.
Na hao wanaoitaja Ghana kuwa ndo nchi ya kwanza kupata uhuru Afrika ama wanafanya hivyo kwa makusudi ya kupotosha watu na kupindisha historia au hawaujui ukweli.