Hivi kunatofauti gani ya uteketezwaji wa budget ya taifa na budget za majumbani kwetu?

mitale na midimu

JF-Expert Member
Aug 26, 2015
10,158
2,000
Uthibitisho kwamba tanzania haina pesa kabisa huwa unaonekana siku ya kufunga budget ya mwaka Unaoisha...
Na hii hali huonekana kwenye maisha ya Kila siku ya mtanzania katika ujenzi wa nyumba, matumizi na mipango ya Shule, sherehe, misibani, kilimo, biashara kote huko wengi huendesha shughuli Bila kuwa na pesa za kutosha wakati mwingine wanaanza Bila kujua watapata wapi pesa ya kumaliza.

Nilimsikiliza Prof wa uchumi ngowi anaonyesha kushangaa ulazima wa budget kuongeza Kila mwaka wakati hata ya mwaka uliopita ilikuwa chini sana katika uhalisia wake...

Nikajiuliza Kuna kikao kimoja cha budget uswahilini kwetu mtu mwenye ushawishi alikuja na budget ya 20Mil ili huo mradi au tukio lifanikiwe tena akitegemea tutumie vyanzo vilevile vya mapato. Wananzengo(lahaja ya Kanda ya ziwa) tukasema hapana, ile budget ikashushwa na kupruni vitu kibao hadi Ikabaki Mil8 na tukio likafanyika kwa gharama chini kidogo ya 8Mil.

Kinachoniuma na kinachoendelea kuniuma ni kupanga budget hasa Ile ya kilimo alafu mwisho wa mwaka unagundua ni 2% tu ndio ikipatikana huku 98% ya kilichopangwa hakikupatikana....

Najaribu kulinganisha uhalisia wa budget ya Tanzania ktk tanzania na budget ya mambo yetu huku uswahilini naona nyota...

Kuna jambo lolote la kimaisha la kujifunza kutoka kwenye upangwaji na uteketezwaji wa budget yetu ya Kitaifa.

Note kwa sababu sio jukwaa la siasa, naomba tusichangie kisiasa zaidi....
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom