Hivi kupata leseni ya biashara ni mpaka uwe na Tax clearance?

Kuna tofauti gani kati ta kusajiri biashara na jina la biashara
Kusajiri biashara na jina la biashara ni Vitu viwili tofauti.
Kwa mfano Kama unataka kuuza madawa ya mifugo na vyakula vya mifugo, unaweza kusajiri jina lako la biashara brela mfano, FELIX VETENARY CENTRE.. Hapo utakuwa umemaliza brela

baada ya hapo ukaenda almashauri wakakupa lesen iliyo andikwa jina hilo.

Sasa kusajiri biashara Kuna anzia hapaa..., Madawa na vyakula vya mifugo viko chini Wizara ya mifugo. So unatakiwa kwenda ofcn kwao kusajiri biashara yako.

Utaenda watakupa form utailipia shs 10,000. Badae utafanya maombi ya kuomba kusajiriwa yaan Wizara ikutambue. Utalipia helf 40, uta ambatanisha na Lesen yako, na tin number, na mchoro wa ofc yako. Badae watakupa certificate utakuwa umesajiriwa biashara yako. Hipo mifano mingine tu watakupa wakuu hum.
 
Jitahidi kabla ya kuongea au kuandika kitu uwe na uhakika nacho tofauti na hapo unajicholesha mbele ya watu.

Una uhakika kweli brela hawatoi lessen? Kama hujui sema tukusaidie
Ok, baada ya kwenda kwenye website yao, wanatoa Industrial licence. My shortcoming. Satisfied ?
 
Upo sahihi kabisa, wanatoa haswa kwa makampuni na nikishawahi kuomba, wana system moja hv ya serikali nimeisahau kidg, ila biashara zingne unachukulia leseni halmashauri husika.
Lesen zote zenye sura ya kimataifa kama vile export and import tangu zaman zilikuwa zinatolewa na Wizara ya viwanda na biashara. Lakn badae wamekasimisha mamlaka kwa brela kuzitoa. Hii sijasimuliwa Bali mm mwenyewe ni ndau wao tangu 2013
 
Ok, baada ya kwenda kwenye website yao, wanatoa Industrial licence. My shortcoming. Satisfied ?
Still bado hajapata majibu Tosha. Leo hii ukitaka kupeleka bidhaa zozote nje au kuingiza ndan ya tz. Ni brela pekee ndo watakupa lesen
 
Upo sahihi kabisa, wanatoa haswa kwa makampuni na nikishawahi kuomba, wana system moja hv ya serikali nimeisahau kidg, ila biashara zingne unachukulia leseni halmashauri husika.
Watu wasuchojua ni kuwa kuna leseni daraja A na B..leseni daraja A zinatolewa Kwenye biashara/kampuni zinazofanya biashara yenye sheria/sera za kitaifa mfano huduma za mikopo,hospital,import naexport nk hawa wote wana apply leseni zao wizara husika sema now brela ndo anatoa leseni hizo miaka miwili sasa..

Leseni daraja B zinatolewa na halmashauri..zinatolewa Kwenye biashara ambazo haziendeshwi na sheria mama za kitaifa mfano saloon,duka la vifaa vya ujenz nk
 
Naombeni ushauri kuendesha biashara kawaida au kuisajili Kama kampuni labda kwa malengo ya kukua badae, ushauri Sasa nikisajili kampuni biashara ikiwa Bado ndogo ipi faida na hasara yake. Msaada plz
 
Labda nitoe ufafanuzi kwa uelewa wangu mdogo

-Leseni ya biashara inatolewa na halamshauri husika
-Leseni ya viwanda vya kati na vikubwa inatolewa BRELA
-Jina la biashara linasajiliwa BRELA
-Nembo ya biashara inasajiliwa BRELA
-Kampuni inasajiliwa BRELA

Huwezi kupata nembo ya utambulisho wa biashara hadi uwe na jina la biashara
 
Back
Top Bottom