Hivi kushika bango linaoonyesha hisia zako ni kosa kisheria?

Mapambano Yetu

JF-Expert Member
Aug 14, 2012
1,121
2,064
Yawezekana wengine hawatanielewa, lakini swali langu hasa ni kwa wale wanaoandaa mabango hasa pale Mtu mkubwa anapokuwa ziarani au kwenye public.

Kuna mtu amekasirishwa na bango kule kigoma na baada ya kuongea kuwa hilo bango hata lisoma nimeona wanausalama wanamvaa huyo kijana na kuondoka naye. Haijaeleweka kapelekwa wapi maana hata huyo aliyekasirishwa alitoa kauli yenye utata kuwa "Wengine mnajitafutia matatizo"

Hapa ndo tulipofika watanzania, wanaochekelea chekeni lakini tunakoelekea sio kuzuri.
 
nikajikuta nauliza kimoyomoyo; Alipitia wapi hadi kufika karibu na mkulu na bango lake bovu?? Basi, lets say, hata huyu mkulu sio safe kabisa. Walinzi mlikuwa wapi hamku muona huyu kibaraka??
 
Hio ni ishara jinsi wananchi walivyo na machungu moyoni.huyo jamaa kawakilisha vile watu wanavyohisi.hali ni tete.
 
Kubeba bango sio kosa. Hiyo ni freedom of expression ambayo imewekwa na katiba ya JMT. Bango linaweza kuwa la kufikisha ujumbe au kutaka ufafanuzi wa kitu flani, au kutoa maoni flani. Bango baya ni lile linaloamsha mihemko ya uchochezi. Aliye na picha ya bango hilo atuwekee hapa
 
Back
Top Bottom