Elections 2010 Hivi kwa nini CCM haisemi kuwa itapiga vita ufisadi katika kampeni zao?

Sep 16, 2010
14
0
WanaJF, nimegundua kuwa ni CHADEMA na vyama vingine vya upinzani ndiyo vinasema kuwa vikipata madaraka vitapiga vita ufisadi. Je ni kwa sababu CCM imejaa mafisadi wengi?
 
Kwanza hata kuutaja tu ufisadi wanaogopa, sembuse kuupiga vita? CCM wamechafuka sana na watu wanajua kwamba wako wachafu. Kumbe kuuzungumzia uchafu huo ni kama kujichongea kwa watanzania. Wameamua kukwepa hiyo mada. Ukweli daima huuma kwani dhamiri inawashtaki
 
WanaJF, nimegundua kuwa ni CHADEMA na vyama vingine vya upinzani ndiyo vinasema kuwa vikipata madaraka vitapiga vita ufisadi. Je ni kwa sababu CCM imejaa mafisadi wengi?

Mkuu kitangakinyafu,kupiga vita ufisadi ni kupiga vita ccm. Siyo kwamba ccm imejaa mafisadi wengi ila ccm = ufisadi.
 
Itasemaje wakati mgombea urais wao ni kiongozi wa mafisadi? JK atasemaje atajipiga vita yeye mwenyewe. Sana sana baadhi ya maeneo anawadanganya wananchi kuwa wameshughulikia mafisadi na wahujumu uchumi, kwa mfano Lowasa na Mramba, wananchi walipiga makofi.

Alipoenda Rombo aliwaambia Warombo kuwa Mramba ni mtu safi, kesi dhidi yake ni 'geresha tu', wananchi walishusha makofi. Vivyo hivyo alivyoenda Monduli alisema Lowasa ni mtu safi, alionewa tu. Wananchi walipiga makofi.

Hiyo ndiyo CCM na kampeni zake, kama unasubiri waseme itapiga vita ufisadi, rushwa na uhujumu uchumi, subiri.

Lakini katika yote kwa mtazamo wangu wa kulaumiwa ni wananchi wanaopiga makofi ovyo hata wakitukanwa. Sielewi tatizo ni unafiki au woga.

Kwa mwanchi anayefikiri vizuri, asiye mnafiki wala mwoga, Kikwete kusema kuwa Lowasa na Mramba walionewa, ni watu safi ni matusi. Walitakiwa wamzomee Jk na kumwacha uwanjani apige blaablaa zake.

NAWAPONGEZA WANANCHI WA MBULU WALIOMZOMEA Kikwete na kuanza kuondoka alipoanza kuzungumza ubaya wa vyama vya upinzani. Hao ni wazalendo wasio na unafiki na woga.

Kwa mtaji wa woga na unafiki uliooneshwa na Warombo na wamonduli, ambao pia unaendelea kuoneshwa sehemu mbalimbali kampeni zinapoendelea hatufiki, wala tusilalamike tunapopokonywa haki zetu.
 
WanaJF, nimegundua kuwa ni CHADEMA na vyama vingine vya upinzani ndiyo vinasema kuwa vikipata madaraka vitapiga vita ufisadi. Je ni kwa sababu CCM imejaa mafisadi wengi?

Mkuu, hapo umegonga penyewe. Hawawezi kwa sababu chama kimejaa mafisadi, wakiongelea tu basi maswali yatakuja kwa nini fulani bin fulani kapitishwa ili hali ana kesi mahakamani ya matumizi mabaya ya fedha za umma na mkulu amekwenda kumnadi, etc
 
kupiga vit ufisadi ccm ni kujipiga vita wenyewe. ili ccm iendelee kuwepo sharti na mafisadi wawepo. ccm without ufisadi haiwezekani
 
WanaJF, nimegundua kuwa ni CHADEMA na vyama vingine vya upinzani ndiyo vinasema kuwa vikipata madaraka vitapiga vita ufisadi. Je ni kwa sababu CCM imejaa mafisadi wengi?

Wanatumia busara ya kawaida tu. Huwezi kukata tawi ulilolikalia kwani utaanguka na tawi lenyewe. Ufisadi ni tawi la muhimu sana kwa CCM hivyo sio busara kwao kuanza kulikata. Ila kama umefuatilia kwa makini wanazungumzia mapambano yao dhidi ya rushwa (sio ufisadi). Na wanafanya hivi kwa makusudi kwani kuna tofauti kubwa ya kimsingi kati ya rushwa wanayoongelea CCM na ufisadi wanaoongelea CHADEMA nd CUF.
 
CCM kupiga vita ufisadi ni sawa na mtu kuukata mkono wake yeye mwenyewe.
 
Nilipoangalia TBC juzi, ikimwonyesha JK akimnadi Lowasa, anayeitwa "waziri mkuu mstaafu" na watu wasijua ukweli,. Nilipoangalia nilipata impression kuwa hata watu wa Mto wa Mbu katika wilaya ya Monduli hawakufurahia kitendo cha JK kumnadi fisadi. nilisikia kama alikuwa nazomewa. Ya huko Rombo je? JK anamnadi Mramba ambaye ameshitakiwa na jamhuri kwa kiletea serikali hasara ya TZS 11b? - HIvi JK kweli zimo sawasawa; hivi kamati yake ya campign haimshauri kuhusu namna ya ku-disguise his acceptance ya mafisadi? Ya huko mbulu nimeyapata live. Marmo akipita ujue kaiba kura.
 
Back
Top Bottom