Hivi kununua product za kigeni tunaipenda nchi yetu?

Snitch

Senior Member
Oct 22, 2011
165
42
Leo nimeona nijikite kwenye mambo ambayo Kama tukiendelea ku criticize kila kitu mwisho wake tutakua tinazalisha taifa lalamishi na nisilotambua wajibu wake kwa Taifa na kutegemea nchi tu itufanyie kila kitu...
Ni kawaida kwa Mtanzania kwenda dukani akaamua kununua Ommo badala ya FOMA Au ni rahisi kwa Mtanzania wa sasa kusema matunda ya Bagamoyo hakuna kiwanda Au Machungwa ya Muheza tanga hayana kiwanda na kulaumu serikali je kikijengwa kiwanda niwangapi tutaacha Juice ya Ceres Au Delmonte na kununua juice ya Muheza?

Tinatakiwa kuanzisha movement ya kupenda vya kwetu hata hao waliofikia hatua ya juu ya ubora nikutokana na support kubwa ya ndani halafu wanje nao watapenda.

Nimeshawishika katakana nawengi kutotambua mchango wetu ktk ujenzi wa taifa na kwenda kupeleka mchango wetu mdogo kwenye nchi jirani Au nje kwa either ignorance Au kutopata elimu ya uraia na uzalendo

We zetu hata kuongea lugha tu ya kigeni ameona anaidhalilisha lugha yake ila sisi tunanunua Hadi bidhaa I think we need to wake up and start this movement.

Mfaransa umepotea tu muulize excuse me do you speak English atakuuliza Excuse me do you speak French je bidhaa atanunua yakwako?
Tujifunze kupenda vya kwetu Hongera Azam na wengineo wajasiria Mali
 
una akili sana wewe,
mi sasa hivi nimetoka kariakoo kununua simu - made in Tabora,
pia nimenunua tyre road ends za fuso made in Kibaha.
 
.......
Mfaransa umepotea tu muulize excuse me do you speak English atakuuliza Excuse me do you speak French je bidhaa atanunua yakwako?
Tujifunze kupenda vya kwetu Hongera Azam na wengineo wajasiria Mali

na mtanzania ukiongea naye kiswahili utasikia ....akichuale ....mmmmmmh! napenda ...mmmmmh!.........egichopu
na........waini yu no?
 
Leo nimeona nijikite kwenye mambo ambayo Kama tukiendelea ku criticize kila kitu mwisho.......... Mfaransa umepotea tu muulize excuse me do you speak English atakuuliza Excuse me do you speak French je bidhaa atanunua yakwako?
Tujifunze kupenda vya kwetu Hongera Azam na wengineo wajasiria Mali
wewe ndo wa kwanza kutopenda bidhaa za tanzania. kama hata lugha tu unatumia ya wazungu. je bidhaa?
na simu ama kompyuta unayotumia imetengenezwa wapi hapa tz?
 
Mi nipo mpakan na kenya na 90% ya bidhaa ni za kenya.... Xo niache kununua coz ni za kenya thn niingie cost nifuate bidhaa za tz mbali whle za karibu zipo,tena bila uhakika wa kupatikana hiyo commodity ya tz? Why keeping a cow while you can get free milk?
 
Leo nimeona nijikite kwenye mambo ambayo Kama tukiendelea ku criticize kila kitu mwisho wake tutakua tinazalisha taifa lalamishi na nisilotambua wajibu wake kwa Taifa na kutegemea nchi tu itufanyie kila kitu...
Ni kawaida kwa Mtanzania kwenda dukani akaamua kununua Ommo badala ya FOMA Au ni rahisi kwa Mtanzania wa sasa kusema matunda ya Bagamoyo hakuna kiwanda Au Machungwa ya Muheza tanga hayana kiwanda na kulaumu serikali je kikijengwa kiwanda niwangapi tutaacha Juice ya Ceres Au Delmonte na kununua juice ya Muheza?

Tinatakiwa kuanzisha movement ya kupenda vya kwetu hata hao waliofikia hatua ya juu ya ubora nikutokana na support kubwa ya ndani halafu wanje nao watapenda.

Nimeshawishika katakana nawengi kutotambua mchango wetu ktk ujenzi wa taifa na kwenda kupeleka mchango wetu mdogo kwenye nchi jirani Au nje kwa either ignorance Au kutopata elimu ya uraia na uzalendo

We zetu hata kuongea lugha tu ya kigeni ameona anaidhalilisha lugha yake ila sisi tunanunua Hadi bidhaa I think we need to wake up and start this movement.

Mfaransa umepotea tu muulize excuse me do you speak English atakuuliza Excuse me do you speak French je bidhaa atanunua yakwako?
Tujifunze kupenda vya kwetu Hongera Azam na wengineo wajasiria Mali

Hivi hicho kifaa ulichotumia kutuma ujumbe humu Jf ni made in wapi? Na hizo nguo ulizovaa zimetengenezwa wapi?
 
Umeleta hoja nzuri. Tatizo kubwa la bidhaa za tz ni viwango. Tatizo haliko kwa walaji wa tz bali watengenezaji wa bidhaa za tz. Tbs ipandishe viwango vya bidhaa za tz watakaoshindwa kuvifikia wasiruhusiwe kuzalisha. miaka ya 1985 hadi 2000 watz walipenda mziki wa kongo lakini sasa tupo nyumbani zaidi, je kuna mtu alituambia tuache muziki wa kongo? tuliacha wenyewe baada ya kuona chetu ni kizuri.
 
Well said mkuu. Tuanze na kusisitiza ubora wa bidhaa tunazotengeneza sisi wenyewe. Karatasi ya chooni tu ukiifungua sijui inatoa unga/chengachenga mpaka unapata mashaka kama kweli uitumie, na katikati huchelewi kukutana na kipande kikubwa kama shuka na hakina hakijulikani kina shepu gani! Huu ni mfano mdogo tu.
 
Shida ni viwanda vyetu na ubora wa bidhaa wanazozalisha,viwanda vingi vya bidhaa za chakula ni vya Waindi na wengi wao wana scandal nyingi katika uzalishaji wa bidhaa zao na uagizaji wa raw materials,natumaini wengi wetu tumeshasikia au kusoma tuhuma mbalimbali za akina Mohamed Enterprises,Zacharia and many more.
 
kama nafahamu mwenye kiwanda fulani ni raia wa nje anawanyanyasa wafanyakazi wazawa na kuwalipa/kuwadhurumu fedha zao, halfu ni mkwepaji mkubwa wa kodi kwa kuhonga wakubwa.. Unataka nikanunue bidhaa yake kwa uzalendo upi alionao? Hapana, nitamuunga mwenye mapenzi mema na nchi yangu
 
Nitoe shukrani kwa wote walioelwa positively na wale pia walioelewa tofauti ipo siku wataelewa na kuniunga mkono kwa kwenda dukani na kununua foma badala ya Ommo. Wataniunga mkono kwa kwenda Shoprite na kutoa maoni kua Tunahitaji Product za Tanzania,wataniunga mkono kwa kupenda cha kwetu hata kwa ubora mdogo wenye mashaka kwa lengo la kujenga Uwezo kubwa Zaidi ni kununua na kukosoa kwa lengo la kujenga na si kukatisha tamaa...

Hata mtoto anza kusema hasemi moja kwa moja ila taratibu ila silisemi hili kwa maana ya ku compromise standard Hapana nalisema hili kwa maana ya kutaka kujenga na kuwatia Moyo waliothubutu na kutoa mchango wao ktk sekta mbali mbali.

Wako waliosema tuangalie TBS na kuhakikisha wanakua makini na objective katika kuset standard na watoke maofisini na kufanya tathmini kujua nini mahitaji ya nchi in the next 5 to 10 years na ni sekta ipi inahitaji kutiliwa mkazo na inaashiria kukua na kuwa shindani kimataifa.

Lakini cha msingi ni kwamba hoja imepata wachangiaji nijukumu langu kuhakikisha napokea mawaZo tofauti na nakuangalia hoja zote.
 
Back
Top Bottom