hivi kuzuia maandamno ni polisi kuvunja mali,kupiga na kuua raia?

King Suleiman

JF-Expert Member
Dec 27, 2010
496
327
salaam ndg zangu,
nataka tuchambue kwa pamoja bila kujali itikadi zetu za kichama, mapenzi ya siasa au mtu. na tuchangie kwa vigezo na hoja nzuri swali hili.

mwaka 2001, nakumbuka kule zanzibar (unguja na pemba ) wananchi waliandamana kudai haki zao wakati wa utawala wa mh. Mkapa, na kilichotokea huko kila mtanzania anajua kwamba raia wasio na hatia waliuawa na wengine wengi kujeruhiwa na kukosa makazi.

siku si nyingi tumeona teana tukio la kama la Zanzibar hapo Arusha, na tumeshuhudia mchuano mkali kati ya waandamanaji na polisi wetu ambao wanaclaim kuipenda sana nchi yao na kutulinda sisi raia na mali zetu.

picha za televisheni na za magazeti zimeonyesha magari yakivuvjwa vioo na polisi na raia wanapigwa kama vile ni vita au waizi. nikapata kigigmizi na mshituko mkubwa, hivi hawa polisi wametumwa KUZUIA AU KUPIGA, KUHARIBU NA KUUA?

nilibahatika kuwa ufaransa wakati wa maandamano ya kuoinga ongeaeko la bei, maandamano yalikuwa makubwa sana (Country wide) but sikuona police wakiua au kupiga raia hovyo wao kazi yao ilikuwa ni kuhakikisha hakuna uvunjifu wa wa amani. cha ajabu hapa kwetu niliwaona polisi ndio wavunjifu wa amani na waleta fujo, kwanini nasema hivyo.
i. kulikuwa na haja gani ya kuwakamata viongozi wa upinzani wkt wa mkutano?
ii. watu wamebeba vitambaa vyeupe kuna haja gani kuwapiga, kama wamevunja sheria si wangesubiri wamalize kazi yao kisha wawafungilie mashitaka?

wote tunakumbuka kipindi cha vuguvugu la mgomo wa wafanyakazi, raisi akihutubia wazee wa CCM wa DSM aliongelea swala hilo kwa kuwatisha wananch kwamba watarudi na NGEU. hii inaamninisha kwamba viongozi wetu wanashabikia polisi kupiga rai.

demokrasia barani afrika ina safari ndefu sana, kwetu ukiwa kinyume na serikali unastahili kupigwa na kuharibiwa mali zako zaidi ya muhalifu. watawala wa kiafrika kama kwetu Tanzania wanachopenda ni kusifiwa hata kama wakifanya madudu.

Mzee mwanakijiji kwenye moj ya post zake aliwahi kuandika, " ukitaka kujenga mnara kaa chini na uhesabu gharama kwanza" sasa najiuliza hii intelijensia tuanayoambiwa ndio imetumika ilishindwa vipi kuhebu gharama za ambacho kingoke baada ya maandamano? na walikuwa wapi kuintelijensia uwizi na ubahirifu wa mali za uma? au ni intelijensia kwenye migomo na maandamano tu?

ni wito wangu serikali kwa upande wao lazima wakiri wameboronga na watu responsible wajiuzuru bila kulazimishwa na mtu balim kwa utashi wao, pia Chadema nao wajiangalie kama kuna sehemu walienda wrong na wajirekebishe kwa faida ya baadae,Jamii na vyama vingine vijifunze kwa kilichotokea Arusha na Zanzibar.

siwezi kuwa adui kwa kusema ukweli.

Suleimani.
nawakilisha.
 
Tatizo Tanzania kila kitu ni siasa,
Wakati wa vuguvugu la maandamano au mgomo wa wafanyakazi, KIKWETE ALITISHIA WAANDAAJI KWA KUWAAMBIA KUWA WAMETUMWA NA VYAMA VYA SAISA VYA UPINZANI HIVYO KAMA WANGEANDAMANA WANGEAMBULIA KIPIGO.........
NIWAKUMBUSHE KUWA SIO KILA MDAI HAKI NI MPINZANI WA SIASA HIVYO KAMA HAWATAKI DEMOCRASIA , WASIPIGE WATU OVYO KWA KISINGIZIO CHA SIASA.
 
Back
Top Bottom