Hivi kuvuta sigara hadharani bado ni habari

kalamu ya chuma

JF-Expert Member
Jan 22, 2014
214
225
wana jf,
miaka kadhaa iliyopita kwa serikali yetu hiii hii wabunge wetu walipitisha sharia ya kutovuta sigara hadharani,napenda kujua hivi sharia hii bado inafanya kazi na inafuatwa? Juzi nilikuwa kwenye daladala mtu mmoja abiria alikuwa anavuta sigara mpaka kero nilijaribu kumuonya haikuwezekana,na abiria wenzangu walinyamaza kimya na hapo nikaona fursa ya kutoa elimu kwa umma juu ya madhara ya mvutaji wa pili ,nilipata upinzani sana na wengi walisema ni haki na uhuru wa mtu kujiamlia mambo yake mwenyewe.
Nilipata nafuu sana pale huyu abiria aliposhuka kituo cha mission mbagala,kiukweli nikakumbuka bunge liliwahi kupitisha sharia juu ya uvutaji sigara hadharani,hivi sharia hii ipo na inafanya kazi sehemu zipi hasa? maana huku mitaani hali ni mbaya,watu tunameza na kuvuta hewa ya sigara kila siku.
Naombeni mwongozo
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom