Hivi kuna Wilaya inaipiku Liwale kutotembelewa na Viongozi wa Kitaifa?

Ni matumaini yangu mu wazima..!?

Hizi wilaya zetu pamoja na changamoto za miundo mbinu ya barabara kuna ulazima wa viongozi wa kitaifa kufanya ziara ikiwezekana mara baada ya mara. Lakini hali ikiwa hivi kama ilivyo huko wilayani Liwale inaleta shida katika utendaji wa baadhi ya watumishi wa ngazi za juu ktk halmashauri. Hufanya kazi kiholela kwa kujua viongozi hawawezi fika huko...!

Jambo hili ni huko Liwale tu au kuna wilaya zingine zina changamoto hii??
Kuna wilaya inaitwa Rorya hii ndio inaongoza
 
Kuna wilaya inaitwa Rorya hii ndio inaongoza
Kusema ukweli sio sawa na wala sio haki. Yaani ndani ya miaka 5 Raisi, au makamu wake, au waziri mkuu wanashindwa kufika wilayani kweli??? Basi hata waziri??? Nchi hii hii? Au tulidanganywa kuambiwa nchi ni moja eeh?
 
Isee..! Very sad. Basi hizi tozo jamani wazipeleke huko. Ila wasiokuana huruma wanazipinga hizi tozo eti jamani...
Haitaji hizo tozo ndugu, hebu jiulize kwanini hali kama hii huwezi kuikuta sehemu zingine kama Kikimanjaro na sehemu zingine je huko wanakatwa hizo tuzo
 
Haitaji hizo tozo ndugu, hebu jiulize kwanini hali kama hii huwezi kuikuta sehemu zingine kama Kikimanjaro na sehemu zingine je huko wanakatwa hizo tuzo
Kwa hiyo hakuna equal distribution of national cake sio?
 
Waziri mkuu alifika miaka mitatu nyuma kama sijakosea. Pia waziri wa maji amefika hapo karibuni na kutibua sana viongozi wazembe kwenye sekta yake hiyo.
Pongezi kwao kwa kufanya ziara. Yaani kwenye wilaya mfano wa hizi akipita kiongozi wa kitaifa lazima akite madudu. Hivyo ziara zao zina mchango mkubwa ktk kurekebisha mambo. Bila shaka huu uzi watakua wameusoma na wamepata wazo...
 
Kwani na wao si walipiga kura?? Kwenda japo hata kuwashukuru ni uungwana pia
Huwa hakuna ziara za kushukuru wapiga kura. Ziara zote huwa ni za kikazi. Akienda waziri Mkuu kwa ziara ya kikazi inatosha kabisa.

Kwanza hizi ziara ni kumaliza hela tu.
 
Huwa hakuna ziara za kushukuru wapiga kura. Ziara zote huwa ni za kikazi. Akienda waziri Mkuu kwa ziara ya kikazi inatosha kabisa.

Kwanza hizi ziara ni kumaliza hela tu.
Kwa hiyo wasifanye ziara za ufuatiliaji? Huko kwenye hizo wilaya wanapelekewa fedha za maendeleo kila mwaka. Na kuna miradi inatekelezwa huko, kwa hiyo hizo fedha na hiyo mirafi haifuatiliwi utekelezaji wake??? Ukisema gharama, gharama haiepukiki kinachoangaliwa ni natija ya ziara. Ziara isilete hasara ukilinganisha na returns zake
 
Back
Top Bottom