Hivi kwa mfumo huu viongozi wanakuwa wanajielewa kweli?

fenestra rotunda

JF-Expert Member
Jun 18, 2015
614
1,000
Niende moja kwa moja kwenye mada;

Tume ya taifa ya uchaguzi ilianzisha mfumo wa kusajili wapiga kura kwa alama za vidole almaarufu BVR ili kurahisisha mfumo wa uandikishaji na utunzaji wa kumbukumbu kuendana na teknolojia ya sasa.

Kama kweli tume imeweza kusajili kwa finger print na picha ya kila mmoja kuchukuliwa ikiwemo "taarifa zote muhimu",ni kwa nini sasa ishindikane watu kupiga kura popote walipo bila kujali kituo alichojiandikisha? Hiki ni kituko na kichekesho cha karne kwa wanaojielewa,haiwezekani tumeamua kutoka analogia kwenda digital system lakini mambo yafanyikayo yabaki kuwa analog.

Sasa kulikuwa na ulazima gani wa kujiandikisha kwa mfumo wa kidigitali ilhali ukifanya mambo ya analogia??Ni akili kweli?

Ukiachana na hilo, Serikali ilikuja na vitambulisho vya taifa vyenye taarifa zote zinazomuhusu muhusika,kwa style hii kulikuwa na haja gani ya kuendelea Kubaki na kadi ya mpiga kura ilhali NIDA inamaliza mchezo wote?

Tuseme nini basi;tume inafurahia usumbufu wa watu ku-update information zao regarding vituo vyao vipya vya kupigia kura? Kwamba wanapata faida gani watu wasipojitokeza kwa wingi kupiga kura ikiwa sababu ni kuwa mbali na vituo? Au tulaumu uzembe wao wa kuruhusu watu kujiandikisha mara mbinu ( na kwamba ndo sababu kubwa ya wao kutoruhusu watu wapige kura popote)?

Ni vyema wakatengeneza mfumo ambapo NIDA ndo iwe mbadala wa kitambulisho cha kupigia kura na pia kukwepa watu kujiandikisha mara mbili. Hii itasolve tatizo la kuongezwa kinyemela idadi ya wapiga kura wakati wa uchaguzi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom