Hivi kuvalishana pete za uchumba ni lazima kuwe na wageni waalikwa pamoja na sherehe?

Watanzania wanapenda kula kula yaani tukio lolote lile wanawaza kula na kunywa. Majuzi napokea mwaliko na kuombwa mchango kutoka kwa miongoni mwa ndugu zangu kuwa Mama mkwe anakuja kulea wajukuu!!

Yaani mtu kaja kwa interest zake tena kuona wajukuu zake tena imekuwa sherehe ya kukusanya mamia ya watu!
Unaishi uswahilini sana
 
Kuvishwa pete tumeiga kwa watu huko na wenyewe wanafanya surprise hata kusipokuwa na ndugu..sisi huku hadi ubwabwa unapikwa kisha binti anaulizwa"Will you marry me?"..unafki mtupu.
Haulizwi bwana, ila ni ishara kuwa kawa mchumba wa mtu. Ndomaana mahari inalipwa then anaveshwa tuspotoshane tafadhali
 
Umeshawahi kuhudhulia ndoa za kibongo? Kina nani wanajazana kwenye sherehe kama si wapambe na marafiki? Utashangaa mtu anapata kadi anaalika rafiki yake waende kwenye mnuso.

Mleta mada anataka kukwepa watu wote including ndugu ndo maana alisema "... au naweza kumuita ghetto tu nikamvalisha na mchezo ukaisha?" Au ndugu wanaruhusuiwa kuja ghetto?
 
Haya mambo ya kuvalishana sijui pete za uchumba, sisi vijana wa zamani hatukuwa nayo. Hata hivyo tusipende kuiga kila kitu Wazungu wanafanya. Mwishowe tunaonekana malimbukeni na mazuzu.
 
Mvalishe hata sehemu tu yenye watu wengi kwa kumshitukiza kama una ujasiri, sehemu kama vile kazini, sokoni nk (yaani kiufupi sehemu zile zenye watu wengi)

NB:Fanya hivyo kama una uhakika anakupenda kweli, kama anakuigizia mapenzi anaweza akakuacha solemba mbele za Raia na hivi hauna hata usafiri private, utakuwa unatembea kuondoka eneo la tukio huku unatamani upotee gahfla tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom