Hivi kutoa misaada kwa miradi ya wananchi ndio kiwe kigezo cha kuwa kiongozi wa umma? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi kutoa misaada kwa miradi ya wananchi ndio kiwe kigezo cha kuwa kiongozi wa umma?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mechard Rwizile, Jan 11, 2012.

 1. m

  mechard Rwizile JF-Expert Member

  #1
  Jan 11, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 938
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 80
  Taifa hili linaelekea kupoteza mwelekeo wa maendeleo kabisa na inaelekea kama CCM haitaendolewa madarakani katika uchaguzi wa mwaka 2015, tutapotea kabisa kama Somalia. Mwanzoni mwa miaka 80, nchi kama Somalia ya Siadi Bare na Zaire ya Mobutu zilitawaliwa sana na ufisadi kama tunaouona hapa Tanzania kwa sasa hivi. Wananchi wa nchi hizo walilalamika lakini hawakuchukua hatua za kutosha kuziondoa tawala hizo kwa njia ya kura. Wapo waliodhani, watawala wao watajirekebisha na wapo waliosema hata wapinzani wao wakiingia madrakani watafanya hayo hayo na hiyo ikawa sababu ya kutojihusisha na masuala ya siasa. Walikosea sana; nasi tutakosea endapo hatutachukua hatua ya makusudi kuiondoa CCM madarakani kwa njia ya kura.

  Woga wangu unatokana na hali inayojionyesha sasa kwa kila anayetaka madaraka katika chaguzi zijazo kuanza kutoa misaada kwa njia ya kuchangia miradi ya maendeleo. Viongozi hata wa kidini wameishajua namna ya kupata fedha kiurahisi, ni kuitisha harambee na kumkaribisha kiongozi ambaye wamesikia anapania uongozi wa umma. Katika hatua ya utambulisho atamwagiwa sifa utadhani labda kafa. Kumbe la, wanataka fedha yake. Naye kwa uroho wake utasikia mimi na rafiki zangu tumetoa milioni kadhaa! Watu wanapiga makofi.

  Uchaguzi ukifika utaanza kusikia nilichangia mradi fulani na fulani kwa kuwa ninapenda maendeleo ya watu. Wapembe wao ndio wanakuwa wa kwanza kuwauliza wapinzani wao wamechangia nini katika maendeleo? Ukisema niliandika kitabu kuhusu kilimo bora, nakadhalika, utaulizwa kitabu kimetusaidiaje? Utazomewa tu !

  Ndugu zangu tufanyeje kuliokoa Taifa letu katika hii safari ya kuelekea Somalia? Hivi ni haki uwezo wakuchangia fedha kiwe kigezo cha kuwapata viongozi wa umma?
   
 2. kingadvisor

  kingadvisor Senior Member

  #2
  Jan 11, 2012
  Joined: Dec 21, 2011
  Messages: 109
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
   
Loading...