Hivi kuzindua Studio ya Kituo cha Redio nayo ni kazi ya Rais, kwani Zanzibar hakuna Waziri wa Habari?

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,530
217,789
Kiukweli nimeshangazwa sana na kitendo cha Rais wa Zanzibar kushiriki uzinduzi wa kilichoitwa Studio za Wasafi FM huko Zanzibar.

Zanzibar inayojitambulisha kama nchi, inao mawaziri walioteuliwa na Rais huyo huyo, miongoni mwao yumo Waziri wa Habari, huyu ndiye alipaswa kushiriki huu uzinduzi wa Studio kama hizi.

Rais wa nchi yenye changamoto nyingi kama Zanzibar, kuacha kuhangaika na Matatizo ya Wananchi na kushobokea uzinduzi wa Wasafi FM, ni Ishara kwamba majukumu ya Urais ni mepesi sana, kwamba kwenye uzinduzi huo angehudhuria Waziri tu ama hata DC kungepungua kitu gani?

Kiongozi unaacha kuhangaika na Uchumi wa Bluu uliotuaminisha kwamba utaondoa umasikini wetu, unaanza kuhangaika na Studio za Wasela! Mbona hujitokezi kuokoa ZBC inayopumulia mashine? Viongozi wetu mbona mnatuchukulia poa sana aisee?
 
Unashangaa ya Rais !. hata idara za ujasusi zenyewe zipo bize na chama cha mapinduzi kuliko chochote mpaka washituliwe idara za nchi nyingine.

Iliniumaga kipindi cha nyuma baada ya ubalozi wa Marekani idara yao ya kijasusi kuwashtua kuwa nchini kwetu kuna magaidi na wapo mkoa wapwani wakawa wanapuuzia mpaka ilivokuja kuwa hatari zaidi hii kitu nilipata kwa Buyombe.
 
Kutokana na Umaskini tulio nao hupelekea Rais kuwa ni cheo cha kawaida sanaa.

Na hata ukifikiria Raisi wa Zanzibar akienda Uwarabuni ama nchi za ulaya hudhania ni mtu wakawaida kama raia wengine.

The statuses of a president candidate Is created by the owner.
Frequently displayed of the president in a society is reduced the value of dignity to him.

Ila sidhan mtu kama Putin ama Xi Pin anaweza sogea kwenye show zi kijinga.
 
Kuna Mambo lazima uyatazame katika picha kubwa, anachofanya Rais na CCM si kwamba hawana kazi za kufanya, anajua Diamond Kwa Sasa ndie msanii mkubwa na mwenye ushawishi mkubwa Kwa watoto, vijana na baadhi ya wazee na Siasa Ina wahitaji ao watu Kwa Asilimia 100.

Leo anacho kifanya Rais mwinyi kwenye jambo la Diamond ni kutengenezeza mahusiano ya uhakika.

Uchaguzi ujao au kwenye mambo Yao ya kisiasa atamwitaji Diamond na wasanii wengine katika kukusanya na kushawishi watu Kwaajili yake na Chama chake.

Anachofanya Kwa Sasa ni uwekezaji wa mahusiano Kwaajili ya matumizia ya baadae, JPM alitumia sana mbinu hizo.
 
Kiukweli nimeshangazwa sana na kitendo cha Rais wa Zanzibar kushiriki uzinduzi wa kilichoitwa Studio za Wasafi FM huko Zanzibar.
Mbona hukumshangaa huyu ambaye alikuwa mpk anagalagala kwenye mawe? Jiweeeee! H

Huyu mtu was a disgrace to our nation.
20221213_071750.jpg
 
Kwani huyo si sawa sawa na mkuu wa mkoa tu huku Tanganyika..ana hadhi hiyo wala usihofu.

#MaendeleoHayanaChama
 
Mbona yule mtu mbaya alikuwa anazindua mpk vyoo vya stendi. Mmesahau mara hii?

Sukuma gang bwana! Sasa unataka kusemaje?

Like jitu baya lilikuwa linazindua mpk grocery halafu unataka kusema nn hapa?
Si bure kuna maruhani na mizimu ya hayati inakutafuna. Bila shaka kuna namna ulimfanyia ubaya, yanakurhdia. Kutwa kucha sentensi zako ni kulaani kusicholaanika.

Uzi hauhusiani na marehemu wewe unakurupuka kumtukana kama vile yeye ndiye kuuanzisha. Tafadhali fanya kazi utajikwamua kiuchumi, kama unapenda siasa Leta siasa za kujenga si za kubomoa kama ufanyavyo.

Haiingii akilini mda wote uko mitandaoni kulaani na kuleta uzushi kwa mtu ambaye hayupo na hatarudi. Vinginevyo mizimu yake inakutesa si bure. Badilika.....
 
Nitapambana na maiti hii mpk naenda kaburini. Na ninavyopambana naye ndiyo napata raha Sana. Hapa ulivyojibu ndiyo najua tusi langu limefika kwa walengwa (wafuasi wake kama wewe).
We mwehu kweli maiti iko chato huku Jamiiforum imefuata nini!?
Cha kukusaidia nenda ukaifukue uifanye unavyotaka uridhike wafuasi wake wanazidi kuongezeka kila uchao
 
Si bure kuna maruhani na mizimu ya hayati inakutafuna. Bila shaka kuna namna ulimfanyia ubaya, yanakurhdia. Kutwa kucha sentensi zako ni kulaani kusicholaanika.

Uzi hauhusiani na marehemu wewe unakurupuka kumtukana kama vile yeye ndiye kuuanzisha. Tafadhali fanya kazi utajikwamua kiuchumi, kama unapenda siasa Leta siasa za kujenga si za kubomoa kama ufanyavyo.

Haiingii akilini mda wote uko mitandaoni kulaani na kuleta uzushi kwa mtu ambaye hayupo na hatarudi. Vinginevyo mizimu yake inakutesa si bure. Badilika.....
Hiyo picha ni ya dadako? Siyo picha yake? Sasa unalalama nn?

Huyu jamaa ameinajisi nchi kiasi cha kutisha. Ndiyo maana mzee Makamba amehitimisha kwa kusema watu wabaya hawaishi (Sasa kazi kwako, akili mkichwa).
 
Kiukweli nimeshangazwa sana na kitendo cha Rais wa Zanzibar kushiriki uzinduzi wa kilichoitwa Studio za Wasafi FM huko Zanzibar.

Zanzibar inayojitambulisha kama nchi, inao mawaziri walioteuliwa na Rais huyo huyo, miongoni mwao yumo Waziri wa Habar , huyu ndiye alipaswa kushiriki huu uzinduzi wa Studio kama hizi.

Rais wa nchi yenye changamoto nyingi kama Zanzibar, kuacha kuhangaika na Matatizo ya Wananchi na kushobokea uzinduzi wa Wasafi FM, ni Ishara kwamba majukumu ya Urais ni mepesi sana, kwamba kwenye uzinduzi huo angehudhuria Waziri tu ama hata DC kungepungua kitu gani?

Kiongozi unaacha kuhangaika na Uchumi wa Bluu uliotuaminisha kwamba utaondoa umasikini wetu, unaanza kuhangaika na Studio za Wasela! Mbona hujitokezi kuokoa ZBC inayopumulia mashine? Viongozi wetu mbona mnatuchukulia poa sana aisee?
Aisee hii nchi ya kikuda kichizi yaan raisi wa nchi unaenda kwnye uzinduz wa kituo cha redio Tena kituo kidogo Cha mtu binafsi, sijui tumerogwa na nani?!
Huu upimbi kweliii
 
Back
Top Bottom