Hivi kwa nini Ghana inatajwa kuwa nchi ya kwanza kupata uhuru Afrika?

Moses Kyando

Member
Mar 4, 2010
48
7
Kabla ya nchi ya Ghana kupata uhuru mwaka 1957 kuna nchi kama sita zilikwisha jipatia uhuru, Libya, Misri, Tunisia na nyinginezo zilikuwa tayari zimejipatia uhuru. Hivi ni kwa nini Ghana inatajwa kama nchi ya kwanza kupata uhuru?
 
Mkuu unadhani nchi ulizotaja za Tunisia, Misri na Libya zilipata uhuru mwaka gani?
 
mtazamo wa kikoloni huwa unapenda sana kututenga nao...lazima wanatumia maneno kama africa kusini mwa jangwa la sahara....na mengineyo ili kuweka tofauti...ukiweka nchi za kiarabu zilizo africa,Ghana sio ya kwanza.lakini hata watu wa nchi hizo wanatuona sisi ndio wa africa na wao sio...politicians wao wanajua umuhimu wa kushirikiana,sababu za kidiplomasia..na biashara na uchumi...lakini wananchi wao,ni hadithi tofauti kabisa.
 
Lakini wanasema Afrka kusini ilipata uhuru wa bendera 1910. Nilivyomwelewa Moses Kyando labda anaongelea uhuru kamili sio uhuru wa bendera. Kama ni uhuru kamili itakuwa ni nchi ya Ghana kama historia inavyosema ukiziondoa Ethiopia sijui na nchi gani tena ambazo hazikutawaliwa na wakoloni.
 
Ghana ni nchi ya kwanza Afrika kupata uhuru kamili kutoka katika mikono ya wakoloni wa kiiingereza na hio ni mwaka 1957.

Hapo waingereza wenyewe walikubali madai ya akina Kwame Nkrumah kwamba waafrika wanaweza kujitawala. Baadae mwaka 1960 Ghana ilkaitwa Jamhuri.

Tunisia ilipata uhuru wake mwaka 1956 kutoka kwa Ufaransa. Wananchi wa Tunisia wana asili ya Uturuki na wakati huo Uturuki ilikuwa ikitawala sehemu kubwa ya kusini mwa ulaya na eneo la Mediteranean na ilikuwa na utawala wao uliokuwa ukiitwa Ottoman Empire. Lakini Tunisia palikuwa na wenyeji ambao ndio zao la raisi alieondolewa madarakani kwa nguvu za wananchi bwana Zine El Abidine Ben Ali.

Libya ina historia nzito kidogo, kwanza ilijitangazia uhuru wake mwaka 1947 na baadae Italia ikaivamia Libya na kuiweka chini ya himaya yake. Baadae ikaamuliwa kwamba Uingereza na Ufaransa waiweke Libya chini ya uangalizi na mfalme Idriss akawa anatawala Libya na wakati huo ikaitwa United Libya Kingdom.

Mwaka 1956 Bwana Idriss akashauriana na mawaziri wake na wakatengeneza barua rasmi ya kupeleka kwenye baraza la umoja wa mataifa kudai uhuru wa Libya. Bwana Idriss akadai kuifanya Libya iwe mfumo wa utawala unaolingana na ule wa nchi za magharibi na Marekani.

Baadae kukagunduliwa mafuta na petroli ikawa inaipa Libya fwedha za kutosha kujikimu na huku waingereza wakijishughulisha na kujenga miundo mbinu mingi tu ambayo wanaibomoa leo hii lakini huku wananchi wengine wakisahauliwa.

Ndipo mwaka 1959 afisa mdogo wa jeshi Muammar Gaddafi akiongoza kikundi kidogo cha wanajeshi wakapindua serikali ya mfalme Idriss na kuweka sheria ya kiislamu.

Kitendo hiki kiliwaudhi sana waingereza, wamarekani , wataliano na wafaransa na ndio maana leo hii wamerudi kwa vishindo kwani wao walikuwa na wanazungumza na serikali halali ya mfalme Idriss.

Kwahio utaona kwamba katika nchi hizo zote ni Ghana peke yake ambayo inahesabika kupata uhuru kamili ambao unafanana na ule wa Tanzania kwani viongozi wake Nkrumah na Nyerere walikuwa na uwezo wa kubishana na wazungu meza moja na kujenga hoja kwamba waafrika tunaweza kujitawala.

Na kwa Afrika Ghana ni nchi ya kwanza kupata uhuru nchi zote ulizozitaja ni waarabu.
 
Misri uhuru mwaka 1923 , Libya 1951 , Tunisia 1956 , Moroko 1956
@ Raia Fulani kama wasihesabiwe sasa Afrika itaanzia wapi mpaka wake wa kaskazini ? kwani kuna nchi kama Maurtani ,Sudan, Chad etc ambazo zina wakaazi mchanganyiko tutaziweka kundi gani ? Je mipaka ya afrika iko wapi ? tufanye tuhamishe makao makuu ya CAF kutoka Qahira (Cairo) mpaka Libreville au .............
 
Na kwa Afrika Ghana ni nchi ya kwanza kupata uhuru nchi zote ulizozitaja ni waarabu.

Kwani waarabu si Waafrika? Au kuwa Mwafrika ni lazima uwe na ngozi nyeusi na uwe na nywele kipilipili?

Na katika walioanzisha OAU hakuna kabisa hao unaowaiita Waarabu?
 
Mkuu mbona tofauti ipo wazi? Soma Historia vizuri.

Waarabu ni waarabu na wana asili ya kutoka Ugiriki na wanaishi katika ulimwengu wa waarabu ambao kwa kiingereza unaitwa "Arab World" ambao umetambaa kwenye eneo la Asia magharibi na Afrika Kaskazini au North Africa ambako kuna nchi nilizozingumzia.

Waafrika ni waafrika na wana asili yao kwenye makundi kama wabantu na wambuti.

Waarabu wametokea Asia na wakaja na lugha yao ya kiarabu na dini yao ya Uislam. Walifika hadi Zanzibar ambako waliwakuta waafrika.

Sina haja ya kueleza yote kwani nafikiri unafahamu.
 
Ubaguzi runs deep!!!! Deeper than I thought!!!!

Mkuu are you serious?

Usikurupuke ukaanza "labeling" watu.

Umetaka kufahamu tofauti right? lakini kama huwezi basi ukae pembeni.

You have to have capacity thinking to go deeper in your thoughts though. It is very disturbing but it's the truth.

You shocked me out of my complacency and smugness / arrogance . I have lots of stuff to think about and it has been great to be so challenged.

This will not be very intense but very helpful and educational – try to take away a lot of positive answers."
 
Misri uhuru mwaka 1923 , Libya 1951 , Tunisia 1956 , Moroko 1956
@ Raia Fulani kama wasihesabiwe sasa Afrika itaanzia wapi mpaka wake wa kaskazini ? kwani kuna nchi kama Maurtani ,Sudan, Chad etc ambazo zina wakaazi mchanganyiko tutaziweka kundi gani ? Je mipaka ya afrika iko wapi ? tufanye tuhamishe makao makuu ya CAF kutoka Qahira (Cairo) mpaka Libreville au .............

Mkuu, unadhani mipaka iliwekwa na nani?, kwa kwanini?
 
Hili swali vile vile liliwahi kujadiliwa kwenye Yahoo answers na kutokana na kura za wachangiaji, jibu lifuatalo lilichaguliwa kama ndio jibu sahihi:

Ghana was the 7th, 8th or 9th African country to gain independence - it depends how you count them.

Ethiopia has been an independent country for at least 2000 years. It was invaded by Italy for a short time until the Italians were overthrown on 5th May 1941. It's generally regarded that Ethiopia has never been colonized and as such this makes it the oldest independent country in Africa.

Liberia which was formed on 26th June 1847. However, it was a newly formed country so it didn't gain it's independence as such. If you exclude Ethiopia then Liberia is Africa's oldest independent country.

Liberia and Ethiopia aside there were 6 countries that gained independence prior to Ghana...

South Africa - 31 May 1910 - From the UK
Egypt - 28 February 1922 - From the UK
Libya - 24 December 1951 - From Italy
Sudan - 01 January 1956 - From the UK and Egypt
Morocco - 02 March 1956 - From France
Tunisia - 20 March 1956 - From France
Ghana - 06 March 1957 - From the UK

A chronological list of independence for African countries can be found in this link
 
Afrika ni ya wote waliomo ndani yake! Tukianza ya nani alitoka wapi na nani ana asili ya wapi sijui tutafika wapi!
 
Kwani waarabu si Waafrika? Au kuwa Mwafrika ni lazima uwe na ngozi nyeusi na uwe na nywele kipilipili?

Na katika walioanzisha OAU hakuna kabisa hao unaowaiita Waarabu?

Uafrika anao uongelea Richard ni pamoja na maumbile na utamaduni. Ukiangalia katika nchi za kusini mwa jangwa la sahara utakuata tamaduni na maumbile yao yanafanana.

Mambo ya AOU ni kidiplomasia zaidi na kiuchumi lakini ukweli ni kwamba tupo tofauti sana nao.
 
Uafrika anao uongelea Richard ni pamoja na maumbile na utamaduni. Ukiangalia katika nchi za kusini mwa jangwa la sahara uatakuata tamaduni na maumbile yao yanafanana.

Mambo ya AOU ni kidiplomasia zaidi na kiuchumi lakini ukweli ni kwamba tupo tofauti sana nao.

Lakini Afrika ni bara lililo diverse. Tofauti ya kimaumbile haimaanishi wengine ni Waafrika zaidi ya wengine.

Hata wazungu nao wametofautiana kimaumbile. Hata Waasia vivyo hivyo. Wahindi hawafanani hata kidogo na Wavietnam lakini huwezi kusema Wavietnam si Waasia kama walivyo Wahindi.
 
Afrika ni ya wote waliomo ndani yake! Tukianza ya nani alitoka wapi na nani ana asili ya wapi sijui tutafika wapi!

Sawa mkuu nimekuelewa turudi kwenye mada yetu tusitoke nje, Je kwanini Ghana inatajwa kuwa ni nchi ya kwanza
kupata uhuru Afrika?
 
Back
Top Bottom