Hivi kuvalishana pete za uchumba ni lazima kuwe na wageni waalikwa pamoja na sherehe?

kyanyangwe

Senior Member
Oct 31, 2018
137
500
Hello wakuu.

Nina mpango wa kumvisha pete mtarajiwa wangu. Swali langu ni je, lazima kualika watu au naweza kumuita ghetto tu nikamvalisha na mchezo ukaisha?

1625995925462.png

 

Mbao za Mawe

JF-Expert Member
May 11, 2015
23,349
2,000
Watanzania wanapenda kula kula yaani tukio lolote lile wanawaza kula na kunywa. Majuzi napokea mwaliko na kuombwa mchango kutoka kwa miongoni mwa ndugu zangu kuwa Mama mkwe anakuja kulea wajukuu!!

Yaani mtu kaja kwa interest zake tena kuona wajukuu zake tena imekuwa sherehe ya kukusanya mamia ya watu!
 

Carleen

JF-Expert Member
Nov 6, 2018
4,893
2,000
Ingependeza zaidi mngevalishana mbele ya madhabahu kama ninyi ni wakristo, naamini jambo lenu lingekuwa na baraka za Mungu zaidi, suala la mambo ya sherehe huwa si muhimu lakini sidhani kama kuna mzazi wa kibongo atakubali hili..!!
 

TJ360

JF-Expert Member
Mar 25, 2019
231
1,000
Kuvishwa pete tumeiga kwa watu huko na wenyewe wanafanya suprise hata kusipokuwa na ndugu..sisi huku hadi ubwabwa unapikwa kisha binti anaulizwa"Will you marry me?"..unafki mtupu.
Afadhali somebody said this. Wabongo sijui nani kawaroga.
 

Castr

JF-Expert Member
Apr 5, 2014
24,475
2,000
Siyo lazima sherehe.

Mtoe out. Kokote.

Muwe mmekaa au mmesimama.

Muelezee kwanini unaona yeye na wewe ni sahihi kuishi pamoja milele na kuoana.

Sababu zako zisiwe "Una matako makubwa na chuchu konzi" "Una hips zinavutia macho na unanimaliza on bed" they shouldn't base kwenye muonekano in fact kama unataka kumuoa kwaajili ya matako, kiuno au hips nakushauri temana naye.

So ukishamuelezea hizo sababu muulize kama anajisikia the same, akikubali, chomoa pete mvishe. Kazi imeisha. Nakuhakikishia ndani ya nusu saa utapigiwa simu kugewa hongera na hata hakuna uliyemuambia mpango wako.

Huu mtindo wa kusurprise wenza wetu (ingawa kwa Tz nadoubt kama ni surprise) unampa presha mwenzako mbele za watu ya kujibu "Ndiyo" kwa kuhofia kukudhalilisha mbele ya watu na kuona watu watamuonaje.
 

Mac Alpho

JF-Expert Member
Aug 5, 2019
3,486
2,000
Gharama mkuu, maana wageni lazima watafune vyuku na vinywaji.
Mvalishe hata sehemu tu yenye watu wengi kwa kumshitukiza kama una ujasiri, sehemu kama vile kazini, sokoni nk (yaani kiufupi sehemu zile zenye watu wengi)

NB:Fanya hivyo kama una uhakika anakupenda kweli, kama anakuigizia mapenzi anaweza akakuacha solemba mbele za Raia na hivi hauna hata usafiri private, utakuwa unatembea kuondoka eneo la tukio huku unatamani upotee gahfla tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom